Aina 8 za wapangaji katika nyumba za kupanga

Aina 8 za wapangaji katika nyumba za kupanga

Mtoto Wa mwenye nyumba 4yrs,alikua mtundu balaaaa!!bhas Mzee baba nimejipinda nikajaza maji pipa akaja akatia sabuni!!daaah nilimvizia nikamkamata nikampa Yale makonzi ya kusugua kichwa na Bonge LA banzi mgongoni!!mamake kuja juu wapangaji wote wakamcharukia wakamwambia mwanao kazidi tumemchoka na wewe unamdekeza!!itabid awe mpole, na yule Mtoto alikua akijua nipo anakua km piritoni!!

umenikumbusha katoto fulani,kalikuwa kanajikuta katukutu,siku moja nilikaita usiku ili nikaelekeze kwa sababu nilikuta kameweka mpira wa maji kwenye mtaro ambao unapitisha maji ya bafuni,nilivokaita ile nimeanza kuongea tu kalinifonza kakaondoka (kana miaka 8 hivi) basi maza ake kwa kuwa alikuwepo sikutaka kukachapa kwa sababu hua anakahurumia,kesho yake asubuhi maza ake hayupo nilikashushia fimbo za hatari tokea siku hiyo kaliniheshimu sana hata watu wengine walikua wanakatisha kukaleta kwangu kakifanya ujinga
 
mimi no sita inanihusu nafungulia mziki mamake hadi akili ziwakae sawa yaani

kuna jamaa alikuwa jirani yangu alikuwa na tabia hii basi akiwasha makelele yake saa 12 asubuhi ananikatisha usingizi na mimi naweka nyimbo zangu za kikongo mara Madilu system mara gatho beevens hajakaa sawa naweka vitu vya awilo,jamaa alikua anazima ki subwoofer chake mwenyewe bila kuambiwa[emoji23]
 
Namba moja nilishawah kaa naye mwee yule mama siwez msahau
Inapofikia muda unahitaji kuanza maisha ya kujitegemea, na unahitaji sehemu/chumba chenye unafuu kwenye suala zima la gharama/kodi, kimbembe hua kwenye utafutaji wa sehemu hio. Hasa pale ukizingatia sehemu unazozipata haziji na taarifa au huduma muhimu.

Hongera kama unasehemu ya kujitegemea kuishi, na hawa ndio aina ya wapangaji ambao tegemea kukutana nao kama unahamia kwenye nyumba ya kupanga.

1) Mashujaa wa kufanya ibada wasiotoa nafasi ya kulala..
Hawa watu, mmh. Shukuru kama hawatakua chumba cha jirani kwako, au lasivyo kulala itakua mtihani kwako. Wanaweza kusali, kuimba na kulia kuanzia asubuhi mpaka asubuhi nyingine bila kituo cha mapumziko, kizaazaa ukijifanya kulalamika tu, kichambo utakachopata sio cha nchi hii. [emoji22] [emoji25]

2) Walio na matatizo na kila mtu[emoji35] [emoji34]
Hawa muda wote hua na hasira hasira, kisirani, wame nuna-nuna bila sababu kuanzia asubuhi mpaka usiku. Hawapokeai wala kutoa salamu. Hua wanasubiri mtu ajikoroge tu aisome. Usiingie tisini zao, wapotezee uishi kwa amani.

3) Wanao kopa/kuazima kila kitu[emoji30] [emoji31]
Hutaki kukutana na hawa jamaa. Kukopa/Kuazima ni kama ibada kwao. Hukopa au kuazima kila kitu, kuanzia vyombo vya ndani, hela, mpaka viungo vya chakula. Halafu cha kukera sasa hua hawana cha kukuazima wewe.

4) Wanao ishi kama vivuli[emoji19] [emoji52]
Hujui kama yupo au hayupo, kwasabu muda wote mlango wao umefungwa. Utakutana nao pale baba/mama mwenye nyumba akiitisha kikao cha wapangaji tu.

5) Wanaopata wageni kila kukicha[emoji126] [emoji125]
Muda mwingine unaweza ukajiuliza kama unaishi kwenye nyumba ya kupanga au gesti. Hawa wapangaji hupata wageni kila kukicha, akitoka huyu kaingia mwingine. Ila hayakuhusu.

6) Wazee wa mziki mnene/pasua vichwa[emoji449] [emoji351] [emoji445]
Asubuhi mpaka jioni unalia mziki mkubwa kama mpo club, sauti full, utahisi speaker za redio zimewekwa chumbani kwako vile. Akiamka vibaya jamaa mnaweza kusikilizishwa mwimbo mmoja kuanzia asubuhi mpaka usiku mpaka mkazijua verse na chorus zote.

7) Wanandoa wanaogombana kila kukicha[emoji144] [emoji143]
(Acha nisitolee ufafanuzi hili, nisije kuwekwa kwenye kikaango humu[emoji124] [emoji124] [emoji124] ).

8) Wajuaji wa kila kitu, hata wasivojua[emoji15]
Hawa hupenda kuongea kuhusu kila kitu, topic ikianza tu lazima anacho cha kuongelea hata kama hawana ufahamu nayo. Jaribu kujiepusha nao hasa wakianza maswala ya siasa, mtakesha.

9) Shushushu/Kiherehere wa baba mwenye nyumba[emoji18]
Kama utashangaa jinsi gani baba mwenye nyumba hupata taarifa juu ya chochote kinachotokea ndani ya nyumba, hata kama hakuepo au haishi humo, tambua kuna huyo funza anaepeleka taarifa kwa maslahi ya kupata favor za mshua.

10) Baba/Mama mwenye nyumba[emoji123]
Sio lazima aishi hapo, wengine huishi sehemu nyingine. Kuna wengine wasela, utawaona mwisho wa mwezi mpaka mwisho wa mwezi. Ila kuna wengine haipiti week moja bila kutia timu mlangoni kwako kupiga mizinga ya hela, mpaka unajikuta unamdai hela ya kodi ya miaka miwili au mitatu. Wana maneno mazuri ya kupigia mizinga halafu utamsikia "ondoa shaka, we ondoa shaka kijana, tutakatana kwenye kodi tu,tuko pamoja".
 
kuna jamaa alikuwa jirani yangu alikuwa na tabia hii basi akiwasha makelele yake saa 12 asubuhi ananikatisha usingizi na mimi naweka nyimbo zangu za kikongo mara Madilu system mara gatho beevens hajakaa sawa naweka vitu vya awilo,jamaa alikua anazima ki subwoofer chake mwenyewe bila kuambiwa[emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23] daah so poa
 
Na wapangaji wanaombana kila kitu chumvi, sahani,mwiko, ila hiyo 4 namba inanihusu mimi kabisa
 
Back
Top Bottom