COMORIENNE
JF-Expert Member
- Dec 25, 2022
- 1,157
- 1,267
Hivi mkuu ni kweli hawana kazi?Afrika ina tatizo gani, hadi sasa haijatoa msaada wowote ule, hata wa watu kwenda saidia Turkiye katika usaidizi wa kuokoa watu.
Ukraine iko vitani ila inapeleka watu
Lebanon imepeleka watu
India imepeleka watu, madawa, mbwa, vifaa
China imepeleka watu (waliojitolea)
Marekani inapeleka watu, vifaa, madawa
Urusi imepeleka watu na madawa
Afrika tuna tatizo gani?
Lile tetemeko limeshusha nyumba zaidi ya 6000 hawataweza wenyewe.
JWTZ wamekaa tu hawana kazi, kwanini serikali isiwapeleke kusaidia?
Kila kitu ni mipango nafikiri watakuwa wanatafakari namna gani ya kusaidia. Kama Nchi hatuja wahi kukaa kimya kwa matatizo yanayo kumba nchi marafiki