Afrika Kusini niijuavyo mimi

Afrika Kusini niijuavyo mimi

Umechoma moto Wachina wasiopungua wane waliouliwa huko.....

HUJAELEWEKA HAPA,UNAMAANISHA NINI?AU WIKENDI ILISHAANZA NA KICHWANI ZIMO ZA MOJA BARIDI,MOJA MOTO??Hahahahaha!!!
Wachina wakifa wanachomwa moto... Hawaziki kama sisi
 
Kumbe ndo ulichosomea pia kwenye ubuddha, je ndo shughuli unayoifanya pia hapa bongo kuchoma wachina?
Yeah kwenye ubudha... Hapana hapa home napiga ishu nyingine kabisa
 
hahahaha Mkuu ata kama ungekua na gari hapo ungeliweka kwenye mfuko wa suruali na ukatimua mbio kaliii
[emoji848][emoji15][emoji23][emoji13][emoji13][emoji12][emoji12][emoji23][emoji23]
 
Nimeishi South kwa takriban miaka mitano hivi kuanzia 1996 ni mara baada ya Mandela kuachia hatamu na kumkabidhi Thabo Mbeki kijiti.... Kinachotokea sasa huko kina mizizi na ubaguzi wa rangi lakini vilevile kina mizizi na uhuru bila maandalizi mtambuka
Nisirudi nyuma sana kihistoria... Lakini wazungu wahamiaji baada ya kutua kwenye nchi nzuri ya kuvutia ya Africa Kusini, wakaitamani na kupanga mipango ya kuitawala milele.... Hili walifanikiwa kwa kiasi kikubwa mno na wasouth walipokuja kushtuka tayari wakawa kwenye 18 za wazungu
. Wakabaguliwa kwa kila hali
. Wakaundiwa matabaka
. Wakanyimwa elimu
. Wakapenyezewa vibaraka ili wapelelezane wao kwa wao
. Wakanyimwa nafasi za kazi nzuri na maisha yanayomstahili binadamu
. Wale waliogutuka na kutaka kuwakomboa wenzao wakateswa
wakafungwa,
wakazushiwa kesi kubwa kubwa,
wengine wakauliwa na
wengine wakawekwa kizuizini

Binadamu hafugiki kama mnyama... Mapambano ya kudai nchi yao na uhuru wao vikazidi kupamba moto.. Ni katika kipindi hiki wasouth kwa makabila yao yote wakawa kitu kimoja... Ikawa ni mwiko kubaguana
Yakajengwa makambi mengi ya kudai uhuru.. Sauti ikawa moja tu UKOMBOZI NA UHURU basi... Maadili mengine yote yakawekwa kando...
Uadilifu
Utu wema
Upendo
Tafakuri
Maono nknk
Haya yote yakawekwa kwenye kabrasha moja tu UKOMBOZI na UHURU.. Kwahiyo hata wanawake thamani yao ikabaki kwenye kuwahudumia wapigania uhuru...

Hatimaye baada ya mapambano ya muda mrefu sana
Dhuluma nyingi sana
Mateso mengi sana
Ukatili mwingi sana
Vifo vingi sana
UKOMBOZI na UHURU vikapatikana kwa kuachiwa Mandela na kuwa Msouth mweusi wa kwanza kuwa rais... Sasa kazi haikuwa ndogo kuwaheshimisha tena weusi... Kuwapa thamani wanayostahili.. Baada ya kudhauliwa kwa miongo mingi

Mipango mingi ikapangwa... Mojawapo ikiwa ni kuwapatia wasouth wote weusi huduma za msingi bure ama kwa bei nafuu.. Mkakati maarufu ni ule wa nyumba million za Mandela....
Fungate ya UKOMBOZI na UHURU vikawabetesha wengi... Wataliwa wakawa watawala bila maandalizi ya kutosha... Bila elimu ya kutosha bila miiko bila uzalendo vya kutosha...
Kasheshe ikaanzia hapa... Kila Msouth mweusi hakutaka tena kuishi kwenye vibanda... Wakataka nyumba za bure za Mandela.. Bati unanunua mwenyewe.... Nyumba za vyumba vitatu... Basi ikawa mtu akiiipata nyumba, akawa na TV ndani na mziki mkubwa basi huyo kawin maisha hataki chochote tena...

UKOMBOZI na UHURU vikawapa jeuri mbaya sana.. Ile nguvu kazi ya taifa ambao asilimia 90 ni vijana wakawa na nguvu kubwa kwenye maamuzi... Msouth mwisho wake wa kufanya kazi ni Ijumaa mchana... Baada ya hapo mlipe chake akalakale bata mpaka Jumapili jioni... Jumatatu anaamka na nauli tu...
Haya ndio yakawa maisha yao... Ndani ya nchi yao huru.....

Uhuru wa Afrika Kusini ukafungua milango kwa mataifa mengine... Wawekezaji wapya wakaja.. Lakini pia watafuta maisha wengine toka mataifa mengine pia hasa ya kiafrika wakamiminika south.. Hawa wakawa hawana shobo wala maringo.. Hawachagui kazi.. Hawachagui maslahi na wanapiga mzigo hadi Jumapili

Wawekezaji wakaona tofauti kubwa kati ya mgeni na mwenyeji... Wakaona tija ya utendaji wa wageni.... Kidogo kidogo wasouth wakaanza kukosa kazi... Wageni wakawa kimbilio la wawekezaji wengi... Wanasiasa wakachelewa kuliona hili... Wakawa busy na yao

Wasouth kuja kushtuka kazi nyingi zikawa zinafanywa na wageni
Wageni wengi wana maendeleo kuliko wao
Wageni wengi wanapendwa na wawekezaji kuliko wao... Chuki ikaanzia hapo...

Wakaanza taratibu kuwadhibiti wageni
Ukitaka Kuishi nao vizuri fuata watakayo wao
Ukitaka Kuishi nao vizuri usiwe na maendeleo yoyote
Ukitaka Kuishi nao vizuri kila weekend mkale bata
Ukitaka kuishi nao vizuri usimiliki Nyumba nzuri, gari au mwanamke mzuri.....

Ukifanya tofauti na haya
Wanakujengea bifu
Wanatafuta watu wakupore
Wanatafuta watu wakupige
Wanakuhmchongea Uhamiaji
Wanakuroga usifanikiwe

Wageni kuja kugundua haya wakabadili mbinu nyingi.... Sasa miongo imepita... Wageni ndio wenye mafanikio kule... Wenyeji bado wako kwenye mawazo mgando ya UKOMBOZI na UHURU.... Bado wako kwenye fungate wakidhani serikali itawafanyia kila kitu... Sasa hawana aibu tena hawawataki wageni kwasababu ya uvivu wao.... Ni mwendo wa mauaji

#RIP Charles (Mak. ma)
#RIP SundiOmolo
#RIP Makaveli
#RIP Kapinga
# RIP Mandy
My college mates.... Wote hawa vifo vyao vilitokana na mikono dhalimu ya weusi wenzao

Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwakuwa nilinusurika kifo mara nne nikiwa South
Mara ya kwanza ghetto kwa demu... Nilitoroka kupitia dirisha dogo la chooni wakati jamaa wanavunja mlango waingie wanimalize...
Mara ya pili bar ya Zithobeni niliwahi kuikwepa chupa ya bia in split of seconds nikiwa na demu huyo huyo wa kule ghetto
Mara ya tatu usiku huo huo nilitekwa ila nikafanikiwa kuruka kwenye gari na kujisalimisha kwa police waliokuwa kwenye patrol
Mara ya NNE kwenye kanisa la kuabudu shetani Witbank.... [emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]

Maybe I was left to tell...!!!
Kumbe na wewe unaabudu mashetani?

Very strange!
 
Ungeijua nguvu yake ungefuta kauli yako hiyo... Wewe mwenyewe ni mfuasi wake mwaminifu lakini hujitambui
Quran 18:50

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَٰٓئِكَةِ ٱسْجُدُوا۟ لِءَادَمَ فَسَجَدُوٓا۟ إِلَّآ إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ ٱلْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِۦٓۗ أَفَتَتَّخِذُونَهُۥ وَذُرِّيَّتَهُۥٓ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِى وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّۢۚ بِئْسَ لِلظَّٰلِمِينَ بَدَلًا

We said to the angels, ‘Bow down before Adam,’ and they all bowed down, but not Iblis: he was one of the jinn and he disobeyed his Lord’s command. Are you [people] going to take him and his offspring as your masters instead of Me, even though they are your enemies? What a bad bargain for the evildoers!
 
Hawa jamaa ni wapenda starehe sana.Nimefanya nao huku wao ni pombe na kupenda wanawake.
Tatizo Wazulu wanajiona kama Africa kusini ndio wao wamiliki halali wa nchi hiyo.
Uvivu wao ndio chanzo wageni kuaminiwa
 
Mwenyekiti afanye nini wakati nchi ile ina uongozi ambao upo ndani ya SADC..yote hii kutafuta choko choko kwa jina moja tu John Pombe. waTanzania bwana
Wa S.A wanatuhuzunisha sana,Mwenyekiti na yeye kapiga Kimya,AU kimya! Trump katema Cheche lakini Mwenyekiti wa SADC kimya.
 
Quran 18:50

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَٰٓئِكَةِ ٱسْجُدُوا۟ لِءَادَمَ فَسَجَدُوٓا۟ إِلَّآ إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ ٱلْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِۦٓۗ أَفَتَتَّخِذُونَهُۥ وَذُرِّيَّتَهُۥٓ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِى وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّۢۚ بِئْسَ لِلظَّٰلِمِينَ بَدَلًا

We said to the angels, ‘Bow down before Adam,’ and they all bowed down, but not Iblis: he was one of the jinn and he disobeyed his Lord’s command. Are you [people] going to take him and his offspring as your masters instead of Me, even though they are your enemies? What a bad bargain for the evildoers!
Unapoingia (log in) kwenye account zako mitandaoni huwa unatumia password (namba au neno la siri)
Unapotaka kufanya miamala mbalimbali aidha bank, kwenye simu yako nk unatumia neno ama namba ya siri kuweza kukamilisha miamala...
Unapoingia mitandaoni ili usome Quran unatumia no ya siri ama neno....

Unafahamu tafsiri ya namba ya siri? Wote sisi ni wafuasi waaminifu wa shetani... Bila kuwa mfuasi wake huwezi kuuishi hii dunia.... NaMBA YA SIRI ndio INATAWALA DUNIA na ndio inaitwa namba ya mpinga Kristo
 
Unapoingia (log in) kwenye account zako mitandaoni huwa unatumia password (namba au neno la siri)
Unapotaka kufanya miamala mbalimbali aidha bank, kwenye simu yako nk unatumia neno ama namba ya siri kuweza kukamilisha miamala...
Unapoingia mitandaoni ili usome Quran unatumia no ya siri ama neno....

Unafahamu tafsiri ya namba ya siri? Wote sisi ni wafuasi waaminifu wa shetani... Bila kuwa mfuasi wake huwezi kuuishi hii dunia.... NaMBA YA SIRI ndio INATAWALA DUNIA na ndio inaitwa namba ya mpinga Kristo
Hebu tufafanulie hapa kidogo, ina maana mimi nikiweka Nywila yangu kwa mfano 2000 au Kiduila tayari nimeshamuabudu Shetani?
 
Hebu tufafanulie hapa kidogo, ina maana mimi nikiweka Nywila yangu kwa mfano 2000 au Kiduila tayari nimeshamuabudu Shetani?
Si lazima lakini jiulize kama una nywila moja tu unayotumia kote?
Angalia kwenye manunuzi yako yote.. Je huna kitu chochote chenye barcode?
 
Back
Top Bottom