#BahariaGLOBALNEWS Watu wasiopungua 11 wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya watu wenye silaha kuvamia nyumba moja ya makazi katika eneo la KwaMakhutha, karibu na Jiji la Durban, Afrika Kusini.
Polisi wameeleza kuwa wavamizi hao watatu waliingia usiku wa kuamkia leo na kuwafyatulia risasi watu 14 waliokuwa wakifanya sherehe ndani ya nyumba hiyo, ambapo watu 10 walifariki papo hapo na wengine wanne wakakimbizwa hospitalini kabla ya mmoja wao kufariki baadaye.
Miongoni mwa waliopoteza maisha katika shambulio hilo ni mwanamke mmoja anayesadikiwa kuwa mjamzito, aliyekuwa pamoja na wanaume 13 waliokuwa wakishiriki sherehe hiyo.
Jeshi la Polisi limebainisha kuwa baadhi ya waathirika walikuwa chini ya uangalizi wa kisheria kutokana na kuhusishwa na shughuli haramu, ingawa maelezo zaidi yamehifadhiwa ili kutoathiri upelelezi unaoendelea.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi halijaondoa uwezekano wa shambulio hilo kutokana na migogoro na visasi kati ya makundi hasimu ya kihalifu.
Hadi sasa msako mkali unaendelea kuwasaka watuhumiwa hao watatu waliofanya mauaji hayo ya kutisha na kutokomea kusiwe na taarifa rasmi ya kukamatwa kwao.
Source BBC
I know you will say it's foreigners, and you're very good to protect your own people who committed crimes. #southafrica #capetown #pretoria #durban #fblifestyle #goviral #goviralreels #hilights #flyp
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.