Afadhali daladala kuliko UDART

yanasaidia ila kwa Morocco problem.Mimi nakuwa nyerere square kila siku SAA 2 usiku hivi.magari ya morocco machache sana.kila gari kimara kimara .mengine matupo yanaenda kupaki na abiria wsnasubiri
hawa watu hawaeleweki kabisa. kama unatoka morocco kwenda kariakoo majira ya jioni hata asubuhi ni afadhali upande daladala kuliko UDA RT maana hayatabiliki. unaweza kata tiketi na ukapata gari baada ya dk 45.
 
Sirikali popote mlipo mmesikia sasa Kazi kwenu .....
 


Duh, aliyeleta uzi huu ni MTANZANIA halisi...kulalamika, kushutumu, kupayuka ovyo, hakuna analysis, asiyeridhika, asiye na shukrani...
 
Miaka ya nyuma ile baada ya kuvunjika Jumuia ya Afrika Mashariki ikasababisha shirika EA Airways kuvunjika. Serikali haikua na budi ila kuanzisha Air Tanzania na ikaagiza ndege 3 Boeng 737 na ukweli yulikua yunaenda London , UAE na nchi zote za jirani kwa ndege zetu..
Hili shirika lilikua siku za mwanzo abiria ni wengi mno na huduma zilikua za kuridhisha.
Zilianza. Hujuma za ufisadi na wizi......Sio mara moja wala mbili kwenda makao makuu ya ATC kutaka ticket na kuambia ndege zimejaa labda 1st class...Mara moja nilikua mkutano muhimu hivyo ilibidi ni kate tu 1st class japo nafasi yangu haiku niruhusu....cha mshangao nilipo ingia ndani ya ndege nikakuta economy class zaidi ya robo 3 iko tupu !!!! Wakati makao makuu na juu ya kuwabembeleza walikataaa na kusema zimejaa...nikajua hii ni hujuma na hupati hizo ticket mpaka kwa rushwa......hatimae ATC likafa
Hivyo hujuma zipo na bado watanzania hawana uzalendo.....uzalendo wao ni wa rangi tu ya kiafrika lakini mapenzi hasa na nchi hakuna....na haya mabasi tusipo angalia yatakufa mbele ya macho yetu tunayaona...na kufa sio lazima mabasi yafe bali ni kama hivi kupita bure matupu bila kupakia..wanakosesha watu huduma na mapato kujiendesha.....Serikali isome makosa ya zamani kwenye kuendesha miradi ya umma...mentality za watu bado ni zile zile
Kazi njema
 
ni kweli unacho kisema, lakini nikicho gundua management ya UDART ndio wa sanii kwa kuto jali makubakiano waliyo fanya na madareva hasa kwenye malipo.

Mfano mdogo ni kuwa walikubaliana ninavyo sikia kulipwa elfu 10 lakini sasa hivi wanalipwa elfu 6 kama posho ta siku.

Vitu kama hivi vinaashiria kuwa mwekezaji hana nia ya dhati ya kutoa huduma nzuri ktk jiji letu pendwa.

Ujanja ujanja mwingi sana.
 
Tajiri angeenda punjab india angepata madereva wazuri tu,tena akawalipa laki 3 tu
Tatizo la wabongo hatuna nidhamu ya kazi, ukifanya kazi na wahindi utagundua ni watu wenye nidhamu ya hali ya juu kazini na ni wavumilivu.
 
Tatizo la wabongo hatuna nidhamu ya kazi, ukifanya kazi na wahindi utagundua ni watu wenye nidhamu ya hali ya juu kazini na ni wavumilivu.
waajiri nao wa kibongo wazushi sana. mnakubaliana mwisho wanakugeuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…