Afrika Kusini niijuavyo mimi

Afrika Kusini niijuavyo mimi

Nimeishi South kwa takriban miaka mitano hivi kuanzia 1996 ni mara baada ya Mandela kuachia hatamu na kumkabidhi Thabo Mbeki kijiti.... Kinachotokea sasa huko kina mizizi na ubaguzi wa rangi lakini vilevile kina mizizi na uhuru bila maandalizi mtambuka
Nisirudi nyuma sana kihistoria... Lakini wazungu wahamiaji baada ya kutua kwenye nchi nzuri ya kuvutia ya Africa Kusini, wakaitamani na kupanga mipango ya kuitawala milele.... Hili walifanikiwa kwa kiasi kikubwa mno na wasouth walipokuja kushtuka tayari wakawa kwenye 18 za wazungu
. Wakabaguliwa kwa kila hali
. Wakaundiwa matabaka
. Wakanyimwa elimu
. Wakapenyezewa vibaraka ili wapelelezane wao kwa wao
. Wakanyimwa nafasi za kazi nzuri na maisha yanayomstahili binadamu
. Wale waliogutuka na kutaka kuwakomboa wenzao wakateswa
wakafungwa,
wakazushiwa kesi kubwa kubwa,
wengine wakauliwa na
wengine wakawekwa kizuizini

Binadamu hafugiki kama mnyama... Mapambano ya kudai nchi yao na uhuru wao vikazidi kupamba moto.. Ni katika kipindi hiki wasouth kwa makabila yao yote wakawa kitu kimoja... Ikawa ni mwiko kubaguana
Yakajengwa makambi mengi ya kudai uhuru.. Sauti ikawa moja tu UKOMBOZI NA UHURU basi... Maadili mengine yote yakawekwa kando...
Uadilifu
Utu wema
Upendo
Tafakuri
Maono nknk
Haya yote yakawekwa kwenye kabrasha moja tu UKOMBOZI na UHURU.. Kwahiyo hata wanawake thamani yao ikabaki kwenye kuwahudumia wapigania uhuru...

Hatimaye baada ya mapambano ya muda mrefu sana
Dhuluma nyingi sana
Mateso mengi sana
Ukatili mwingi sana
Vifo vingi sana
UKOMBOZI na UHURU vikapatikana kwa kuachiwa Mandela na kuwa Msouth mweusi wa kwanza kuwa rais... Sasa kazi haikuwa ndogo kuwaheshimisha tena weusi... Kuwapa thamani wanayostahili.. Baada ya kudhauliwa kwa miongo mingi

Mipango mingi ikapangwa... Mojawapo ikiwa ni kuwapatia wasouth wote weusi huduma za msingi bure ama kwa bei nafuu.. Mkakati maarufu ni ule wa nyumba million za Mandela....
Fungate ya UKOMBOZI na UHURU vikawabetesha wengi... Wataliwa wakawa watawala bila maandalizi ya kutosha... Bila elimu ya kutosha bila miiko bila uzalendo vya kutosha...
Kasheshe ikaanzia hapa... Kila Msouth mweusi hakutaka tena kuishi kwenye vibanda... Wakataka nyumba za bure za Mandela.. Bati unanunua mwenyewe.... Nyumba za vyumba vitatu... Basi ikawa mtu akiiipata nyumba, akawa na TV ndani na mziki mkubwa basi huyo kawin maisha hataki chochote tena...

UKOMBOZI na UHURU vikawapa jeuri mbaya sana.. Ile nguvu kazi ya taifa ambao asilimia 90 ni vijana wakawa na nguvu kubwa kwenye maamuzi... Msouth mwisho wake wa kufanya kazi ni Ijumaa mchana... Baada ya hapo mlipe chake akalakale bata mpaka Jumapili jioni... Jumatatu anaamka na nauli tu...
Haya ndio yakawa maisha yao... Ndani ya nchi yao huru.....

Uhuru wa Afrika Kusini ukafungua milango kwa mataifa mengine... Wawekezaji wapya wakaja.. Lakini pia watafuta maisha wengine toka mataifa mengine pia hasa ya kiafrika wakamiminika south.. Hawa wakawa hawana shobo wala maringo.. Hawachagui kazi.. Hawachagui maslahi na wanapiga mzigo hadi Jumapili

Wawekezaji wakaona tofauti kubwa kati ya mgeni na mwenyeji... Wakaona tija ya utendaji wa wageni.... Kidogo kidogo wasouth wakaanza kukosa kazi... Wageni wakawa kimbilio la wawekezaji wengi... Wanasiasa wakachelewa kuliona hili... Wakawa busy na yao

Wasouth kuja kushtuka kazi nyingi zikawa zinafanywa na wageni
Wageni wengi wana maendeleo kuliko wao
Wageni wengi wanapendwa na wawekezaji kuliko wao... Chuki ikaanzia hapo...

Wakaanza taratibu kuwadhibiti wageni
Ukitaka Kuishi nao vizuri fuata watakayo wao
Ukitaka Kuishi nao vizuri usiwe na maendeleo yoyote
Ukitaka Kuishi nao vizuri kila weekend mkale bata
Ukitaka kuishi nao vizuri usimiliki Nyumba nzuri, gari au mwanamke mzuri.....

Ukifanya tofauti na haya
Wanakujengea bifu
Wanatafuta watu wakupore
Wanatafuta watu wakupige
Wanakuhmchongea Uhamiaji
Wanakuroga usifanikiwe

Wageni kuja kugundua haya wakabadili mbinu nyingi.... Sasa miongo imepita... Wageni ndio wenye mafanikio kule... Wenyeji bado wako kwenye mawazo mgando ya UKOMBOZI na UHURU.... Bado wako kwenye fungate wakidhani serikali itawafanyia kila kitu... Sasa hawana aibu tena hawawataki wageni kwasababu ya uvivu wao.... Ni mwendo wa mauaji

#RIP Charles (Mak. ma)
#RIP SundiOmolo
#RIP Makaveli
#RIP Kapinga
# RIP Mandy
My college mates.... Wote hawa vifo vyao vilitokana na mikono dhalimu ya weusi wenzao

Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwakuwa nilinusurika kifo mara nne nikiwa South
Mara ya kwanza ghetto kwa demu... Nilitoroka kupitia dirisha dogo la chooni wakati jamaa wanavunja mlango waingie wanimalize...
Mara ya pili bar ya Zithobeni niliwahi kuikwepa chupa ya bia in split of seconds nikiwa na demu huyo huyo wa kule ghetto
Mara ya tatu usiku huo huo nilitekwa ila nikafanikiwa kuruka kwenye gari na kujisalimisha kwa police waliokuwa kwenye patrol
Mara ya NNE kwenye kanisa la kuabudu shetani Witbank.... [emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]

Maybe I was left to tell...!!!
Unaonesha kweli ulikaa SA na kuifahamu....

R.I.P kwa wote waliotangulia kwa figisu izo na wanaoendelea kufa huko SA...

Hapo mwisho kama filamu ya kuigiza mkuu [emoji75]
 
Mkuu dizain flani kama umefupisha story, lakini asante sana kwa ku share na sisi yapo mengi ya kujifunza hasa pale unapotamani kwenda nchi ya watu.
 
Yeah labda niandike kitabu ndio naweza kusimulia kila kitu vizuri
 
Bro umepita kona nyingi sana katika haya maisha, kichwa chako kimebeba memories za kutosha.

Hongera sana.. . [emoji4]
 
Kama wateja wapo waacheni vijana wafanye kazi. Bora wauze kuliko kutumia. Unga uko kila nchi humu duniani, sidhani kama wabongo ndio wauzaji.
Mimi nina ndugu yangu wa damu. Alizamia huko SA na yeye mishe zake ndio hizo za kufanya biashara haramu.
 
Unaonesha kweli ulikaa SA na kuifahamu....

R.I.P kwa wote waliotangulia kwa figisu izo na wanaoendelea kufa huko SA...

Hapo mwisho kama filamu ya kuigiza mkuu [emoji75]
Ukisimulia unitag mkuu
Hapa ndio chuo tulisoma... Mazingira ya sasa yamebadilika mno.... Hapo tumetoka darasani tunaenda lunch temple.... Kila kitu ilikuwa ni sheria... Mpaka kutembea
2269239_orig.jpeg
 
Kwa mtazamo wangu naona Luna mkono Wa Wazungu, HawA jamaa hawatupendi na wanatumia kila njia kuhakikisha kuwa bara la Afrika halitulii,haiwezekani tukaua na wenyewe kama hamna uchochezi, huo uchochezi wanajua utasambaa Afrika nzima, device and rule, tusubiri tutaona mengi
Hadi karne hii ya 21 kuendelea kuwalumu wazungu ni kujikosea heshima na kubainisha kwamba tuna uwezo mdogo wa kufikiri. Mbona wahindi walitawaliwa na muingereza lakini hatuwasikii wakilalamika kama sisi.
 
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji117][emoji117][emoji117][emoji117]Announcement to all All South Africans. President Cytill Ramaphosa, Minister Bheki Cele, Minister of Home Afairs Motsoaledi you have failed the country nizoyikhomba ibhenge yomile, Sizozibambela umthetho ngezandla akufe ofayo this is our Country our Ancestors died for that you are giving to Foreigners, As Amazulu Sithukuthele siganwe unwabu sizobulala kwasani , From the 09 September 2019 at 7am whole September .All Churches , Business , Schools that are run by Foreigners must be closed they will be fire and blood. All the Tax Ranks will be closed , Hospital, All Departments to march to Homes affairs National and office of the President of Southafrica to take an urgent action against the removing all the foreigners in the country We will sleep even in the Mountains to fix this Country . The strike will go to all Provinces all cities,Township and villages . Tax owners are taking charge now .If you are foreign you should have been by the border gate as now and Aiports will be busy for The whole September we are cleaning Southafrica now. No foreigners from Nageria and Malawi,Tanzania, Congo, Ghana will be allowed in the aiports coming to Southafrica. All airports will be not operating whole September we are closing all gates and we will bunt down even the aiports in Southafrica. If the President is not taking action they will be blood all over the world. Every Business whole September must be closed down include all their Internet Cafe stations especially Hillbrow, Down town Witbank,Point Durban ,South Beach durban,Sunnyside Pretoria, Kemptonpark, Yeoville,Jhb CBD, Capetown all over ,Nelspruit and Polokwane, We are killing and destroying all their business ,Shops for clothing.We dont event want their Airlines to come to mzansi anymore. All places where they operate with Corruptions each street will be closed down .Their flats will be burnt down ,their cars they will be killed , Till all foreigners are back to their countries. Each houses that have foreigners especially in Witbank, Nelspruit, Durban and Capetown and PE,Durban .look what Omotos and Bushiri Did to our Country. South African didn't not open Churches and Business in their foreign Countries . All the freeway will be a closed down for business operators. All buildings, busines , Malls that will be operating from nextweek will be burnt down , Convoy to Pretoria. We are doing what the President Cyril Ramaphosa said # Thuma mina.We want to bring back the dignity of Southafrica not the place of Corruption and Drugs dealers .
Note
# They will be Blood and Death, Fire all all over until Southafrica is clean .Only if we are united and one this country will be clean . All foreigners Pack your staff and go within 48 hours.
# Thuma mina
# We are fixing Southafrica
# Drugs dealers must fall
# Corruption must end .
2020 Southafrica will be a place of Peace

Hali inazidi kuwa mbaya... Viongozi wa SADC wako kimya
 
Chuo cha nini hicho mkuu ?
Ingia hapa

Back
Top Bottom