Afadhali daladala kuliko UDART

Kwenye ukweli tuongee ukweli jamani, na sio kukosoa kila kitu. Mwendokasi unasaidia sana, tena sana, na tupo wengi sana tunaofurahia UDART. Kwa hili serikali wamejitahidi, na natamani kungekua na route za sehemu nyingine muhimu pia kama vile buguruni, makumbusho na kadhalika
 
ndio maana magufuli husema uwe maskini jeuri.. hapa hatuzungumzii tuu kusafiri tunazungumzia adha zinazo tokana na uzembe au kuto jari kwa mtoa huduma.

serikali imaefanya kazi yake lakini aliye kabidhiwa atoe huduma ndio ivo utadhani kila mfanyakazi ni mjomba.
 
S
Ushakurupuka kumlaumu Mtanzania. Hapa halijalalamikiwa basi, wamelalamikiwa watumishi, sasa usichoelewa nini? Kwa hiyo ulitaka tuchekecheke tu hata kama tunakaa masaa kumi vituoni na mabasi yanapita?
Sasa mradi wenyewe umeanza juzi unategemea kila kitu kiwe perfect, hizo ni changamoto ndogo ndogo ambazo ziteendelea kurekebishwa jinsi muda unavyoenda. tujifunze ku appreciate maendeleo tunayoletewa hata kama kwa baadhi ya watu wanaweza wasione kama haya ni maendeleo.
 
sio changamoto ndogo, kuna watu wamechelewa interviewa kwa sababu ya uzembe wa dereva au mtoa huduma.
 
Sijajua daladala unazoziongelea kusema zina afadhali kihuduma kuliko mwendokasi ni za kutoka wapi kwenda wapi, ila kwa nionavyo mimi kero za daladala na makondakta wake zinachosha kupita maelezo, walau mwendokasi imesaidia kuziepuka
 
Sijajua daladala unazoziongelea kusema zina afadhali kihuduma kuliko mwendokasi ni za kutoka wapi kwenda wapi, ila kwa nionavyo mimi kero za daladala na makondakta wake zinachosha kupita maelezo, walau mwendokasi imesaidia kuziepuka
daladala wanajali abiria wao na kuwapa huduma kadiri wawezavyo.

UDART wanawaina abiria kama wasumbufu, hata kuwakwepa.mara nyingine.

Ni mara ngapi madereva wamekua wanapita vituo bila kuchukua abiria wakati basi lake halina abiria wa kutosha eti anawahi kuchukua wengine.

Ina maana hao anao wapita hawana hawana haki ya kusafiri.

Na hii inatokana na kuwa madereva hawalipwi pesa , kama wale wa daladala kwa hiyo yeye kupita abiria hapotezi chochote.
 
Hoja zako hazina mashiko. Endelea na daladala zako, acha tunaoona mwendokasi unatusaidia tuendelee nao
 
Hapo kaka naona umefunua kila kitu.. Japo sijawahi kuyapanda ila napata picha ya kile kinachotokea...
 
Ni hatari sana. Pia kwa mfumo Wa kulipia kwa kadi angekuwa ameinyima mapato kampuni.
 
Hivi mawazo ya namna hii watanzania wenzangu mnayatoa wapi? Hivi kweli kwa akili ya kawaida ungependelea tubaki na daladala? instead of DART? Shame on you. Kama kuna kasoro toa mapendekezo namna ya kuzirekebisha. Its really sad kuona baadhi ya watanzania tunashindwa ku-appreciate efforts za wenzetu katika kuboresha maisha ya wananchi.

#Alwaysbepositive#
 
Tatizo lako unaisoma hii post kama mtoto wa darasa la kwanza
 
si bure..una lako wewe
 
watanzania kwa kulalamika huwawezi sasa kinachokulalamisha ni nini
labda ndio taratibu zao walizojipangia jamani tukue hata kwa kuona
 
watanzania kwa kulalamika huwawezi sasa kinachokulalamisha ni nini
labda ndio taratibu zao walizojipangia jamani tukue hata kwa kuona
nikuulize, unalipa nauli ili upewe huduma mbovu. au wamepewa leseni ya kutoa huduma mbouvu.

Mbona unajifanya mwelewa wakati unacho kiongea kinapishana na weledi wako.

Hawata kuja kukulipa kwa kuwatetea wanapo toa huduma.
 

Mradi kabla haujaanza walifanya majaribio kwanza.muda gani unaotaka tuwape wakae sawa hiyo ni hatari .kama hawajaelewa wajibu wao wasimamishe huduma wakapewe elimu upya wakiwa tayar warud tena barabarani
 
Mradi kabla haujaanza walifanya majaribio kwanza.muda gani unaotaka tuwape wakae sawa hiyo ni hatari .kama hawajaelewa wajibu wao wasimamishe huduma wakapewe elimu upya wakiwa tayar warud tena barabarani
Safi sana, mi nashangaa watu wanawatetea hawa watoa huduma wakati wanatoa huduma mbovu kabisa
 
Changamoto zipo kila siku, hata kwenye maisha binafsi changamoto haziishi. Leo ukitatua hili, kesho utakumbana na lingine. Hayo mabasi, wamiliki wa mradi pamoja na wafanyakazi ni lazima wapitie changamoto hizi ili kupata kitu kizuri.

Wenzetu huko ulaya, marekani na nchi zilizoendelea walipitia changamoto nyingi zaidi ya hizo katika kuleta maisha tofauti kwa watu wao.

Niliangalia documentary moja ya "when we left earth", vitu kama hivi ndio vimeleta dunia ya tofauti na iliyokuwa mwanzo. Wengine walipoteza maisha yao ili tu kubadilisha maisha ya wengine.

Natamani sana DART ingekuwa implemented throughout the city, hakuna usafiri mzuri kama huu. Watu wangeacha usafiri binafsi nyumbani asee.
 
Tatizo hawa ndugu zako hawataki kukosolewa. hata mhudumu wao hataki kabisa anakwambia sio wajubu wake kupeleka matatizo ya abiria. Dereva naye ndio hivo anaona abiria kama adui zake.

Ndio maana tumeamua kutafuta njia yankutatua haya matatizo. wasifanye watu tuchukie BRT kwa uzembe wao.
Mtoa huduma kama hawezi awambie DART watafute operator mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…