Afande Sele: Nitapambana na Abood

Afande Sele: Nitapambana na Abood

safi sana kamanda sele, mtetezi wa wanyonge--hakuna kulala mpaka abood aachie jimbo. tuko pamoja mfalme wa rhymes. people'ssss.........
 
Msanii wa kizazi kipya, mfalme wa rymes, Selemani msindi a.k.a baba tunda, simba dume, AFANDE SELE amesema sasa yupo tayari kwaajili ya mapambano ya kweli katika kuhakikisha jimbo la morogoro linapata kile walichokikosa kwa miaka 50 sasa.

Akizungumza ofisin ya chadema kata ya msufini, mkali huyo mwenye nyimbo za kuelimisha kasema sasa watanzania twahitaji kubadilika na kuangalia mbele kwani ni muda mrefu sasa tumechoshwa na unyanyasaji wa uongozi wa ccm, tumehaidiwa mengi na bwana mkuu lkn hakuna anachokitekeleza zaidi ya kutembea nchi za watu.

Anasema taifa haliwezi kuendelea kwa kuomba misaada nchi za nje bali kwa jasho la mtanzania mwenyewe ambaye atapata elimu bora itakayo mwezesha kujiajiri mwenyewe na sio mfumo wa sasa wa elimu unao tegemea ajira kutoka serikalini. Akiongeza kua nimejiunga chadema kupambana na wasiopenda haki na demokrasia, wasiojali utu na umasikini wa mtanzania, wasiojua shida ninin hasa, wasio jua uchungu wa vifo vya wa mama wajawazito na watoto wanaokufa kwa malari kutokana na huduma duni zinazo tolewa na serikali isiyowajali watu wake kwa mda mrefu tangu serikali ya awamu ya tatu.

Anasema sasa yupo fiti kuungana na watanzania wapenda haki na wanademokrasia kuzunguka nchi nzima kuelimisha jamii kuhusu serikali hii mbovu ya ccm.Akizungumzia mgoogoro unaokikumba chama anasema ni vema mh.zitto akawa mpole na kujishusha ilikufikisha chama salama,, anaongeza kuwa haoni sababu ya malumbano yasio kuwa ya msingi hasa wakati huu ambao tunaukaribia uchaguzi wa serikali za mtaa kwahiyo ni bora zitto akapatana na mwenyekiti wake ili tutimize ndoto ya watanzania 215.

Akizungumzia nia yake yakugombea ubunge jimbo la morogoro mjini anasema watakavyoona wananchi ndivyo atakavyo fanya yeye kwani anatamani jimbo hilo lisiwe chini ya ccm 2015 tena chini ya abood.Anasema abood kageuka kuwa mfazili na sio mbunge wakupeleka matatizo ya wananchi bungeni, wananchi wa morogoro hawataki msaada wa magari ya kusafirisha maiti kwakuwa hata iwevipi maiti haiwezi kuozea ndani kisa hakuna ufadhili wa magari ya abood na nitahakikisha abood analiacha jimbo hilo kwa watu wanaojali utu wa mtanzania, aliongeza afande sele.

piiipoooozzzzzz!!!,

Hay bana...hii haki ya kuchagua na kuchaguliwa naona watu wanaitumia vibaya sana.
 
Mimi na kina nani???!!!!
Never associate me with any group with political purposes mkuu. M a one free rider! !!!!!!Fikra huru mwanzo mwisho no affiliation wala inclination!!!!!!

Kama uamuzi wangu wooote hao saa hizi wangekuwa vilio tu!!
Huna degree go do some other businesses sio kukaa kwa maslahi ya umma,ningeonekana mbaguzi sijui nini potelea mbali!!!!!!

So kawaambie na wenzio!!!!


Sasa Kama nisipokuunganisha na vyama mbona unamponda Sele?
 
Afande Sele asubiri taratibu za chama...kupitishwa kugombea kama kweli anataka kugombea kupitia Chadema....
 
Huyu naye ni MHAINI... bado mapema mno kuzungumzia hayo
 
Kila la kheri kamanda... hawa wanashangaa manjonjo ya jukwaani wanashinwa kusikitika Rais anavyotudhalilisha kwa umatonya wakati mungu katujaalia rasilimali lukuki
 
Sasa Kama nisipokuunganisha na vyama mbona unamponda Sele?

Sababu kazi anayoitaka inahitaji upeo na uwezo wa kuangalia mambo kwa jicho la tatu na hiki sio kipaji cha wote, wanatakiwa wakae shule ili kupata uwezo huo,mambo ya kujaribu yametosha sasa kwa miaka hii hamsini!!!!!!!

Tukiingiza vichwa wazalendo kule ndani hatuwezi kubaki hivi!!!!
 
Yani huyo nae anataka kuwa mbunge,chadema kweli hawajielewi ila kama ndio maamuzi yao kumweka huyo mtambo, no coment,
 
:welcome:

Abunuas;
Umefika huko? Huna hata hofu kabisa kuonyesha chuki yako hivyo? Hivi weye ulizaliwa na mwanamke au ulidondoka kama senene za kwetu? Unaonesha chuki kiasi cha kumwita mtu ka weye ati "Takataka". God forbid! Jamani, hata kama nimekuchukia kiasi gani nisikuite hivyo.
Kakosa maadili, sawa, kabuia sembe sawa, lakini bado ni mwanadamu si Takataka. Anayo familia ka weye na kama tukiendelea hivi, na hilo lichama tawala likiwa linafanya madudu haya ya kuuza sembe mpaka wabunge wake wanauza, sidhani itachukua muda kabla haijauzwa huko huko mjengoni. Si wabunge wake wanajidai kuwa ni sifa watoto wao wanauza hadharani na hakuna wa kuwafanya lolote? Biashara kutoka banaa. Wateja popoteee, hivyo si shida kuupanua ungo wamwuzie naibu. na supika yake kwani nini banaa mteja ni mteja tu. Unamwogopa Afande Sele, ngoja wamalize wateja huku hata mjengoni watapiga hodi.
Acha kutukana wanadamu ka weyee.
Huyo jamaa anyedharau wengine ni Ngatara +++
 
Ila mjue afande sele ni mfuasi wa zitto na amekiri wazwaz kuwa ni rafiki wa zitto na hata ktk press conference aliingia ukumbini na zitto

perio....
 
Baada ya Sugu kuukwaa ubunge, wasanii wengi watajitokeza wakidhani it's that simple. Kama Afande Sele atakuwa serious, then kwanza tumuombee uzima hiyo 2015 aione!. Matajiri wa mabasi kwa kupotezeana ni balaa!.
Pasco
 
Hawa akina Afande sele wakishindwa uchaguzi wa ndani lazima waasi!
Mtu hajafahamu upinzani ndani ya chama ukoje anawaza next stage.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom