Aina 8 za wapangaji katika nyumba za kupanga

Aina 8 za wapangaji katika nyumba za kupanga

Nyuzi ijayo itakua inahusu WALE WATU tunaokutana nao katika sherehe za harusi: Kuna wale wazee wa kula, Wazee wa make-up na nyusi kama paka mwizi, Mashangazi/Wajomba wenye viherehere kutuuliza lini tunaoa/kuolewa wakati bado tuna tafrani kupambana na hawa wapangaji tulionao kwenye hii nyuzi ya leo
 
Aisee haya mambo yakupanga yamenipata si mchezo

Nilipanga upande ila kuna mpangaji mwenzetu ana familia hatar yaan utasema ana shule ya kindergaten ndan mda wote ni fujo tu kuanzia asubuh had saa nane usiku utasema ni kituo cha kulelea watoto wa mtaani

Kwa kweli ilinishinda maana ilinibidi kila siku nimuache mke wangu chumban mm nilale sebuleni
 
Mtoto Wa mwenye nyumba 4yrs,alikua mtundu balaaaa!!bhas Mzee baba nimejipinda nikajaza maji pipa akaja akatia sabuni!!daaah nilimvizia nikamkamata nikampa Yale makonzi ya kusugua kichwa na Bonge LA banzi mgongoni!!mamake kuja juu wapangaji wote wakamcharukia wakamwambia mwanao kazidi tumemchoka na wewe unamdekeza!!itabid awe mpole, na yule Mtoto alikua akijua nipo anakua km piritoni!!
Yaani Mimi ningemzamisha kwa pipa atoe Sabuni aloo. Sipendagi ujingaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom