Afrika Kusini niijuavyo mimi

Afrika Kusini niijuavyo mimi

Kama mgeni anakuja nchini mwako na anatoboa wazawa lazima mtakuwa na matatizo,Tatizo la wasauzi ni ulevi,uvivu, kutokusafiri,na kuamini Waafrika wengine ni masikini.
Hali hii unasema ya wageni kufanikiwa kuliko wenyeji ipo Sana Africa chunguza hata hapa Tanzania unaona ukitoa mikoa michake Kama Kilimanjaro mingine mingi wenyeji huwa hawaendelei kuwashinda wageni
Unajua sababu kubwa ni Nini ?

Sababu kubwa ni ufinyu wa exposure kwa wenyeji, wenyeji Kuna kuwa fursa wanazo/zipo hapo kwao ila hawazioni na Kama wakiziona hawawezi ku-take action Sasa kwa mazingira Kama haya unawezaje kumshinda mgeni maendeleo ?

kwa kua yeye kafika na kiasi anakua na exposure kwa alikotoka na huku anakofika anaona fursa anatumia fursa ni lazima tu ata-win life
Wenyeji kazi zao zinakua kulalamika tu
 
Ina maana huwa wanaongea kiswahili ?

Nje ya mada nina ndugu yangu mmoja huwa namuona amepiga picha kashika pesa nene na bastola mkononi. Huwa nashindwa kumuelewa zile bastola anazitumia kufanya nini
Hawa watu Tuombe MUNGU hayo MAMBO yao wafanyie huko huko! Wakiyaleta huku sijui itakuwaje?!
 
Nimeishi South kwa takriban miaka mitano hivi kuanzia 1996 ni mara baada ya Mandela kuachia hatamu na kumkabidhi Thabo Mbeki kijiti.... Kinachotokea sasa huko kina mizizi na ubaguzi wa rangi lakini vilevile kina mizizi na uhuru bila maandalizi mtambuka
Nisirudi nyuma sana kihistoria... Lakini wazungu wahamiaji baada ya kutua kwenye nchi nzuri ya kuvutia ya Africa Kusini, wakaitamani na kupanga mipango ya kuitawala milele.... Hili walifanikiwa kwa kiasi kikubwa mno na wasouth walipokuja kushtuka tayari wakawa kwenye 18 za wazungu
. Wakabaguliwa kwa kila hali
. Wakaundiwa matabaka
. Wakanyimwa elimu
. Wakapenyezewa vibaraka ili wapelelezane wao kwa wao
. Wakanyimwa nafasi za kazi nzuri na maisha yanayomstahili binadamu
. Wale waliogutuka na kutaka kuwakomboa wenzao wakateswa
wakafungwa,
wakazushiwa kesi kubwa kubwa,
wengine wakauliwa na
wengine wakawekwa kizuizini

Binadamu hafugiki kama mnyama... Mapambano ya kudai nchi yao na uhuru wao vikazidi kupamba moto.. Ni katika kipindi hiki wasouth kwa makabila yao yote wakawa kitu kimoja... Ikawa ni mwiko kubaguana
Yakajengwa makambi mengi ya kudai uhuru.. Sauti ikawa moja tu UKOMBOZI NA UHURU basi... Maadili mengine yote yakawekwa kando...
Uadilifu
Utu wema
Upendo
Tafakuri
Maono nknk
Haya yote yakawekwa kwenye kabrasha moja tu UKOMBOZI na UHURU.. Kwahiyo hata wanawake thamani yao ikabaki kwenye kuwahudumia wapigania uhuru...

Hatimaye baada ya mapambano ya muda mrefu sana
Dhuluma nyingi sana
Mateso mengi sana
Ukatili mwingi sana
Vifo vingi sana
UKOMBOZI na UHURU vikapatikana kwa kuachiwa Mandela na kuwa Msouth mweusi wa kwanza kuwa rais... Sasa kazi haikuwa ndogo kuwaheshimisha tena weusi... Kuwapa thamani wanayostahili.. Baada ya kudhauliwa kwa miongo mingi

Mipango mingi ikapangwa... Mojawapo ikiwa ni kuwapatia wasouth wote weusi huduma za msingi bure ama kwa bei nafuu.. Mkakati maarufu ni ule wa nyumba million za Mandela....
Fungate ya UKOMBOZI na UHURU vikawabetesha wengi... Wataliwa wakawa watawala bila maandalizi ya kutosha... Bila elimu ya kutosha bila miiko bila uzalendo vya kutosha...
Kasheshe ikaanzia hapa... Kila Msouth mweusi hakutaka tena kuishi kwenye vibanda... Wakataka nyumba za bure za Mandela.. Bati unanunua mwenyewe.... Nyumba za vyumba vitatu... Basi ikawa mtu akiiipata nyumba, akawa na TV ndani na mziki mkubwa basi huyo kawin maisha hataki chochote tena...

UKOMBOZI na UHURU vikawapa jeuri mbaya sana.. Ile nguvu kazi ya taifa ambao asilimia 90 ni vijana wakawa na nguvu kubwa kwenye maamuzi... Msouth mwisho wake wa kufanya kazi ni Ijumaa mchana... Baada ya hapo mlipe chake akalakale bata mpaka Jumapili jioni... Jumatatu anaamka na nauli tu...
Haya ndio yakawa maisha yao... Ndani ya nchi yao huru.....

Uhuru wa Afrika Kusini ukafungua milango kwa mataifa mengine... Wawekezaji wapya wakaja.. Lakini pia watafuta maisha wengine toka mataifa mengine pia hasa ya kiafrika wakamiminika south.. Hawa wakawa hawana shobo wala maringo.. Hawachagui kazi.. Hawachagui maslahi na wanapiga mzigo hadi Jumapili

Wawekezaji wakaona tofauti kubwa kati ya mgeni na mwenyeji... Wakaona tija ya utendaji wa wageni.... Kidogo kidogo wasouth wakaanza kukosa kazi... Wageni wakawa kimbilio la wawekezaji wengi... Wanasiasa wakachelewa kuliona hili... Wakawa busy na yao

Wasouth kuja kushtuka kazi nyingi zikawa zinafanywa na wageni
Wageni wengi wana maendeleo kuliko wao
Wageni wengi wanapendwa na wawekezaji kuliko wao... Chuki ikaanzia hapo...

Wakaanza taratibu kuwadhibiti wageni
Ukitaka Kuishi nao vizuri fuata watakayo wao
Ukitaka Kuishi nao vizuri usiwe na maendeleo yoyote
Ukitaka Kuishi nao vizuri kila weekend mkale bata
Ukitaka kuishi nao vizuri usimiliki Nyumba nzuri, gari au mwanamke mzuri.....

Ukifanya tofauti na haya
Wanakujengea bifu
Wanatafuta watu wakupore
Wanatafuta watu wakupige
Wanakuhmchongea Uhamiaji
Wanakuroga usifanikiwe

Wageni kuja kugundua haya wakabadili mbinu nyingi.... Sasa miongo imepita... Wageni ndio wenye mafanikio kule... Wenyeji bado wako kwenye mawazo mgando ya UKOMBOZI na UHURU.... Bado wako kwenye fungate wakidhani serikali itawafanyia kila kitu... Sasa hawana aibu tena hawawataki wageni kwasababu ya uvivu wao.... Ni mwendo wa mauaji

#RIP Charles (Mak. ma)
#RIP SundiOmolo
#RIP Makaveli
#RIP Kapinga
# RIP Mandy
My college mates.... Wote hawa vifo vyao vilitokana na mikono dhalimu ya weusi wenzao

Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwakuwa nilinusurika kifo mara nne nikiwa South
Mara ya kwanza ghetto kwa demu... Nilitoroka kupitia dirisha dogo la chooni wakati jamaa wanavunja mlango waingie wanimalize...
Mara ya pili bar ya Zithobeni niliwahi kuikwepa chupa ya bia in split of seconds nikiwa na demu huyo huyo wa kule ghetto
Mara ya tatu usiku huo huo nilitekwa ila nikafanikiwa kuruka kwenye gari na kujisalimisha kwa police waliokuwa kwenye patrol
Mara ya NNE kwenye kanisa la kuabudu shetani Witbank.... [emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]

Maybe I was left to tell...!!!
Ok baharia mstaafu tumekupata. (RIP) ndugu zetu
 
pole sana mkuu ila hata huku tunawaona wanapenda bata mnoo wakishapokea pesa ya jin ni kula mziki ijumaa mpaka jumapili myu analewa siku mbili anakunywa tuu aisee
 
na wanaona wapo wana maendeleao sana ila nimekuja kugundua ni wavivu mnoo na wana roho mbaya ila mademu wao wakipenda wanapenda kweli mzee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
demu atafanya kila kitu wao ni kupakua tuu ndio wanapenda ukiweza hiyo hata kama huna pesa mno atakuvumilia na wana wivu mnoo mnooo hatari
 
Inawezekana walipigwa repatriation halafu wakaishia jela za Msumbiji
Aloyce Kapinga ambaye kwasasa ni marehemu aliwahi kupitia hiyo hali... Baada ya kukamatwa kule mahabusu akakutana wa wajuzi wakamwambia asiseme anatoka bongo kwakuwa atarudishwa kwa ndege bali aseme anatokea Msumbiji ambapo safari ni kwa train
Kwanini safari ya train ni nzuri? Kwa vile kuna chances za kutoroka...
Yeye alifanya hivyo na train ilipofika huko katikati mbugani kwenye kona kali ikapunguza mwendo kuepusha ajali hapa ndio maaskari wasindikizaji huwatangazia wale waliokamatwa mwenye RAND 100 atoe apewe nafasi ya kuruka kabla treni halijamaliza kona na kuongeza mwendo
Kapinga na vijana wengine wawili wakatoa... Lakini baada tu ya kutoa wakasachiwa tena na kuchukuliwa pesa zao nyingine kisha wakaruhusiwa kuruka
Kapinga aliruka na kutua salama lakini kijana mmoja alivunjika niguu yote.. Hapo hakukuwa na kusaidiana kila mmoja alijua lwake

Mkuu,sababu ya wabongo wengi kusema wanatokea msumbiji,hasa hasa kwa miaka ya nyuma ni,
Kitambo kile ukirudishwa kutoka nje,ukifika bongo unapandishwa mahakamami,na kama huna mpunga wa kulipa fine unakwenda jela.

Msumbiji na AK,ni karibu sana na gharama za kurudi tena AK ni ndogo sana kufananisha na gharama za kutoka bongo kurudi tena AK,sasa kwa vile wabangu bangu tangu zamani wao wakirudishwa kwao na train wanabwagwa tu Maputo,hakuna cha kesi wala nini,wabongo wakaona hiyo fursa,wanajifanya wao wabangu bangu,wakimwagwa tu Maputo,wanafanya maujanja ujanja flani then wanageuka tena AK
 
Kingine South Africa uadilifu ni Zero nchi zetu hizi angalau kuna chembechembe za uadilifu, ila SA hakuna kabisa kuanzia raia wa kawaida, kiongozi hadi polisi. Polisi wanawaogopa sana watu wake nani atamfunga paka kengele?

Hebu tujiulize sheria zao za uhamiaji zikoje hadi watu waingie watakavyo? Hili limewashinda kabisa ku control for decades. Madawa ndio kabisaa nchi inanuka madawa, polisi ni wala rushwa wakutupwa.
Polisi wanaogopa kwa sababu ya watu kumiliki bunduki, ndio maana police wanaogopa wananchi. Nchi ikishindwa kwy umiliki wa bunduki ndio inakuwaga ivyo. Tanzania sio kwamba watu waoga ili watu kumiliki bunduki hakuna kabisa. Watu wakimiliki bunduki ni kuheshimiana hakuna ambae analeta kudharauriana
 
Umechoma moto Wachina wasiopungua wane waliouliwa huko.....

HUJAELEWEKA HAPA,UNAMAANISHA NINI?AU WIKENDI ILISHAANZA NA KICHWANI ZIMO ZA MOJA BARIDI,MOJA MOTO??Hahahahaha!!!
Wachina wanauliwa tena sana tu nimechoma moto wachina wasiopungua wane waliouliwa huko... Kuna majiji hakuna hizo shida
Matatizo yako Jo'burg Cape na Durban na Pretoria kidogo tena baadhi ya mitaa..
Kule kwenye virugu mechi kama hillbrow ndio fujo hutokea na mauaji ni jambo la kawaida kabisa
 
Back
Top Bottom