Aina 8 za wapangaji katika nyumba za kupanga

Aina 8 za wapangaji katika nyumba za kupanga

Soma paragraph ya mwisho vizuri... Tunashirikishana events au matatizo vizuri tu. Kama mtu anasafiri tunajulishana ili wengine tutupie jicho kwake once in a while.
Kujifungia ndani haimaanishi kujitenga na wengine ila inasaidia tu usijue yasiyokuhusu na wasijue yanayokuhusu. Mnabaki kuheshimiana.
Siku hizi si umeshahamia kwa bibi lakini? Kwenye lile hekalu lenu.
 
Inapofikia muda unahitaji kuanza maisha ya kujitegemea, na unahitaji sehemu/chumba chenye unafuu kwenye suala zima la gharama/kodi, kimbembe hua kwenye utafutaji wa sehemu hio. Hasa pale ukizingatia sehemu unazozipata haziji na taarifa au huduma muhimu.

Hongera kama unasehemu ya kujitegemea kuishi, na hawa ndio aina ya wapangaji ambao tegemea kukutana nao kama unahamia kwenye nyumba ya kupanga.

1) Mashujaa wa kufanya ibada wasiotoa nafasi ya kulala..
Hawa watu, mmh. Shukuru kama hawatakua chumba cha jirani kwako, au lasivyo kulala itakua mtihani kwako. Wanaweza kusali, kuimba na kulia kuanzia asubuhi mpaka asubuhi nyingine bila kituo cha mapumziko, kizaazaa ukijifanya kulalamika tu, kichambo utakachopata sio cha nchi hii. [emoji22] [emoji25]

2) Walio na matatizo na kila mtu[emoji35] [emoji34]
Hawa muda wote hua na hasira hasira, kisirani, wame nuna-nuna bila sababu kuanzia asubuhi mpaka usiku. Hawapokeai wala kutoa salamu. Hua wanasubiri mtu ajikoroge tu aisome. Usiingie tisini zao, wapotezee uishi kwa amani.

3) Wanao kopa/kuazima kila kitu[emoji30] [emoji31]
Hutaki kukutana na hawa jamaa. Kukopa/Kuazima ni kama ibada kwao. Hukopa au kuazima kila kitu, kuanzia vyombo vya ndani, hela, mpaka viungo vya chakula. Halafu cha kukera sasa hua hawana cha kukuazima wewe.

4) Wanao ishi kama vivuli[emoji19] [emoji52]
Hujui kama yupo au hayupo, kwasabu muda wote mlango wao umefungwa. Utakutana nao pale baba/mama mwenye nyumba akiitisha kikao cha wapangaji tu.

5) Wanaopata wageni kila kukicha[emoji126] [emoji125]
Muda mwingine unaweza ukajiuliza kama unaishi kwenye nyumba ya kupanga au gesti. Hawa wapangaji hupata wageni kila kukicha, akitoka huyu kaingia mwingine. Ila hayakuhusu.

6) Wazee wa mziki mnene/pasua vichwa[emoji449] [emoji351] [emoji445]
Asubuhi mpaka jioni unalia mziki mkubwa kama mpo club, sauti full, utahisi speaker za redio zimewekwa chumbani kwako vile. Akiamka vibaya jamaa mnaweza kusikilizishwa mwimbo mmoja kuanzia asubuhi mpaka usiku mpaka mkazijua verse na chorus zote.

7) Wanandoa wanaogombana kila kukicha[emoji144] [emoji143]
(Acha nisitolee ufafanuzi hili, nisije kuwekwa kwenye kikaango humu[emoji124] [emoji124] [emoji124] ).

8) Wajuaji wa kila kitu, hata wasivojua[emoji15]
Hawa hupenda kuongea kuhusu kila kitu, topic ikianza tu lazima anacho cha kuongelea hata kama hawana ufahamu nayo. Jaribu kujiepusha nao hasa wakianza maswala ya siasa, mtakesha.

9) Shushushu/Kiherehere wa baba mwenye nyumba[emoji18]
Kama utashangaa jinsi gani baba mwenye nyumba hupata taarifa juu ya chochote kinachotokea ndani ya nyumba, hata kama hakuepo au haishi humo, tambua kuna huyo funza anaepeleka taarifa kwa maslahi ya kupata favor za mshua.

10) Baba/Mama mwenye nyumba[emoji123]
Sio lazima aishi hapo, wengine huishi sehemu nyingine. Kuna wengine wasela, utawaona mwisho wa mwezi mpaka mwisho wa mwezi. Ila kuna wengine haipiti week moja bila kutia timu mlangoni kwako kupiga mizinga ya hela, mpaka unajikuta unamdai hela ya kodi ya miaka miwili au mitatu. Wana maneno mazuri ya kupigia mizinga halafu utamsikia "ondoa shaka, we ondoa shaka kijana, tutakatana kwenye kodi tu,tuko pamoja".
Bahat nzuri mm sipo hapo
 
Mada inaondoa bacteria sugu[emoji869][emoji869]tatizo ni demu wangu analeta mazoea zoea na wapangaji wa kike ambao sijui hata wnafanya kazi gani kutwa mziki na wanalipa kodi na kula fresh tu....nifanyeje nimekataza sana
 
Mada inaondoa bacteria sugu[emoji869][emoji869]tatizo ni demu wangu analeta mazoea zoea na wapangaji wa kike ambao sijui hata wnafanya kazi gani kutwa mziki na wanalipa kodi na kula fresh tu....nifanyeje nimekataza sana
Kazi zao itakua za usiku, kama mchana wanakula mziki tu.[emoji4]
 
Hapa kwetu namba 4 inamhusu kila mpangaji. Unaeza kaa wiki mbili mpaka 3 hujamuona jirani yako. Kwenye bills ninakaa na ya umeme kuna jamaa anakaa na za maji. Wakizingua tu anaambiwa mwenye nyumba Anarara nao Mberee, haina kupigizana kelele na mtu
 
Hapa kwetu namba 4 inamhusu kila mpangaji. Unaeza kaa wiki mbili mpaka 3 hujamuona jirani yako. Kwenye bills ninakaa na ya umeme kuna jamaa anakaa na za maji. Wakizingua tu anaambiwa mwenye nyumba Anarara nao Mberee, haina kupigizana kelele na mtu
Huyo jamaa ni vizuri kukaa nae kwa ukaribu, atafaa mbeleni mfuko ukichacha mkuu.
 
Mm yangu namba 4 hadi kuna siku mama mwenye nyumba kaniuliza dada umekuja kupanga sehemu ya kuweka vitu vyako mara oooh siku zote haupo haufanyi usafi sijui nn na nn

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23] [emoji23] Sasa yeye mama mjengo inamuhusu nini kama umepanga kuweka vitu au kuishi, si anakula kodi yake.
 
Back
Top Bottom