Marine creature
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 2,255
- 2,978
kero kwa hawa mother house,ukiweka hata carpet la salon watakwambia linaaribu sakafu huk ukiangalia kwny mkataba hakuna terms kamam hizo
Sasa utakuta mtu mbishi wa kulipa luku halafu yeye ndo anaishi kwenye nyumba yenye main switch..Tunao ishi kama kivulii,gonga like hapa...
pia umewasahau Wale wabishi wa kuchangia bili ya umeme, maji..
Binafsi wasipo changia, huwa nawakatia umeme kwenye main switch,, ule unao enda vyumbani mwao
😂😂😂Nahisi hii ishamkuta baba mwenye nyumba wangu, maana hafurukuti hata kidogo tangu huyu mpangaji mwenzetu kigagula ahamie hapa!Umesahau washirikina na wachawi mkuu, Upate mpangaji kama mshana, anaweza akuroge usahau ka nyumb n yako mwishowe we ndo unamlipa mpangaji
mbona ume addres ishu ya wapangaji kama vile watu walivyo na mawazo potofu kuhusu mahousegirlInapofikia muda unahitaji kuanza maisha ya kujitegemea, na unahitaji sehemu/chumba chenye unafuu kwenye suala zima la gharama/kodi, kimbembe hua kwenye utafutaji wa sehemu hio. Hasa pale ukizingatia sehemu unazozipata haziji na taarifa au huduma muhimu.
Hongera kama unasehemu ya kujitegemea kuishi, na hawa ndio aina ya wapangaji ambao tegemea kukutana nao kama unahamia kwenye nyumba ya kupanga.
1) Mashujaa wa kufanya ibada wasiotoa nafasi ya kulala..
Hawa watu, mmh. Shukuru kama hawatakua chumba cha jirani kwako, au lasivyo kulala itakua mtihani kwako. Wanaweza kusali, kuimba na kulia kuanzia asubuhi mpaka asubuhi nyingine bila kituo cha mapumziko, kizaazaa ukijifanya kulalamika tu, kichambo utakachopata sio cha nchi hii. [emoji22] [emoji25]
2) Walio na matatizo na kila mtu[emoji35] [emoji34]
Hawa muda wote hua na hasira hasira, kisirani, wame nuna-nuna bila sababu kuanzia asubuhi mpaka usiku. Hawapokeai wala kutoa salamu. Hua wanasubiri mtu ajikoroge tu aisome. Usiingie tisini zao, wapotezee uishi kwa amani.
3) Wanao kopa/kuazima kila kitu[emoji30] [emoji31]
Hutaki kukutana na hawa jamaa. Kukopa/Kuazima ni kama ibada kwao. Hukopa au kuazima kila kitu, kuanzia vyombo vya ndani, hela, mpaka viungo vya chakula. Halafu cha kukera sasa hua hawana cha kukuazima wewe.
4) Wanao ishi kama vivuli[emoji19] [emoji52]
Hujui kama yupo au hayupo, kwasabu muda wote mlango wao umefungwa. Utakutana nao pale baba/mama mwenye nyumba akiitisha kikao cha wapangaji tu.
5) Wanaopata wageni kila kukicha[emoji126] [emoji125]
Muda mwingine unaweza ukajiuliza kama unaishi kwenye nyumba ya kupanga au gesti. Hawa wapangaji hupata wageni kila kukicha, akitoka huyu kaingia mwingine. Ila hayakuhusu.
6) Wazee wa mziki mnene/pasua vichwa[emoji449] [emoji351] [emoji445]
Asubuhi mpaka jioni unalia mziki mkubwa kama mpo club, sauti full, utahisi speaker za redio zimewekwa chumbani kwako vile. Akiamka vibaya jamaa mnaweza kusikilizishwa mwimbo mmoja kuanzia asubuhi mpaka usiku mpaka mkazijua verse na chorus zote.
7) Wanandoa wanaogombana kila kukicha[emoji144] [emoji143]
(Acha nisitolee ufafanuzi hili, nisije kuwekwa kwenye kikaango humu[emoji124] [emoji124] [emoji124] ).
8) Wajuaji wa kila kitu, hata wasivojua[emoji15]
Hawa hupenda kuongea kuhusu kila kitu, topic ikianza tu lazima anacho cha kuongelea hata kama hawana ufahamu nayo. Jaribu kujiepusha nao hasa wakianza maswala ya siasa, mtakesha.
9) Shushushu/Kiherehere wa baba mwenye nyumba[emoji18]
Kama utashangaa jinsi gani baba mwenye nyumba hupata taarifa juu ya chochote kinachotokea ndani ya nyumba, hata kama hakuepo au haishi humo, tambua kuna huyo funza anaepeleka taarifa kwa maslahi ya kupata favor za mshua.
10) Baba/Mama mwenye nyumba[emoji123]
Sio lazima aishi hapo, wengine huishi sehemu nyingine. Kuna wengine wasela, utawaona mwisho wa mwezi mpaka mwisho wa mwezi. Ila kuna wengine haipiti week moja bila kutia timu mlangoni kwako kupiga mizinga ya hela, mpaka unajikuta unamdai hela ya kodi ya miaka miwili au mitatu. Wana maneno mazuri ya kupigia mizinga halafu utamsikia "ondoa shaka, we ondoa shaka kijana, tutakatana kwenye kodi tu,tuko pamoja".
Utakua mtoto wa baba mwenye nyumba wewe.mbona ume addres ishu ya wapangaji kama vile watu walivyo na mawazo potofu kuhusu mahousegirl
Au kwaya za kanisani. Unajikuta upo na manzi getto nje kwaya inagonga kinoma[emoji1787][emoji1787][emoji1787] wazee wa muziki mneneee... Usiombe akawa anapenda singeli...
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe. utakuwa namba 9.Wapangaji wachafu kuoga hata wiki inakatika hujamuona anaenda bafuni kuoga.
Hatari dadeq[emoji3]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] wazee wa muziki mneneee... Usiombe akawa anapenda singeli...
Sent using Jamii Forums mobile app
Umesahau wapangaji walevi...Inapofikia muda unahitaji kuanza maisha ya kujitegemea, na unahitaji sehemu/chumba chenye unafuu kwenye suala zima la gharama/kodi, kimbembe hua kwenye utafutaji wa sehemu hio. Hasa pale ukizingatia sehemu unazozipata haziji na taarifa au huduma muhimu.