Afrika haijatuma msaada wowote Uturuki

Afrika haijatuma msaada wowote Uturuki

Afrika ina tatizo gani, hadi sasa haijatoa msaada wowote ule, hata wa watu kwenda saidia Turkiye katika usaidizi wa kuokoa watu.

~ Ukraine iko vitani ila inapeleka watu

~ Lebanon imepeleka watu

~ India imepeleka watu, madawa, mbwa, vifaa

~ China imepeleka watu (waliojitolea)

~ Marekani inapeleka watu, vifaa, madawa

~ Urusi imepeleka watu na madawa

Afrika tuna tatizo gani?

Lile tetemeko limeshusha nyumba zaidi ya 6000 hawataweza wenyewe.

JWTZ wamekaa tu hawana kazi, kwanini serikali isiwapeleke kusaidia?
na hapo bado tunataka tulipwe pesa za uchafuzi wa mazingira kwasababu tumeyachafua na kukata miti hovyo
 
Tule tunywe tuchezee mbususu, tukwende choo ,tulale siku imeisha unataka tusaidie nini tena hizo sio fani zetu
 
Daah Jaman sisi wenyewe kwangu pakavu tia mchuzi ndio tukatize meditreniani kwenda kutoa msaada
 
Dah ila waafrika tunazingua sana.
 
Ndege tu ilishindakana sembuse hayo, acha wasiende wasijekuaibika.
 
Yatokee huko huko usiombee yatokee huku, nyumba 6000 si mchezo.

Mtu kajenga kasebule na vichumba vhake viwili kwa miaka 7.. Leo kwa sekunde kadhaa kako chini na kila kitu kimefukiwa humo humo..
Mungu tunusuru sisi.
Serikali yao inadai hili tetemeko litaathiri zaidi ya watu milioni 10
Hadi sasa wasio na makazi ni watu 150,000
 
Waturuki ndo wafadhili wakuu kipindi cha mfungo mpaka sikukuu ya Eid,, sasa kwa hili islamic wajiandae kisaikolojia
 
Ndio sasa najua earthquake imetokea Uturuki. 6000 people dead? Hii kazi ya Shetani.
 
Waturuki ndo wafadhili wakuu kipindi cha mfungo mpaka sikukuu ya Eid,, sasa kwa hili islamic wajiandae kisaikolojia
Hadi sasa Iran pekee ndo kaenda, wengine wamekaa kimya
 
Nikutake radhi kaka usiwaseme ndugu zangu wa JWTZ kua wamekaa hawana kazi!!!Unajua undercover ngapi ndugu zangu wa JWTZ wanafanya kwa ajili ya kusaidia watu sehemu mbalimbali duniani????Vijana Wengine wamepoteza mpaka maisha yao kulinda amani ya wengine kwa kujitolea kwa mioyo dhabiti!!!Usiwazungumzie vibaya ndugu zangu wa JWTZ!!!!Sawa ndugu yangu
Wanasaidia nchi za Africa.
Sisi waafrika hatuwezi kusaidia wazungu? Au hawataki msaada wetu
 
Wenyewe tunataka msaada tena acha kabisa hii topic, Mwigulu akiisikia anaweza akaja fasta na toza ya kusaidi Uturuki.
 
Back
Top Bottom