witnessj
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 28,839
- 47,772
MM uache kushikilia tumbo jomoni...tunajua una mimbaHeheheeh kwa bibi sheria na protoko nyingi. Hatutajiachia vizuri.
Sent using Jamii Forums mobile app
MM uache kushikilia tumbo jomoni...tunajua una mimbaHeheheeh kwa bibi sheria na protoko nyingi. Hatutajiachia vizuri.
Hapa wanaweza kuhisi unafanya biashara haramu aise. Maana wabongo hawana dogo.#4 . Nimeishi nyumba mwaka mzima sijui jina la jirani hata mmoja.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nipo namba 4, 8.Wapangaji wachafu kuoga hata wiki inakatika hujamuona anaenda bafuni kuoga.
[emoji52][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mambo ya kufunguliana Muziki, kuna mpangaji tulikuwa tumepanga naye akiamua anapiga muziki kweli, kipindi hiko ndo Ali Kiba na Queen Darleen, Marlow Bembeleza, Latifa ya Mb Dogg ikawa full, ukimkataza ndo kama umechokoza.
Kuna siku alitembelewa na shangazi zake, jamaa wa chumba walichopakana akaweka porno, akafunga mlango akaondoka, halafu sauti ya juu.
Ilikuwa shida, mpaka wale shangazi wanaondoka bila kuaga, na wanamwambia ahame pale, ilikuwa aibu sana.
Hii ikukute ndio umeachana na mpenzi wako kama mwezi mmoja umepita, halafu chumba cha jirani ameleta mzigo unaopiga kelele. Haulali kwa mawazoKuna wasiojua kuzuia hisia inapofika wakati wa unyumba wanasikika mpaka barabarani
Hii namba 6 unaweza kuichukulia poa ila inakwaza jamani hhahahah eti kuamka vibaya yaani kuna jirani yangu kila siku ana nyimbo moja tena mpaka usiku na hana habari kabisaInapofikia muda unahitaji kuanza maisha ya kujitegemea, na unahitaji sehemu/chumba chenye unafuu kwenye suala zima la gharama/kodi, kimbembe hua kwenye utafutaji wa sehemu hio. Hasa pale ukizingatia sehemu unazozipata haziji na taarifa au huduma muhimu.
Hongera kama unasehemu ya kujitegemea kuishi, na hawa ndio aina ya wapangaji ambao tegemea kukutana nao kama unahamia kwenye nyumba ya kupanga.
1) Mashujaa wa kufanya ibada wasiotoa nafasi ya kulala..
Hawa watu, mmh. Shukuru kama hawatakua chumba cha jirani kwako, au lasivyo kulala itakua mtihani kwako. Wanaweza kusali, kuimba na kulia kuanzia asubuhi mpaka asubuhi nyingine bila kituo cha mapumziko, kizaazaa ukijifanya kulalamika tu, kichambo utakachopata sio cha nchi hii. [emoji22] [emoji25]
2) Walio na matatizo na kila mtu[emoji35] [emoji34]
Hawa muda wote hua na hasira hasira, kisirani, wame nuna-nuna bila sababu kuanzia asubuhi mpaka usiku. Hawapokeai wala kutoa salamu. Hua wanasubiri mtu ajikoroge tu aisome. Usiingie tisini zao, wapotezee uishi kwa amani.
3) Wanao kopa/kuazima kila kitu[emoji30] [emoji31]
Hutaki kukutana na hawa jamaa. Kukopa/Kuazima ni kama ibada kwao. Hukopa au kuazima kila kitu, kuanzia vyombo vya ndani, hela, mpaka viungo vya chakula. Halafu cha kukera sasa hua hawana cha kukuazima wewe.
4) Wanao ishi kama vivuli[emoji19] [emoji52]
Hujui kama yupo au hayupo, kwasabu muda wote mlango wao umefungwa. Utakutana nao pale baba/mama mwenye nyumba akiitisha kikao cha wapangaji tu.
5) Wanaopata wageni kila kukicha[emoji126] [emoji125]
Muda mwingine unaweza ukajiuliza kama unaishi kwenye nyumba ya kupanga au gesti. Hawa wapangaji hupata wageni kila kukicha, akitoka huyu kaingia mwingine. Ila hayakuhusu.
6) Wazee wa mziki mnene/pasua vichwa[emoji449] [emoji351] [emoji445]
Asubuhi mpaka jioni unalia mziki mkubwa kama mpo club, sauti full, utahisi speaker za redio zimewekwa chumbani kwako vile. Akiamka vibaya jamaa mnaweza kusikilizishwa mwimbo mmoja kuanzia asubuhi mpaka usiku mpaka mkazijua verse na chorus zote.
7) Wanandoa wanaogombana kila kukicha[emoji144] [emoji143]
(Acha nisitolee ufafanuzi hili, nisije kuwekwa kwenye kikaango humu[emoji124] [emoji124] [emoji124] ).
8) Wajuaji wa kila kitu, hata wasivojua[emoji15]
Hawa hupenda kuongea kuhusu kila kitu, topic ikianza tu lazima anacho cha kuongelea hata kama hawana ufahamu nayo. Jaribu kujiepusha nao hasa wakianza maswala ya siasa, mtakesha.
9) Shushushu/Kiherehere wa baba mwenye nyumba[emoji18]
Kama utashangaa jinsi gani baba mwenye nyumba hupata taarifa juu ya chochote kinachotokea ndani ya nyumba, hata kama hakuepo au haishi humo, tambua kuna huyo funza anaepeleka taarifa kwa maslahi ya kupata favor za mshua.
10) Baba/Mama mwenye nyumba[emoji123]
Sio lazima aishi hapo, wengine huishi sehemu nyingine. Kuna wengine wasela, utawaona mwisho wa mwezi mpaka mwisho wa mwezi. Ila kuna wengine haipiti week moja bila kutia timu mlangoni kwako kupiga mizinga ya hela, mpaka unajikuta unamdai hela ya kodi ya miaka miwili au mitatu. Wana maneno mazuri ya kupigia mizinga halafu utamsikia "ondoa shaka, we ondoa shaka kijana, tutakatana kwenye kodi tu,tuko pamoja".
Tulisikilizishwa "KANYAGA" ya diamond mpaka tukaijua sehemu alizokosea mashairi. Kuna watu wanakero hatariHii namba 6 unaweza kuichukulia poa ila inakwaza jamani hhahahah eti kuamka vibaya yaani kuna jirani yangu kila siku ana nyimbo moja tena mpaka usiku na hana habari kabisa
hahahahahahah pole mkuuTulisikilizishwa "KANYAGA" ya diamond mpaka tukaijua sehemu alizokosea mashairi. Kuna watu wanakero hatari