Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,075
Ndivyo unavyojifajiri?Zitto akitimuliwa kesho yake chadema inakufa bila zito hakuna chadema.
Wakubwa zako,akina Wassira na Nape,nao ndiyo zilikuwa njozi zao,mara Chadema haiwezi kumaliza mwaka huu kabla hatujaizika.
Kumbe walikuwa wakijiamini hivyo,wakijua kwamba ndani ya CDM,wana watu wao,watakaowafanyia kazi ya "kuinyonga" Chadema.
Kwa bahati nzuri kwa CDM,na bahati mbaya sana kwa magamba,walisahau ule msemo unaosema Mungu si Athumani,ile mipango yao hao akina MM, M2,na M3 sasa imebumbuluka!
Na kinachoshangaza sana ni kuwa wanaomlilia Zitto,wengi wao ni wanaCCM kuliko wanaCDM!!
Ushahidi ni comments zilizotolewa mtandaoni na Ridhiwani na Mwigulu Nchemba!!
Huo ni uthibitisho mwingine kuwa,kiwiliwili cha ZZK kilikuwa CDM lakini moyo wake wote ulikuwa kwa magamba!!