mamayeyo
Senior Member
- Apr 4, 2012
- 167
- 138
Jana mchana wa saa 8 hivi niliona kituko na nikahisi aibu sana. Nilikuwa ndani ya posta ya Meru(Arusha) kwenye foleni ya dirisha la Western Union. Watu walikuwa wengi wakisubiri kuhudumiwa na wengi tulisimama kwani viti ni vichache. Nilipochoka kusimama nikatupa macho sehemu kwenye viti kama kuna upenyo nikae. Lahaula! Nilimwona kijana wa kiume wa Kiarika mwenye umri kati ya miaka 20-25 akiwa ameketi na mama mzee wa kizungu asiyepungua miaka 60. Uzee wa huyu bibi ulionekana wazi kwani hata ngozi yake ilikuwa imekunjamana na kupwaya. Mama huyo alikuwa amekumbatiwa na huyo kijana kwa mkono mmoja na mkono wa pili wa kijana ulikuwa busy akimkuna kuna bibi kizee yule na kumpapasa papasa kimapenzi. Bibi alikuwa ametulia tuli akionesha kuwa anafurahia zoezi la kijana. Kila mtu pale karibu yao alikuwa akiwatazama lakini kijana hakujali, alikuwa serious na kazi yake. Nilihisi aibu sana kwa sababu yule kijana alikuwa mtoto sana kwa yule bibi na pia niliogopa kuendelea kuwatazama kwa sababu nilihisi yule kijana ni mwanangu nikajikuta nataka nikamchape kibao aache ujinga ule. Mama wa kizungu akaitwa akachukue pesa dirishani. Wakapelekana akiwa bado kakumbatiwa. Mama alipokea pesa akampa mtoto akaziweka kibindoni, haooo wakaondoka wakisindikizwa na macho kama 50 hivi. Jamani! ndo nini hii? Mungu tuhurumie.