tatizo hapa AshaDii umesema yooote, kila nikitafuta nipite wapi hata sipaoni..... kila angle umeigusa.
labda ninaloweza tu kusema, kwa wadada ambao waoga wa kuvunjwa mioyo yao kama mimi, delaying technique inasaidia sana kupepeta nafaka. ni mtu aliyekuwa na nia nawe tu anaweza kuvumilia story za kesho/siku nyingine/nado nafikiria........ kwa muda mrefu, otherwise kama ndo kwa matamanio tu wengi wanamwagika njiani...
kuna hilo swala ameliongelea
kabanga la mitego........ na kuna siku niliwahi kumsikia rafiki yangu
BAK anaongelea kitu inaitwa kujipitishapitisha......... wakaka wengi sana wanajificha kwenye hii kitu (nadhani nahitaji sana elimu kuhusu hili, limegoma kabisa kuingia akilini kwangu)