Nimeishi South kwa takriban miaka mitano hivi kuanzia 1996 ni mara baada ya Mandela kuachia hatamu na kumkabidhi Thabo Mbeki kijiti.... Kinachotokea sasa huko kina mizizi na ubaguzi wa rangi lakini vilevile kina mizizi na uhuru bila maandalizi mtambuka
Nisirudi nyuma sana kihistoria... Lakini wazungu wahamiaji baada ya kutua kwenye nchi nzuri ya kuvutia ya Africa Kusini, wakaitamani na kupanga mipango ya kuitawala milele.... Hili walifanikiwa kwa kiasi kikubwa mno na wasouth walipokuja kushtuka tayari wakawa kwenye 18 za wazungu
. Wakabaguliwa kwa kila hali
. Wakaundiwa matabaka
. Wakanyimwa elimu
. Wakapenyezewa vibaraka ili wapelelezane wao kwa wao
. Wakanyimwa nafasi za kazi nzuri na maisha yanayomstahili binadamu
. Wale waliogutuka na kutaka kuwakomboa wenzao wakateswa
wakafungwa,
wakazushiwa kesi kubwa kubwa,
wengine wakauliwa na
wengine wakawekwa kizuizini
Binadamu hafugiki kama mnyama... Mapambano ya kudai nchi yao na uhuru wao vikazidi kupamba moto.. Ni katika kipindi hiki wasouth kwa makabila yao yote wakawa kitu kimoja... Ikawa ni mwiko kubaguana
Yakajengwa makambi mengi ya kudai uhuru.. Sauti ikawa moja tu UKOMBOZI NA UHURU basi... Maadili mengine yote yakawekwa kando...
Uadilifu
Utu wema
Upendo
Tafakuri
Maono nknk
Haya yote yakawekwa kwenye kabrasha moja tu UKOMBOZI na UHURU.. Kwahiyo hata wanawake thamani yao ikabaki kwenye kuwahudumia wapigania uhuru...
Hatimaye baada ya mapambano ya muda mrefu sana
Dhuluma nyingi sana
Mateso mengi sana
Ukatili mwingi sana
Vifo vingi sana
UKOMBOZI na UHURU vikapatikana kwa kuachiwa Mandela na kuwa Msouth mweusi wa kwanza kuwa rais... Sasa kazi haikuwa ndogo kuwaheshimisha tena weusi... Kuwapa thamani wanayostahili.. Baada ya kudhauliwa kwa miongo mingi
Mipango mingi ikapangwa... Mojawapo ikiwa ni kuwapatia wasouth wote weusi huduma za msingi bure ama kwa bei nafuu.. Mkakati maarufu ni ule wa nyumba million za Mandela....
Fungate ya UKOMBOZI na UHURU vikawabetesha wengi... Wataliwa wakawa watawala bila maandalizi ya kutosha... Bila elimu ya kutosha bila miiko bila uzalendo vya kutosha...
Kasheshe ikaanzia hapa... Kila Msouth mweusi hakutaka tena kuishi kwenye vibanda... Wakataka nyumba za bure za Mandela.. Bati unanunua mwenyewe.... Nyumba za vyumba vitatu... Basi ikawa mtu akiiipata nyumba, akawa na TV ndani na mziki mkubwa basi huyo kawin maisha hataki chochote tena...
UKOMBOZI na UHURU vikawapa jeuri mbaya sana.. Ile nguvu kazi ya taifa ambao asilimia 90 ni vijana wakawa na nguvu kubwa kwenye maamuzi... Msouth mwisho wake wa kufanya kazi ni Ijumaa mchana... Baada ya hapo mlipe chake akalakale bata mpaka Jumapili jioni... Jumatatu anaamka na nauli tu...
Haya ndio yakawa maisha yao... Ndani ya nchi yao huru.....
Uhuru wa Afrika Kusini ukafungua milango kwa mataifa mengine... Wawekezaji wapya wakaja.. Lakini pia watafuta maisha wengine toka mataifa mengine pia hasa ya kiafrika wakamiminika south.. Hawa wakawa hawana shobo wala maringo.. Hawachagui kazi.. Hawachagui maslahi na wanapiga mzigo hadi Jumapili
Wawekezaji wakaona tofauti kubwa kati ya mgeni na mwenyeji... Wakaona tija ya utendaji wa wageni.... Kidogo kidogo wasouth wakaanza kukosa kazi... Wageni wakawa kimbilio la wawekezaji wengi... Wanasiasa wakachelewa kuliona hili... Wakawa busy na yao
Wasouth kuja kushtuka kazi nyingi zikawa zinafanywa na wageni
Wageni wengi wana maendeleo kuliko wao
Wageni wengi wanapendwa na wawekezaji kuliko wao... Chuki ikaanzia hapo...
Wakaanza taratibu kuwadhibiti wageni
Ukitaka Kuishi nao vizuri fuata watakayo wao
Ukitaka Kuishi nao vizuri usiwe na maendeleo yoyote
Ukitaka Kuishi nao vizuri kila weekend mkale bata
Ukitaka kuishi nao vizuri usimiliki Nyumba nzuri, gari au mwanamke mzuri.....
Ukifanya tofauti na haya
Wanakujengea bifu
Wanatafuta watu wakupore
Wanatafuta watu wakupige
Wanakuhmchongea Uhamiaji
Wanakuroga usifanikiwe
Wageni kuja kugundua haya wakabadili mbinu nyingi.... Sasa miongo imepita... Wageni ndio wenye mafanikio kule... Wenyeji bado wako kwenye mawazo mgando ya UKOMBOZI na UHURU.... Bado wako kwenye fungate wakidhani serikali itawafanyia kila kitu... Sasa hawana aibu tena hawawataki wageni kwasababu ya uvivu wao.... Ni mwendo wa mauaji
#RIP Charles (Mak. ma)
#RIP SundiOmolo
#RIP Makaveli
#RIP Kapinga
# RIP Mandy
My college mates.... Wote hawa vifo vyao vilitokana na mikono dhalimu ya weusi wenzao
Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwakuwa nilinusurika kifo mara nne nikiwa South
Mara ya kwanza ghetto kwa demu... Nilitoroka kupitia dirisha dogo la chooni wakati jamaa wanavunja mlango waingie wanimalize...
Mara ya pili bar ya Zithobeni niliwahi kuikwepa chupa ya bia in split of seconds nikiwa na demu huyo huyo wa kule ghetto
Mara ya tatu usiku huo huo nilitekwa ila nikafanikiwa kuruka kwenye gari na kujisalimisha kwa police waliokuwa kwenye patrol
Mara ya NNE kwenye kanisa la kuabudu shetani Witbank.... [emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]
Maybe I was left to tell...!!!
Hayamhusu
Wachina wanauliwa tena sana tu nimechoma moto wachina wasiopungua wane waliouliwa huko... Kuna majiji hakuna hizo shidaWa South wanaweza kuwa na hoja ya wao kutengwa na uchumi nchini mwao lakini sio kuwauwa weusi wenzao.
Ukakasi wa vurugu hizi mbona hauwagusi Wazungu,Waarabu,Wachina,Wahindi na Jamii nyingine nyeupe wahamiaji wanaoishi nchini humo?Kwanini ni ndugu zao weusi tu wanawaua,kuwaharibia mali,nk?
Halafu mara nyingi vurugu zao huwa hazitamalaki sana Johannesburg, wanaogopa mikono ya mabeberu itaeashughulikia kwa sababu ya uwekezaji mkubwa wa mabeberu au?
Mshana Jr hebu jipinde kutudadavulia kwa haya mawili niliyouliza.
Naukumbuka vizuri sana... Kama umeufuatilia vizuri story za bongo nimesimulia miaka ya kuanzia 90-96 halafu nikaendelea kuanzia 2001Miaka iyo iyo ndio aliyoishi Mwananyamala, temeke, ubungo kibo, manzese na sehemu nyingine. Wewe mshana jr. Unakumbuka uzi wako wa miaka iyo uliishi sehemu izo
Nilimaliza masomo yangu na kwenda mashariki ya kati ila kuna baadhi sijasimulia hapa kutokana na ufinyu wa muda ila kuna visa vichache nitasimulia baadaeMkuu endelea kidogo inavutia sana...endelea kidogo mwisho wako ulikuaje huko Kwa Madiba
EeeNimeishi South kwa takriban miaka mitano hivi kuanzia 1996 ni mara baada ya Mandela kuachia hatamu na kumkabidhi Thabo Mbeki kijiti.... Kinachotokea sasa huko kina mizizi na ubaguzi wa rangi lakini vilevile kina mizizi na uhuru bila maandalizi mtambuka
Nisirudi nyuma sana kihistoria... Lakini wazungu wahamiaji baada ya kutua kwenye nchi nzuri ya kuvutia ya Africa Kusini, wakaitamani na kupanga mipango ya kuitawala milele.... Hili walifanikiwa kwa kiasi kikubwa mno na wasouth walipokuja kushtuka tayari wakawa kwenye 18 za wazungu
. Wakabaguliwa kwa kila hali
. Wakaundiwa matabaka
. Wakanyimwa elimu
. Wakapenyezewa vibaraka ili wapelelezane wao kwa wao
. Wakanyimwa nafasi za kazi nzuri na maisha yanayomstahili binadamu
. Wale waliogutuka na kutaka kuwakomboa wenzao wakateswa
wakafungwa,
wakazushiwa kesi kubwa kubwa,
wengine wakauliwa na
wengine wakawekwa kizuizini
Binadamu hafugiki kama mnyama... Mapambano ya kudai nchi yao na uhuru wao vikazidi kupamba moto.. Ni katika kipindi hiki wasouth kwa makabila yao yote wakawa kitu kimoja... Ikawa ni mwiko kubaguana
Yakajengwa makambi mengi ya kudai uhuru.. Sauti ikawa moja tu UKOMBOZI NA UHURU basi... Maadili mengine yote yakawekwa kando...
Uadilifu
Utu wema
Upendo
Tafakuri
Maono nknk
Haya yote yakawekwa kwenye kabrasha moja tu UKOMBOZI na UHURU.. Kwahiyo hata wanawake thamani yao ikabaki kwenye kuwahudumia wapigania uhuru...
Hatimaye baada ya mapambano ya muda mrefu sana
Dhuluma nyingi sana
Mateso mengi sana
Ukatili mwingi sana
Vifo vingi sana
UKOMBOZI na UHURU vikapatikana kwa kuachiwa Mandela na kuwa Msouth mweusi wa kwanza kuwa rais... Sasa kazi haikuwa ndogo kuwaheshimisha tena weusi... Kuwapa thamani wanayostahili.. Baada ya kudhauliwa kwa miongo mingi
Mipango mingi ikapangwa... Mojawapo ikiwa ni kuwapatia wasouth wote weusi huduma za msingi bure ama kwa bei nafuu.. Mkakati maarufu ni ule wa nyumba million za Mandela....
Fungate ya UKOMBOZI na UHURU vikawabetesha wengi... Wataliwa wakawa watawala bila maandalizi ya kutosha... Bila elimu ya kutosha bila miiko bila uzalendo vya kutosha...
Kasheshe ikaanzia hapa... Kila Msouth mweusi hakutaka tena kuishi kwenye vibanda... Wakataka nyumba za bure za Mandela.. Bati unanunua mwenyewe.... Nyumba za vyumba vitatu... Basi ikawa mtu akiiipata nyumba, akawa na TV ndani na mziki mkubwa basi huyo kawin maisha hataki chochote tena...
UKOMBOZI na UHURU vikawapa jeuri mbaya sana.. Ile nguvu kazi ya taifa ambao asilimia 90 ni vijana wakawa na nguvu kubwa kwenye maamuzi... Msouth mwisho wake wa kufanya kazi ni Ijumaa mchana... Baada ya hapo mlipe chake akalakale bata mpaka Jumapili jioni... Jumatatu anaamka na nauli tu...
Haya ndio yakawa maisha yao... Ndani ya nchi yao huru.....
Uhuru wa Afrika Kusini ukafungua milango kwa mataifa mengine... Wawekezaji wapya wakaja.. Lakini pia watafuta maisha wengine toka mataifa mengine pia hasa ya kiafrika wakamiminika south.. Hawa wakawa hawana shobo wala maringo.. Hawachagui kazi.. Hawachagui maslahi na wanapiga mzigo hadi Jumapili
Wawekezaji wakaona tofauti kubwa kati ya mgeni na mwenyeji... Wakaona tija ya utendaji wa wageni.... Kidogo kidogo wasouth wakaanza kukosa kazi... Wageni wakawa kimbilio la wawekezaji wengi... Wanasiasa wakachelewa kuliona hili... Wakawa busy na yao
Wasouth kuja kushtuka kazi nyingi zikawa zinafanywa na wageni
Wageni wengi wana maendeleo kuliko wao
Wageni wengi wanapendwa na wawekezaji kuliko wao... Chuki ikaanzia hapo...
Wakaanza taratibu kuwadhibiti wageni
Ukitaka Kuishi nao vizuri fuata watakayo wao
Ukitaka Kuishi nao vizuri usiwe na maendeleo yoyote
Ukitaka Kuishi nao vizuri kila weekend mkale bata
Ukitaka kuishi nao vizuri usimiliki Nyumba nzuri, gari au mwanamke mzuri.....
Ukifanya tofauti na haya
Wanakujengea bifu
Wanatafuta watu wakupore
Wanatafuta watu wakupige
Wanakuhmchongea Uhamiaji
Wanakuroga usifanikiwe
Wageni kuja kugundua haya wakabadili mbinu nyingi.... Sasa miongo imepita... Wageni ndio wenye mafanikio kule... Wenyeji bado wako kwenye mawazo mgando ya UKOMBOZI na UHURU.... Bado wako kwenye fungate wakidhani serikali itawafanyia kila kitu... Sasa hawana aibu tena hawawataki wageni kwasababu ya uvivu wao.... Ni mwendo wa mauaji
#RIP Charles (Mak. ma)
#RIP SundiOmolo
#RIP Makaveli
#RIP Kapinga
# RIP Mandy
My college mates.... Wote hawa vifo vyao vilitokana na mikono dhalimu ya weusi wenzao
Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwakuwa nilinusurika kifo mara nne nikiwa South
Mara ya kwanza ghetto kwa demu... Nilitoroka kupitia dirisha dogo la chooni wakati jamaa wanavunja mlango waingie wanimalize...
Mara ya pili bar ya Zithobeni niliwahi kuikwepa chupa ya bia in split of seconds nikiwa na demu huyo huyo wa kule ghetto
Mara ya tatu usiku huo huo nilitekwa ila nikafanikiwa kuruka kwenye gari na kujisalimisha kwa police waliokuwa kwenye patrol
Mara ya NNE kwenye kanisa la kuabudu shetani Witbank.... [emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]
Maybe I was left to tell...!!!
Rushwa... Rushwa... Rushwa....Kingine South Africa uadilifu ni Zero nchi zetu hizi angalau kuna chembechembe za uadilifu, ila SA hakuna kabisa kuanzia raia wa kawaida, kiongozi hadi polisi. Polisi wanawaogopa sana watu wake nani atamfunga paka kengele?
Hebu tujiulize sheria zao za uhamiaji zikoje hadi watu waingie watakavyo? Hili limewashinda kabisa ku control for decades. Madawa ndio kabisaa nchi inanuka madawa, polisi ni wala rushwa wakutupwa.
Alafu ndo wanavunja magari ya watu wanaiba laptop, ipad na simu. Ukienda pale kinondoni manyanya mtaa wa bm saloon utakuta wapo kibao pale wanauza iPhone, samsung, tablet zilizoibwa south. Na ukikosa unaambiwa subiri kuna mzigo unaingia toka south wikiendi.Kweli hamna nchi ambayo itakubali kuwa jalala ya wahamiaji haramu.....hata sisi Tz kukubali wa Kenya kufanya kazi ya ualimu wa kiingereze ni issue kubwa licha cha kua hatuna waalimu wa kiingereza wazuri na wakutosha majuzi mkenya alizuiliwa kufanya kazi Voda com kama CEO kwa kulinda ajira ya wa Tz........kwa S.A. ni too much inafika johnesburg unaweza kufikiri ni Lagos Nigeria niwengi kuliko wazawa, nani atakubali hilo kwenye nchi yake amamambazi (high way robbery) na drug dealers 90% ni wa Tz na Nigerians kwanini wafanyie uko sio kwao?
Nilimaliza masomo yangu na kwenda mashariki ya kati ila kuna baadhi sijasimulia hapa kutokana na ufinyu wa muda ila kuna visa vichache nitasimulia baadae
A failed state ndio huruhuru watu kuja kwenye nchi zao ki holela.Kweli hamna nchi ambayo itakubali kuwa jalala ya wahamiaji haramu.....hata sisi Tz kukubali wa Kenya kufanya kazi ya ualimu wa kiingereze ni issue kubwa licha cha kua hatuna waalimu wa kiingereza wazuri na wakutosha majuzi mkenya alizuiliwa kufanya kazi Voda com kama CEO kwa kulinda ajira ya wa Tz........kwa S.A. ni too much inafika johnesburg unaweza kufikiri ni Lagos Nigeria niwengi kuliko wazawa, nani atakubali hilo kwenye nchi yake amamambazi (high way robbery) na drug dealers 90% ni wa Tz na Nigerians kwanini wafanyie uko sio kwao?