Kwanza kabisa nitangaze interest yangu mimi ni muumini wa mpira wa pasi zote ndefu na fupi na matokeo uwanjani yaonekane.Kwa miaka mingi sana yanga imekua na utamaduni wa kutumia pasi ndefu na mashambulizi ya kushitukiza(counter attack) lakini kwa bahati mbaya kwa miaka ya hivi karibuni kama sio yote wamekosa kikosi imara na sahihi cha kuendana na mfumo huo kitu kinachopelekea timu kuonekana inacheza hovyo hovyo na kupata matokeo ya kubahatisha(mpapatu papatu),aidha kwa miaka mingi yanga imekua inapata wachezaji ambao uwezo wao ni mdogo wengine hata kupokea mpira ni shida,kupiga pasi sahihi na eneo sahihi,kwa wakati sahihi ni shida achilia mbali uwezo wa kuliona lango,uwezo wa kukimbia na mpira(dribling).
Hivyo basi niwakati mwafaka uongozi wote kwa ujumla kuja na mbinu nyingine ya uchezaji ambayo itaendana na aina ya wachezaji waliokua nayo na kila kocha atakae kua amepewa kandarasi kukinoa kikosi lazima aufuate huo mfumo hata kama atakua na mbinu zake lakini zisicheze mbali na mfumo huo.Timu imekua haina uwezo wa kumiliki mpira kitendo kinachopelekea hata pale timu inapokua imetangulia basi hupoteza umiliki mpira na kuipa faida timu pinzani ya kurudisha mashambulizi hatimae mechi zingine magoli yamekua yakirudishwa na hata kufungwa.Kwa misimu mitatu mfululizo yanga wamekosa ubingwa kutokana na udhaifu wao wa kutokumiliki mpira.Timu imekua ikiongoza lakini inapoteza umiliki,kikosi dhaifu hata kufunga magoli mengi hawawezi kisha timu pinzani inachomoa mpira unaisha suluhu.Kwa maana hiyo kwa nini tusitumie pasi fupi fupi kuliko hizi pasi ndefu ambazo hazina macho.