Aina ya mpira wanao cheza yanga hauvutii hata kidogo

Sasa huo ushindi wenyewe kwani mnaupata? Au kumfunga Simba basi kwako ndio ushindi ni aibu kua na mashabiki Kama nyie.Juzi tu tumetoka kutolewa na rivers United kwa kupoteza ndani na nje hiyo si aibu Bali tumekubali kuaminishwa eti tumetolewa kwakua aucho,djuma na mayele hawakucheza utetezi wa kijinga sana huu.
Tulitolewa kwa kuwa River United walikuwa bora Zaidi uwanjani dhidi yetu. Simba hawakuwa bora Zaidi dhidi yetu.
 
unafahamu kuwa chelsea ni mabingwa wa ulaya? unafahamu pia mara ya mwsho kuchukua champions league walichukuaje? kila watu wana philosophy yao, Pepn alivyopeleka mpira wake bayern waliona anazingua tu ila baada ya kurudi kwe philosophy yao wametisha tena, usikariri kaka wala usijifariji pia mi km fan wa yanga nawashauri mfanyie kazi issue ya kiungo mshambuliaji pia washambuliaji waongeze juhudi maana ile balance iliokuwa inaletwa na konde boy haipo tena na kumlazimisha bwalya acheze km chama ni kazi bure mana chama c bwalya, kimsingi uwezo wenu wa kushambulia na kujilinda at the same ime umepungua sana mpeni mda coach atengeneze utaratibu mpya wa maisha mapema mfike tena robo fainali
 
Kwani team analysis inahitaji ucheze match ngapi,au wewe ndo yule kocha aliehitaji miezi 3 ili aweze kutengeneza chemistry ya team.
Utakuwa ni mpumbavu wa hali ya juu na usiyejua mpira kwa kuifanyia analysis timu kwa mechi tatu.tena kukiwa na rundo la wachezaji wapya Na kwanza nimeshakukosoa kuwa hizo analysis zako ni za uongo. Mechi ya Yanga vs river. Umiliki wa mpira umeongozwa na Yanga. Kwenye mechi ya simba vs Yanga umiliki wa mpira wamepishana kidogo tu kwa maana Yanga wamepiga pass 462 simba 467. Unasemaje hapo. Je unaweza kunipa ni mechi ipi ndani ya msimu Yanga walikuwa wamezidiwa kwa kiwango kikubwa. Njoo na takwimu. Sio una bwabwaja tu uharo hapa utafikiri mechi unaangalia peke yako
 
Kwanza kabisa nitangaze interest yangu mimi ni muumini wa mpira wa pasi zote ndefu na fupi na matokeo uwanjani yaonekane.Kwa miaka mingi sana yanga imekua na utamaduni wa kutumia pasi ndefu na mashambulizi ya kushitukiza(counter attack) lakini kwa bahati mbaya kwa miaka ya hivi karibuni kama sio yote wamekosa kikosi imara na sahihi cha kuendana na mfumo huo kitu kinachopelekea timu kuonekana inacheza hovyo hovyo na kupata matokeo ya kubahatisha(mpapatu papatu),aidha kwa miaka mingi yanga imekua inapata wachezaji ambao uwezo wao ni mdogo wengine hata kupokea mpira ni shida,kupiga pasi sahihi na eneo sahihi,kwa wakati sahihi ni shida achilia mbali uwezo wa kuliona lango,uwezo wa kukimbia na mpira(dribling).

Hivyo basi niwakati mwafaka uongozi wote kwa ujumla kuja na mbinu nyingine ya uchezaji ambayo itaendana na aina ya wachezaji waliokua nayo na kila kocha atakae kua amepewa kandarasi kukinoa kikosi lazima aufuate huo mfumo hata kama atakua na mbinu zake lakini zisicheze mbali na mfumo huo.Timu imekua haina uwezo wa kumiliki mpira kitendo kinachopelekea hata pale timu inapokua imetangulia basi hupoteza umiliki mpira na kuipa faida timu pinzani ya kurudisha mashambulizi hatimae mechi zingine magoli yamekua yakirudishwa na hata kufungwa.Kwa misimu mitatu mfululizo yanga wamekosa ubingwa kutokana na udhaifu wao wa kutokumiliki mpira.Timu imekua ikiongoza lakini inapoteza umiliki,kikosi dhaifu hata kufunga magoli mengi hawawezi kisha timu pinzani inachomoa mpira unaisha suluhu.Kwa maana hiyo kwa nini tusitumie pasi fupi fupi kuliko hizi pasi ndefu ambazo hazina macho.
Yanga ilikuwa na ukata , hakuna pesa utalaumu Tu , wewe kama umetoa pesa nyingi na wachezaji wanalipwa vzr na makocha ndiyo uje kusema

Ungewekeza au umesahau wanachama walikuwa wanaichangia mikoani

Hebu Acha zako
 
wewe ni miongoni mwa mashabiki mnaotuchelewesha kwenda kwenye mfumo mpya.Mkipata matokeo match moja basi mnasahau shida zote mnazopitia shame on you,na wewe kama utakua sio shabiki wa arsenal sijui
Hoja yako haina mashiko. Kwa mawazo ya aina hii, haishangazi kuona miaka nenda hakuna hata timu ya ligi daraja la tatu huko Katavi kwenu.
 
Wewe una hasira zako binafsi zimekufanya uamke na stress. Unasema Yanga kumiliki Mpira wanashindwa. Wakati mechi ya Yanga vs Rivers United Yanga anaongoza katika ball possession. Mechi ya Simba vs Yanga, Simba imeizidi Yanga kwenye umiliki wa mpira kwa tofauti ya asilimia 6 tu kwa kuzidiwa pass 5 tu Yanga wamepiga pass 462 wakati Simba wamepiga pass 467View attachment 1954627View attachment 1954628
 
Kocha wa Utopolo amesema baada ya miezi 3 ndio timu itakuwa imekamilika, kwani miezi 3 imetimia?

Sasa hivi wana kama mwezi 1 wanatisha, je ikifikisha miezi 3 si itakuwa hatari.

Nina wasiwasi uko baadae Boss Mo atatukimbia na mbaya zaidi sasa hivi Hans hayupo sijui tutaficha wapi sura zetu!
 
Pamoja na matokeo. Mchezo wa mpira wa miguu ni burudani. Kuna match moja nimeangalia, Mpaka nikaboreka.
 
Kwamba Yanga wabadili mfumo wao wa uchezaji ili wakufurahishe wewe? Huko kichwani kwako kuna akili kweli? Au umejaza sabuni za Mo?

Anyway, unateseka ukiwa wapi?
tunataka wacheze vizuri wapate ushindi wapiye hata round ya kwanza CAF champion league
 
Kwanza kabisa nitangaze interest yangu mimi ni muumini wa mpira wa pasi zote ndefu na fupi na matokeo uwanjani yaonekane.Kwa miaka mingi sana yanga imekua na utamaduni wa kutumia pasi ndefu na mashambulizi ya kushitukiza(counter attack) lakini kwa bahati mbaya kwa miaka ya hivi karibuni kama sio yote wamekosa kikosi imara na sahihi cha kuendana na mfumo huo kitu kinachopelekea timu kuonekana inacheza hovyo hovyo na kupata matokeo ya kubahatisha(mpapatu papatu),aidha kwa miaka mingi yanga imekua inapata wachezaji ambao uwezo wao ni mdogo wengine hata kupokea mpira ni shida,kupiga pasi sahihi na eneo sahihi,kwa wakati sahihi ni shida achilia mbali uwezo wa kuliona lango,uwezo wa kukimbia na mpira(dribling).

Hivyo basi niwakati mwafaka uongozi wote kwa ujumla kuja na mbinu nyingine ya uchezaji ambayo itaendana na aina ya wachezaji waliokua nayo na kila kocha atakae kua amepewa kandarasi kukinoa kikosi lazima aufuate huo mfumo hata kama atakua na mbinu zake lakini zisicheze mbali na mfumo huo.Timu imekua haina uwezo wa kumiliki mpira kitendo kinachopelekea hata pale timu inapokua imetangulia basi hupoteza umiliki mpira na kuipa faida timu pinzani ya kurudisha mashambulizi hatimae mechi zingine magoli yamekua yakirudishwa na hata kufungwa.Kwa misimu mitatu mfululizo yanga wamekosa ubingwa kutokana na udhaifu wao wa kutokumiliki mpira.Timu imekua ikiongoza lakini inapoteza umiliki,kikosi dhaifu hata kufunga magoli mengi hawawezi kisha timu pinzani inachomoa mpira unaisha suluhu.Kwa maana hiyo kwa nini tusitumie pasi fupi fupi kuliko hizi pasi ndefu ambazo hazina macho.
Yanga kelele nyingi sana
 
Kocha wa Utopolo amesema baada ya miezi 3 ndio timu itakuwa imekamilika, kwani miezi 3 imetimia?

Sasa hivi wana kama mwezi 1 wanatisha, je ikifikisha miezi 3 si itakuwa hatari.

Nina wasiwasi uko baadae Boss Mo atatukimbia na mbaya zaidi sasa hivi Hans hayupo sijui tutaficha wapi sura zetu!
wasiwasi wako ulikuwa sahihi bosi kashakimbia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom