Uongo wa kisiasa hauwezi kuficha ukweli kwamba China na Afrika zinatafuta maendeleo pamoja

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111428165323.jpg


Hivi karibuni, mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa onyo tena kuhusu hatari ya baadhi ya nchi zinazoendelea kushindwa kulipa madeni, nyingi zikiwa ni za Afrika. Hivyo baadhi ya vyombo vya habari vya Marekani vinachukua fursa hiyo kurudia tena kile kinachoitwa “mtego wa madeni”. Mathalan, Shirika la Habari la Marekani AP lilidai kuwa Kenya na Zambia zote ni "wahanga" wa "mtego wa madeni". Lakini, je, huu ni ukweli?

Kwa mujibu wa Wizara ya Fedha ya Kenya, hadi kufikia Machi mwaka huu, jumla ya deni la nje la nchi hiyo lilikuwa dola za Kimarekani bilioni 36.66, lakini nyingi zimetoka kwenye taasisi za fedha za kimataifa na wakopeshaji wa kibiashara wa nchi za magharibi, na China ilichangia asilimia 17.2 ya deni lote la nchi hiyo. Hali nchini Zambia inafanana na ile ya Kenya. Kulingana na ripoti ya Taasisi ya Sera ya Afrika iliyotolewa mwaka jana, karibu robo tatu ya malipo ya madeni ya nchi za Afrika Kusini mwa Sahara yamekwenda kwa wakopeshaji wa biashara wa nchi za magharibi, ambao wao ndio wadai wakubwa zaidi wa madeni barani Afrika. Ili kuficha ukweli huo, Marekani na nchi nyingine za magharibi ziliunda kile kinachoitwa "mtego wa madeni" ili kugeuza ufuatiliaji wa watu.

Wakati huohuo, riba kutoka kwa wakopeshaji wa nchi za Magharibi imezipa nchi nyingi za Afrika shinikizo kubwa. Shirika la "Debt Justice" la Uingereza lilitoa ripoti mwaka jana ikisema, kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia, wastani wa riba ya mikopo ya China kwa nchi za Afrika ni 2.7%, huku ile ya mikopo ya nchi za Magharibi ni 5%, karibu mara mbili zaidi ya China. Na sera ya fedha ya kutowajibika ya Marekani imeongeza zaidi riba ya madeni, na hii ndiyo sababu kuu ya mlipuko wa hivi karibuni wa hatari za kushindwa kulipa madeni katika nchi za Afrika. Marekani kwanza ilitekeleza sera ya fedha iliyolegea sana na kuruhusu dola zenye riba ya chini kuingia katika nchi za Afrika. Lakini tangu Januari 2022, Marekani imepandisha viwango vya riba ovyoovyo, jambo ambalo limesababisha kushuka kwa thamani ya sarafu za nchi za Afrika, na shinikizo la ulipaji wa madeni kwa dola limeongezeka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Guterres hivi karibuni alisema riba za madeni yanayolipwa na nchi za Afrika kwa sasa ni mara nne zaidi ya zile za Marekani.

Hali halisi ni kuwa suala la madeni ya nchi za Afrika ni suala la maendeleo. Ili kutatua tatizo la madeni, si tu ni kupitia kushughulikia madeni, lakini pia ni lazima kuboresha uwezo wa nchi za Afrika wa kupata maendeleo endelevu, hasa wakati athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa dhidi ya maendeleo ya Afrika zimefikia kiwango kikubwa sana. Kwa mujibu wa takwimu mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kupunguza GDP ya bara hilo kwa asilimia 3 ifikapo mwaka 2050. Katika hali hii, maendeleo ya kijani yanakuwa sekta muhimu ya ushirikiano kati ya Afrika na sehemu nyingine, na China tayari iko katika nafasi ya kuongoza katika ushirikiano huo.

China ni mwekezaji mkubwa katika sekta ya uzalishaji wa umeme barani Afrika, na vituo vingi vya umeme ilivyowekeza barani Afrika ni vya nishati safi, hasa umeme wa maji (60%). Hii ni tofauti kabisa na uwekezaji wa nishati wa Marekani ambao unajikita zaidi kwenye mafuta. Tangu mwaka 2015, serikali ya Marekani imewekeza zaidi ya dola bilioni 9 katika miradi ya mafuta na gesi barani Afrika, ikilinganishwa na dola milioni 682 tu za miradi safi ya nishati kama vile upepo na jua. Kwa hivyo wakati Marekani imetoa "ilani za kijani" za kuunga mkono mabadiliko ya nishati barani Afrika, ni dhahiri pesa hizo zinakwenda wapi.

Basi kati ya China na Marekani, nani ni mshirika wa dhati kwa maendeleo ya Afrika na nani anatekeleza vipaumbele vyake binafsi kwa kuhatarisha maslahi ya nchi za Afrika, jibu ni wazi. Sasa mitego mbalimbali ya kauli iliyotolewa na wanasiasa wa Marekani haina soko tena. Kama alivyosema balozi wa zamani wa Zimbabwe nchini China Christopher Mutsvangwa, "Ushirikiano kati ya China na Afrika unaifanya Afrika kuwa ya kisasa na kuifikisha Afrika katika uwanja wa uchumi wa dunia, jambo ambalo halijawahi kufanywa na nchi za Magharibi."
 
Back
Top Bottom