Afrika itatawaliwa tena ama itageuzwa dampo la walioendelea

Afrika itatawaliwa tena ama itageuzwa dampo la walioendelea

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,966
Reaction score
51,111
Wakati Mabara na nchi toka kwenye mabara mengine zinawekeza kwenye mbongo za watu wao, Afrika bado watu wake wanatangatanga kwenye lindi la ujinga na udumavu wa akili unaosababisha umaskini wao. Leo hii karibia Afrika nzima serikali zilizoko madarakani ni taasisi za kikandamizi dhidi ya watu wa nchi zao.

Afrika watu wanakwenda shule siyo kupata maarifa bali kukariri maarifa ya mataifa mengine, leo hakuna uwekezaji wa kutosha kuhakikisha kizazi cha ukarne (Millennial Generation) kinaweza kushindana na wenzao toka mabara mengine.

Miaka 30 ijayo ama Afrika itakuja kutawaliwa tena ama itageuzwa kuwa dampo la mabara mengine yaliyoendelea.

Ule uamuzi wa Uingereza kwamba wakimbizi toka Afrika wanaokimbilia Uingereza,sasa watapelekwa Rwanda ni mfano mmojawapo kwamba tunaonekana hatuna faida kwa wengine.
 
Can't imagine, unapiga mbizi kule Mediterranean sea unadakwa halafu unapelekwa Rwanda 🤔.
Wenyewe wanaona kwamba ukienda kule huna faida yoyote. Wakati Ujerumani inafanya kila iwezalo kuhakikisha inakuwa ni rahisi wa kwa Raia wa India wenye ujuzi wa IT kupata Visa za kazi Ujerumani. Lakini wakiona mwafrika mtaani wanachefukwa!!
 
Badili kichwa kisomeke: Africa inatawaliwa, na ni dampo la walioendelea.
 
Back
Top Bottom