Niliwaambia humu,huyu demu ana ki-booklet cha cheti cha form four.Huyu alikuwa anarudia rudia mtihani wa Form four ili apate credit kwa zaidi ya miaka sita.
Kila mwaka aliokuwa anarudia una cheti chake,ukimwambia leta cheti chako cha kidato cha nne ataleta kibunda cha vyeti kama cha noti feki za elfu tano tano.Kuna mwaka amerudia somo moja tu.Alipoona kituo cha Mtihani Musoma wamemzoea kama "Resitter" sugu akahamia Mwanza kuwa anafanyia mitihani kukwepa aibu,akawa kituo cha Butimba TTC.Huko nako mpaka wakamkariri.
Hiyo QT yenyewe kufaulu ili aweze kukaa kwa ajili ya mtihani wa form four aliisoma miaka karibu minne!!
Hawa ndio watu tunawapa dhamana ya kutunga sheria,kurekebisha,kutazama miswaada na kuihoji serikali,mtu hana hata msingi wa Elimu ya Uraia.Huyu ina maana hata ile Topic ya Form Two ya "Organs of the State" hajawahi kuiona maisha yake yote,ndio maana anaona Serikali na Bunge ni kitu kimoja.
Angesoma "Organs of the State" angejua kuna "Government","Parliament" na "Judiciary" na hata lile swali maarufu la "Civics" kidato cha pili la "With vivid examples,define what is Separation of Power",angejuwa umuhimu wa vikao vya Bunge kuwa mwiba kwa serikali na umuhimu wa wananchi kuona uwajibikaji wa wabunge wao bungeni,hivyo "Bunge Live" kwake isingekuwa hoja ya watu kutaka kuuza sura bali umuhimu wa organ moja ya State kuisimamia nyingine kwa dana ya "Separation of Power".Elimu thabiti ya kidato cha kwanza hadi cha nne ingeweza kumpa upeo tu wa kuchambua mambo.Kuna watu humo bungeni hawajasoma sana lakini wanatoa vitu vyenye ujazo,Wapo walioishia kidato cha nne lakini wanajenga hoja na kusema kwa staha.
Hii swala litazamwe upya,haiwezekani katika nchi moja,dereva wa mbunge ili apewe funguo ya kumuendesha mbunge anatakiwa awe na elimu ya kidato cha nne,leseni,Cheti cha VETA na course "Advanced Driving Grade Two-VIP" halafu sifa za kazi za anayeendeshwa ni "kujuwa kusoma na kuandika" bila kujali huko kuandika na kusoma kajuwa chini ya mti au katika mfumo wa elimu rasmi.
Ndio maana tunaokoteza watu kama kina "Agness Marwa" na kuwatupia bungeni,wanatuletea Lugha za sokoni na uelewa wa vitini vya Nyambari Nyangwine