Agnes Marwa ang'aka, adai wanaomzushia wanampa 'Kick'

Agnes Marwa ang'aka, adai wanaomzushia wanampa 'Kick'

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Mbunge Agnes Marwa leo akihojiwa na Clouds Fm amesema wanaomzushia matokeo feki wanampa Kick. Aidha Mbunge huyo amesema yeye hakusoma shule za shati jeupe na sketi ya blue, kwa sababu alipomaliza darasa la saba na baba yake kuwa amefariki ilibidi aanze kushirikiana biashara ndogondogo na mama yake.

Pia mbunge huyo akaongeza kuwa amejisomesha QT(Qualifying Test), Pia ameuza dagaa ili apate ada ya kulipia masomo yake. Mh Marwa akasema matokeo yanayosambazwa sio ya kwake ijapokuwa CV ya bungeni ni ya kwake. Hii ni nukuu ya maneno yake akihojiwa na kipindi cha POWER BREAKFAST cha Clouds Fm.

downloadfile-23-jpeg.348356



“Nimesoma muda mrefu kwasababu nilikuwa nasoma kidogo kidogo, msiwakatishe tamaa watu wanaotaka kusoma QT lakini CV ya Bungeni ni kweli ni ya kwangu”.

13173753_910335449088810_9110294170724599123_n-jpg.348380


Ikumbukwe: Chanzo cha yote haya kuibuka ni baada ya mbunge huyo kusema anasikia uchungu hadi kulia akipinga Bunge kuonekana Live.



BAADA YA MEMBER WA JF KUILETA HABARI HII MAPEMA JANA LEO GAZETI LA MWANANCHI LIMERIPOTI HABARI HII PIA SOMA ZAIDI HAPA CHINI:
========================
asigwa
Mbunge wa viti maalumu (CCM), Agness Marwa amesema waliosambaza habari mbaya kuhusu elimu yake, wamemsaidia kupata umaarufu. Habari kuhusu utata wa elimu yake zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii hususan JF kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya habari ya Mwananchi Digital kumuonyesha akiponda wabunge wa upinzani kushikilia hoja ya kutaka shughuli za Bunge ziendelee kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni.

Katika mkanda huo wa Mwananchi Digital, mbunge huyo alisema anasikia uchungu kwa wapinzani kung'ang'ania hoja hiyo na akadiriki kusema anataka kulia kutokana na hoja hizo akisema wanawadanganya wananchi.

Mkanda huo ulifuatiwa na habari kusambazwa zinazoeleza mambo kumi tata kuhusu elimu na ajira yake, huku ikitoa matokeo yake ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Nne ambayo hayakuwa mazuri.

"Inawezekana mwenyezi Mungu kawatumia ili nifahamike," alisema Marwa jana asubuhi kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kila siku asubuhi na kituo cha Redio Clouds.

Aliwashukuru walioandika habari hizo iwe kwa ubaya au uzuri, akidai kuwa wamempa umaarufu kwa kuwa ingekuwa vigumu kwa mbunge kutoka Mara kufahamika.
Kuhusu suala la vyeti vilivyoibua utata wa shule alizosoma kama zilivyoainishwa kwenye CV hiyo, alisema si ya kweli na hakusoma shule zilizotajwa.

Alisema hakuwahi kufanikiwa kusoma shule hizo kwa sababu kwa wakati huo mkoani Mara ilikuwa ni vigumu kwa mtoto wa kike kusomeshwa au kuaminika kwamba anaweza kusoma na baadaye kusaidia familia ambayo haikuwa na uwezo baada ya baba yake kufariki dunia.

"Uwezo wa mama ulikuwa mdogo kiasi cha kwamba alikuwa hawezi kumudu hata mlo wa siku moja kwa familia," alisema Marwa.

Alisema baada ya kuhitimu shule ya msingi alibakia nyumbani akifanya shughuli za kujiingizia kipato, huku akimsaidia mama yake. Marwa alisema hapo aliweza kujiendeleza kwa masomo ya sekondari kwa kufanya mtihani wa maarifa (QT).

"Kwa hiyo wanapotosha kusema nimesoma kwa miaka sita. Nimesoma zaidi ya miaka 10," alisema Marwa na kwamba alikuwa akiuza dagaa akipitisha mitaani huku akichoma mahindi barabarani.

Alipoulizwa kuhusu uhalali wa vyeti, alijibu "Hivyo vyeti siyo vyangu, isipokuwa CV ya bungeni ni ya kweli, wala si ya uongo."

Alisema mtu akisoma QT hazuiliwi kusitisha masomo kwa muda kama hana uwezo wa kumudu ada.

Chanzo: Mwananchi
 
Kama kweli elimu yake ni kama ilivyo pitishwa mitandaoni basi binafsi nampongeza sana. Lazima ni mwanamke jasiri anayejiamini na kutetea hoja yake iliyoshindwa kukosolewa na wasomi wanaojiita wamebobea kwa kutumia busara na hekima zao.

Kutafuta namna ya kumdhoofisha mtu ambaye kwa maelezo si tishio ni kudhihirisha kwamba kweli ni tishio. Ni wangapi wana degree zao na busara kwao ni Sifuri?, wakianza kupayupa unatamani kuziba maskio. Ukweli lazima utatuweka huru na njia ya mwongo daima ni fupi.
 
kwani amesema kwa nini alikuwa anatetea Bunge lisirushwe live? huyu mdada ni matatizo, mara anasema matokeo siyo yake, mara aseme amesoma QT, mara amesoma muda mrefu, atuambie hiyo QT alisomea wapi na kituo alichofanyia mtihani pia atupe na matokeo yake halisi, alafu kusoma kwa kuuza dagaa hakumuondelei mtu busara, tena wengi waliosoma kwa mtindo huo ndo leo wanaongoza kwa kuwa na busara na hekima,
 
Huyu inawezekana hata alipokuwa nje mbunge alikuwa haangalii bunge vinginevyo angejua watu wanavyochangia hoja
 
Back
Top Bottom