AFCON 2015 Qualifiers: Msumbiji vs Tanzania

AFCON 2015 Qualifiers: Msumbiji vs Tanzania

Mie mwenyewe naomba wafungwe,maana Taifa linacheza mechi kubwa kama ile nchi nzima haionyeshwi.Duhh
Tuwaachie wenyekujua.
Haya mambo ya TFF na Super sport,maana waligoma ili wapate Pesa,wenzao wakenya hadi mechi za uchochorin Supersport wanaonyesha ligi ya Kenya.Sie hapa tulimgomea DSTv Leo tumempa Azam TV,Hopeless kabisa.
Fungwa huko,mrudi huku na kauli za tumeonyesha kiwango ila bahati sio yetu,hahahaha kazi kweli
Nimedokezwa stars imeshalala 1-0 na sasa ni half time
 
Mimi nilishazoea maumivu kutoka timu yangu ya taifa, sasa tatizo sijui hawalioni? Ntaendelea kuumia hadi lini? Karibuni nyumbani.
 
Duh! Naona na Kenya kakaliwa kooni na Lesotho, yaani bado 0 - 0 ikiwa hivi kenya out. EA majanga! Labda Uganda ambayo ina mabao mawili mkononi inacheza baadaye!
 
I told u ,mambaz tunashinda hii game,wachezaji wenu wa staz wanaanguka anguka kama wamelewa.

full time Sisi 2 TZ Moja.

haya mkawapokee mashujaa wenu kesho.
 
Nchi kwanza kwani mwanao akikunyea kiganjani unakata mkono? Jibu ni hapana naipenda Tanzania nchi yangu Tanzania nyumbani kwanza
 
Bora tuache kwanza kushiriki hadi hapo tutakapokuwa vizuri ndo tushiriki.
 
Majirani zetu vipi kenya hapo na Lesotho nani anamatokeo..wakuu

Kenya bado kakaliwa kooni ngoma bado ni 0 - 0 hadi sasa dk za nyongeza

UPDATE:

mpira umekwisha Kenya OUT! Afadhali sisi yaani Lesotho nina uhakika tungewatoa kabisa!
 
Back
Top Bottom