Afadhali daladala kuliko UDART

Kwa hiyo unafurahia vurugu za daladala? Kusimama ovyo kila sehemu bila kufuata vituo rasmi. Kwenda bila kuzingatia muda wa safari? Ama kweli wewe ni Tabutupu
tatizo lako umesoma hiyo post kama mtoto wa darada la kwanza.
 
Kwa nini ugeuze.Huo ndio ushamba ambao ni kikwazo kikubwa katika utaratibu huu mzuri
 
Kwa nini ugeuze.Huo ndio ushamba ambao ni kikwazo kikubwa katika utaratibu huu mzuri
wewe ndio mshamba, hayo magari unapanda popote na unaenda popote. kazi ya dereva ni kutaja vituo, kufungua milango na kufunga full stop. usilete mawazo ya daladala hapa
 
Changamoto niliyoiona,baadhi ya madereva hawapendi kutaja majina ya vituo ila kuna wengine wanataja.Si abiria wote wanajua majina ya vituo kwakweli.Hili waliangalie.Narudia BAADHI YA MADEREVA
Mule ndani ya mabasi niliona kunasehemu ya display anayoweza kuwaonyesha abilia kuwa wamefika kituo fulani itumike hiyo pia wanaweza kurekodi sauti yenye vituo vyote kwenye route husika na wakaseti kwa kutumia spika ndani ya basi dereva anabonyeza batani yenyewe inasema ...ulaya wanafanya hivyo ingawa wao wanatumia mifumo ya sensors zaidi....!
 
N
Ngoja tuwaangalie kwanza
 
Inachekesha sana, kila mtanzania anamuona mwenzio hana taaluma kwenye anachokifanya.
 
tatizo kubwa na kero ya haya magari ni kufika mbezi, ukishatoka mjini ukafika kimara mwisho unajuta, unaanza kuyakumbuka daladala za zamani.

kwanini hili tatizo la kimara wamekaa kimya?
 
Jamani hivi nauli za haya mabasi ni sh .ngapi maana sijawahi kupanda tangu tuanze kulipia
 
Sasa kwa nini mengine yasimame kila kituo,na mengine baadhi ya vituo kama hayajajaza abiria,huo si ndio usumbufu wenyewe? But daladala wanatafuta abiria kila mahali kwenye line yake! Nadhan wanaohusika wanatakiwa kurekebisha
 
Mimi kero niliyopata kuna dereva alitupitisha kituo ilikuwa tunashuka urafiki akatupitisha hadi shekilango. Yaani walishuka wawili tu akaondoa gari na gari lilikuwa lilimejaa sana hadi wakati wa kushuka ilikuwa ni taabu kufika mlangoni ila yeye hakuliangalia hilo alihesabu zile sekunde zake tu akafunga mlango na kutuacha tunasukumana tunataka kushuka. Kwa kweli hakutumia busara kabisa. Alinikera sana bahati yake sikushika namba ya gari ningemripoti kwa mabosi wake.
 
Sawa mkuu nimekuelewa hizo ni changamoto pia ila natumaini maoni watayasiki warekebishe hizo tatizo

 
Sasa kwa nini mengine yasimame kila kituo,na mengine baadhi ya vituo kama hayajajaza abiria,huo si ndio usumbufu wenyewe? But daladala wanatafuta abiria kila mahali kwenye line yake! Nadhan wanaohusika wanatakiwa kurekebisha
daladala kwenye customer care wapo vizuri sana.
 
Kero niliyoishuhudia ni kuhusu chenji. Kama hauna 650/# ya chenji utaganda hapo mpaka! Mi nilienda nikiwa na 10,000/# sikuwa na chenji...kila nikipanga foleni nikifikiwa mhudumu anakataa kupokea hela yangu...na siyo mimi tu...wote waliokuwa na 2,000/#, 5,000/# na 10,000/# tulikaa zaidi ya robo saaa wanakataa hela zetu.
 

Namba 3 na 5, nitawarudishia majibu mabaya tu siwezi kuvumilia mropokaji
 
yanasaidia ila kwa Morocco problem.Mimi nakuwa nyerere square kila siku SAA 2 usiku hivi.magari ya morocco machache sana.kila gari kimara kimara .mengine matupo yanaenda kupaki na abiria wsnasubiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…