MmmmmmhWao tu ndo waliongea na Shetani direct na kuonana naee...!! Achana kabisa na mwanamke hujui shetani alimwambia nini.. na siku ile ulipolala usingizi mzito ili apatikane hujui baada ya kuumbwa Mungu nae alimwambia nini...
MWANAMKE NI FUMBO KUBWA SANA...
Mmmmmmh
Hahahah umenichekesha sana ila sijui utaua na kujeruhi wangapi? kwani wengi ndo wapo hivyo.Siku za usoni natazamia kumiliki silaha ya moto a.k.a paja la kuku ili kutatua suprise mbaya kama hizo.
Mkuu uchumba maana yake binti umemtolea barua na mahali pia hawa watu ni wapenzi sidhani kama wamefikia kwenye uchumaPole mkuu sijaona kama umekosea sababu pete za uchumba wengine wanafanya surprise
Habari za mida hii wana jf?
Mimi sio mpenzi sana wa uandishi mana mwandiko wangu mbaya.
Wacha niadithie ilivokuwa mwanzo mwisho..
Ni likizo time.Yeye(binti)akiwa anafanya kazi serikalini na mimi nafanya biashara zangu binafsi wakati mwingine napokea tenda za mda mrefu.Sikua na dili la msingi saana kuniingizia pesa ya maana.So tukawa kwenye mipango ya kwenda kuhesabiwa mimi na yeye.
Kwa kumbukumbu zangu ni tarehe 10 mwezi wa 12 tukiwa tumeshapangilia kila kitu kihusu safari ya uchagani..Tukakubaliana kuondoka tarehe 14 ya mwezi wa 12.
Usiku wa kuamkia tarehe 13 nikapata wazo.Kwanini kama tuko kwenye mahusiano ya mda mrefu na kila mmoja anampenda mwenzie tusipeleke mambo levo ingine???"Wazaz"pande zote mbili wanatufahamu.
"Tabia"tunafahamiana vyema japo mikwaruzano ya hapo na pale haikosekani.
Nikalitafakari wazo langu la usiku huo kwa undani na kwa kina nikajisemea mwenyewe"yafaa nimvishe pete ya uchumba"je ni wapi?Lini?Nani na nani awepo?mwisho ikawa mimi na yeye tunatosha mengine tutawajulisha yatakapokamilika..
(Nimechoka kuandika nafupisha)
Asubuh tarehe 14 tunaanza safari ila anashangaa! Ajui tunaelekea wapi.Safari ilikua "Zanzibar"nilipangilia kila kitu.
Kesho yake jion "romantic dinner"hajui chochote.
Namfanyia suprise katika ya dinner nimvishe pete nikiwa nimepiga magoti mbele yake.Siku ile kulikua na bendi inatumbuiza(coconut band)..
Anyway ni hivi aliigomea pete mbele ya wageni zaidi ya 90...mbele ya kila mtu mwenye shauku ya kuona anakubali.Aliniangalia kwa dakika tena halafu akamwagika machozi akasema "siwezi"
Usitake kujua nilikutwa na hali gani?
Nilijisikiaje mbele ya kadamnasi?pia sijui walinichukuliaje ila nilihisi kudhalilika..
Kila mtu alifika dar anavojua yeye.
Toka mwaka juzi lilivotokea hilo tukio hatukuwai kulizungumzia hadi leo na hatukuwai kuwa wapenzi tena.Ninachojua saizi yuko na mtoto mmoja.
Je kama ni wewe ungefanyaje?
Hapo nimeikumbuka nyimbo ya Sugu. Hayakuwa MapenziHapana zech . Let me give you hostoria fupi about mylife. Niliwahi kumpenda mwanamke.. nikampa almost everything vilivyomo ndani ya uwezo wangu. mpaka nilikuwa nampikia sometimes.
by then nilikuwa namaliza chuo. Nimeshajitambulisha kwao.. na anajulikana kwetu pia. Imebaki mahari.. lakin one day out of blue akasepa.
Nilimuuliza tatizo ni nn hana jibu. It has been five years.. nimekutana nae tena this year.. bado amekosa hatajib la kusema. Anajutia tu.
Tell me alikosa nn?
Never everUsijeingia Kwenye Lile Kundi Kubwa Linalowapigia Magoti Wanawake Wakati Wa Kuwavisha Pete
Hapo nimeikumbuka nyimbo ya Sugu. Hayakuwa Mapenzi
HahaaSiku za usoni natazamia kumiliki silaha ya moto a.k.a paja la kuku ili kutatua suprise mbaya kama hizo.
Hivi huwa inatokea ....hahaa daah aibu SanaNaonaga youtube haya mambo ...aisee hili swala unahitaji pumbu za chuma kuvumilia hiyo aibu
Hahaa jf raha sanaGoti umepiga hola Pvmbv wamepiga wengine na mtoto juu!!!
Vijana wa siku hizi mnatudhalilisha sana kaka zenu,ulichotakiwa kufanya ni kumtia mimba kisha umuache aamue mwenyewe kwamba aishi na wewe au asiishi na wewe.
Umeona wajanja walivyo?wame-skip ishu ya kuvishana pete wakamvisha pete ya ukweli sasa anahangaika nayo wewe umeenda kupiga magoti,kwani uliambiwa Mungu yule?