Adhabu za wanajeshi

Adhabu za wanajeshi

Mpaka umuone mkubwa wao labda iwe tu ni bahati yako

Kama askari tu anazinguliwa na akitaka zinapigwa na hakuna anaefukuzwa kazi(kuna mjeshi alizinguliwa na polisi,akaenda kambini akawashitua wana,wana wakavamia kituo cha polis kikapigwa),na sikusikia mtu katimliwa
Ujinga huo haupo tena mkuu.
 
Nasemaje!, usije kutana na hao watu ukaleta ujuaji, utaumia mzee baba!. Nasema utaumia sababu hakuna atakayeajibishwa kwa wajeshi wa nchi hii. Bro wangu mmoja hivi alikutana na kisanga pale makongo kipindi anasoma pale Tumaini bachelor of laws, alileta ujuaji wa sheria lkn kilichokuja kumpata hatasahau maisha yake yote.
Wale wana wanatumia neno AMRI, zingatia sana hilo neno usije jichanganya aisee...
😂😂😂
 
Sitaki kukumbuka huo ufedhuli...zaidi aliutenda rafiki yangu.
Nakumbuka siku tunarudi kambini jioni tukiwa tumepakiana kwenye pkpk XL250.

Nyuma yetu tulifuatwa na lori la mchanga na juu yake walikuwa na vijana sita wakielekea kupakia mchanga.

Mbele yetu kulikuwa na beria ya kambi yetu ambayo hufanya ukaguzi wa magari ya kiraia.

Sasa sisi tulikuwa tunaendesha mwendo wa kawaida tu lkn lori lilikuwa na fujo na speed likitaka kutupita

Kwa vile tulikaribia hiyo beria hatukuwapisha...sasa vijana juu ya gari wakaanza kuporomosha mitusi kama ujuavyo wavuta bangi.

Kwa vile tulikuwa tunaongea kwa sauti kama ujuavyo mkiwa na pikpiki mnalazimika kuongea kwa sauti hatukuweza kusikia hayo matusi lkn askari aliyekuwa getini alisikia na tulipofika getini alusema...afande mbona mnatukanwa na hawa vijana wapuuzi?

Yule rafiki yangu kusijia vile aligeuka kichaa kwa hasira...

Geti likafunguliwa ile beria na kuamuriwa wapaki pembeni...
Wote wakaamuriwa kushuka pamoja na dereva wao.

Amri ikatolewa wavue mashati na suruali.

Wakaulizwa...hawa mnaowatukana mnawafahamu? Au kwa vile wamevaa kiraia?
Jamaa yangu akaruka juu ya mti akavunja tawi...

Ghafla wote wakapokea fimbo 6 kila mmoja mgongoni.

Akawaamuru walale chini kwenye kokoto
Na waviringike...daah jamaa walitokwa damu hadi niliwaonea huruma.

Ndani ya dakika 10 hawafai kutazama.

Niliingilia kati kuzuia kuendekea kuteswa kidogo tuzipige na jamaa yangu.

Mengine...yabaki tu
Dah,Kumbe mkuu wewe ni bakabaka?

Nina kisa changu pia..

Siku moja nimetoka zangu home (enzi hizo Dar)mida ya saa moja usiku naelekea ubungo kutuma mzigo fuani nyeti uende Mkoa fulani kwa jamaa yangu mmoja enzi zile stendi Ni ubungo. Nafika pale nikawa sielewi elewi maana wapiga debe wananisumbua alafu limebaki gari moja tu linatoka nje..Lilikuwa BM,nikasema wacha nisepe nalo tu badala ya kutuma Kama parcel.

Tumefika Moro mida Kama ya saa tano usiku,nikamcheki bodaboda nikamuuliza Sasa hivi hadi kbi fulani ya jeshi Ni Bei gani? Boda akastuka,kwanza akaniangalia anaona mtu mwenyewe bwana mdogo early 20s. Akaniuliza uliza maswali nikamwambia mzee,maswali ya nini kama polisi niambie Kama unaenda au huendi. Nikampa hela, kinyonge akawasha chombo tukasepa.

Tumefika getini tumewakuta bakabaka pale wameshika mijegeja wanatukazia macho,hiyo Kama saa sita usiku Sasa. Kosa la boda boda si akapiga honi!! Bwana wee!!

Afande mmoja "Asee nyie raia mnajiamini nini kuingia maeneo haya mida hii,na mbaya zaidi mnatupigia Hadi honi?"

kilichonisaidia ni jina. Nilipotaja jina la mtu fulani kidogo wakapunguza kutuwashia Moto ila ilikuwa balaa,walishatuweka kwenye kanyampasila.

Hata hivyo bodaboda hawakumwacha bure bure kwa kitendo Cha kupiga honi kambini,tena saa sita usiku.

Jamaa watu wema ila ukijichanganya Sasa.
 
Mpaka umuone mkubwa wao labda iwe tu ni bahati yako

Kama askari tu anazinguliwa na akitaka zinapigwa na hakuna anaefukuzwa kazi(kuna mjeshi alizinguliwa na polisi,akaenda kambini akawashitua wana,wana wakavamia kituo cha polis kikapigwa),na sikusikia mtu katimliwa
Labda akuue, lakini kama hujafa, na ukakomaa na hiyo ishu ya uonevu na kuhakikisha unaifikisha mbele ya vyombo vya nidhamu za kijeshi Askari aliyekuwa Lindo siku hiyo msala anao. Labda kama jeshi limegeuka kikundi cha Kihuni, lakini kama kweli ni jeshi lenye nidhamu, huyo afande au hao maafande msala wanao, tena si mdogo!
 
Usichokijua kuhusu hawa watu wao hawakupigi ili wakuuwe na wana nidhamu ya ajabu kuhusu silaha,usitegemee akushikie bunduki hata kiwembe tu hawakushikii huwa wanachotaka wao nidhamu izingatiwe na hata uwe mkorofi vipi wewe mbele yao ni mchumba tu,na wanaweza kuwa na njaa lakini hela yako hawachukui.

Usije siku ukakutana nao ukawajibu hovyo ukitegemea watakupiga ili wakuuwe nduguzo wakafungue jalada,hao utapewa adhabu mbalimbali ukitoka hapo wiki nzima kuna vitu hutaweza kuvifanya kama ulivyozoea.

Nina jamaa yangu tulivuka maji tukaenda Kigamboni na Starlet yake ina music mkubwa kuna kambi ipo sehemu inaitwa kitu kama Longoni au Ulongoni kuna kambi ya wanajeshi sasa tukapita pale sauti ipo juu,hatukujua walipotokea walitupeleka kwenye mess yao kikaletwa kindoo litre kumi kimejaa ubwabwa jamaa wakatuzunguka wakasema nanukuu "tunakunywa bia moja moja zikiisha hamjamaliza tunaleta ya litre 20 zingine"

Wakashauri atakaeshiba apige push ups ili chakula kijisage aendelee kula,cha kushukuru jamaa walikuwa wameshalewa na jamaa yangu nae alikuwa dizain amelewa so akili za kilevi zikakutana adhabu haikuzingatiwa sana,jamaa hupenda ukiwa mtiifu wanakuacha ukijifanya much know utaiva.
Ukiwatii ndo umeumia kwa sababu utafanya adhabu ambazo siyo haki kwa mujibu wa sheria. Usiwatii kabisa ili option yao iwe ni wakupige wakuumize au wakuue, halafu waje waone kama Jeshi litawakingia kifua. Itakula kwao!.

Baadhi ya Wanajeshi hasa vijana wanaendeshwa na Mob psychology. Hizi tabia za kihuni huwezi kuzikuta kwa wanajeshi ambao ni matured!.
 
Na tuliotoa adhabu tunaruhusiwa kusimulia?
Mungu anisamehe tu
Sitaki kukumbuka huo ufedhuli...zaidi aliutenda rafiki yangu.
Nakumbuka siku tunarudi kambini jioni tukiwa tumepakiana kwenye pkpk XL250.

Nyuma yetu tulifuatwa na lori la mchanga na juu yake walikuwa na vijana sita wakielekea kupakia mchanga.

Mbele yetu kulikuwa na beria ya kambi yetu ambayo hufanya ukaguzi wa magari ya kiraia.

Sasa sisi tulikuwa tunaendesha mwendo wa kawaida tu lkn lori lilikuwa na fujo na speed likitaka kutupita

Kwa vile tulikaribia hiyo beria hatukuwapisha...sasa vijana juu ya gari wakaanza kuporomosha mitusi kama ujuavyo wavuta bangi.

Kwa vile tulikuwa tunaongea kwa sauti kama ujuavyo mkiwa na pikpiki mnalazimika kuongea kwa sauti hatukuweza kusikia hayo matusi lkn askari aliyekuwa getini alisikia na tulipofika getini alusema...afande mbona mnatukanwa na hawa vijana wapuuzi?

Yule rafiki yangu kusijia vile aligeuka kichaa kwa hasira...

Geti likafunguliwa ile beria na kuamuriwa wapaki pembeni...
Wote wakaamuriwa kushuka pamoja na dereva wao.

Amri ikatolewa wavue mashati na suruali.

Wakaulizwa...hawa mnaowatukana mnawafahamu? Au kwa vile wamevaa kiraia?
Jamaa yangu akaruka juu ya mti akavunja tawi...

Ghafla wote wakapokea fimbo 6 kila mmoja mgongoni.

Akawaamuru walale chini kwenye kokoto
Na waviringike...daah jamaa walitokwa damu hadi niliwaonea huruma.

Ndani ya dakika 10 hawafai kutazama.

Niliingilia kati kuzuia kuendekea kuteswa kidogo tuzipige na jamaa yangu.

Mengine...yabaki tu
Kumbe wewe ni soldier mkuu??? Uwiiiii jambo afande
 
Ukiwatii ndo umeumia kwa sababu utafanya adhabu ambazo siyo haki kwa mujibu wa sheria. Usiwatii kabisa ili option yao iwe ni wakupige wakuumize au wakuue, halafu waje waone kama Jeshi litawakingia kifua. Itakula kwao!.

Baadhi ya Wanajeshi hasa vijana wanaendeshwa na Mob psychology. Hizi tabia za kihuni huwezi kuzikuta kwa wanajeshi ambao ni matured!.
Hawakupi adhabu km huna kosa, uwe unaelewa
 
Mtu yeyote anayekuonea na kukufedhehesha kwa makusudi, huyo naamini unatakiwa kufa naye kabisa, hatakiwi kusamehewa pasipo kuadhibiwa.
Ndio maana wanajeshi hawapendi kuzinguliwa kwenye himaya yao eneo la Jeshi, we mtambie kote Ila usiende kumtambia kwenye himaya yake hatoangalia wewe ni raia au wewe ni nani utachangamshwa kidogo ili siku nyingine ujifunze na uwe mfano kwa wengine
 
Afande akileta upuuzi huo unamgomea tu, maana ni kinyume cha maadili ya kazi za jeshi. Hawezi kukufanya lolote. Hawezi kukuua na kama Akikudhuru unamfikisha kwa wakubwa wake tu , uone kama kibarua chake hakijaota nyasi.

Tatizo watu hawajui haki zao na wanaogopa magwanda. Lakini nidhamu za kijeshi zinakataza kabisa askari kuonea raia.
Askari wa Tanzania wengi - ingawa sio wote- hawana adabu, wanapenda kutumia uaskari wao kuonea watu.

Hizi habari zinanikumbusha mbali sana.

Kuna siku tulikuwa tumekaa maskani Upanga, muda wa jioni vijana wanakutana maskani. Mara paap, tukawa tumeaona askari kibao wanakuja kutoka mbali, wako doria kundi zaidi ya ishirini, wamebeba bunduki na marungu.

Basi nikawaambia madogo tuliokuwa tumekaa nao maskani, kama hamjiamini, ondokeni kabisa, wale wanakuja kutaka kututingisha hapa.

Basi kuna madogo wakaondoka, wengine tuliojiamini tukabaki.

Wakaja wakafika maskani, sisi kama kumi, wao zaidi ya ishirini. Mmoja akatuuliza "Haroo, mnafanya nini hapa?".

Basi hawakujua wanaongea na watu wa aina gani, jamaa mmoja wa maskani akamjibu "Afande hivyo ndivyo ulivyofundishwa kusalimia watu?". Ikabidi yule askari astuke kwanza. Alitegemea watu wataogopa, hakutegemea kujibiwa vile.

Sasa akaja askari mmoja, nafikiri ndiye alikuwa mkubwa wao yule, akaanza kuuliza watu, mmoja mmoja, "Wewe unakaa wapi?" Mtu anamwambia hapo, "Wewe unakaa wapi?" Mtu anamwambia hapo. Wakamfikia jamaa mmoja.Wakamuuliza "Wewe unakaa wapi?" Akajibu kwa Baba Ben.

Askari akauliza, "Kwa Baba Ben? Baba Ben gani?" Jamaa akajibu "Kwa Ben huyo huyo wa Jamhuri ya Muungano, kwani wewe unamjua Ben gani mwingine Tanzania?" (Hapo kipindi cha urais wa Ben Mkapa).

Yule Polisi akawa kastuka, kama hajaamini hivi, sasa kumbe kuna wenzake huwa walikuwa wanaenda kulinda kwa Mkapa, wakawa wamemjua yule kijana wa kwa Mkapa. Ikawa kama wanamwambia yule mkubwa wao kwamba huyu tunamjua anakaa kwa Mkapa, tunamuona tukienda kulinda pale.

Basi hapo hapo nikaona wale polisi wanabadilika mara moja, wanasema unajua wazee ni suala la kufahamiana tu, tulikuwa tunajuana tu, hamna tatizo, hamna tatizo tulikuwa tunatambuana tu.

Kuanzia siku hiyo mpaka kituoni kwao kile kijiwe walikiwekea alama ya X kisiguswe, wakasema hapa kuna watoto wa Mkapa huwa wanakaa.

Nikasema hapa ingekuwa wamewakuta watu wasio na majina wangewasumbua sana.
 
Mpaka umuone mkubwa wao labda iwe tu ni bahati yako

Kama askari tu anazinguliwa na akitaka zinapigwa na hakuna anaefukuzwa kazi(kuna mjeshi alizinguliwa na polisi,akaenda kambini akawashitua wana,wana wakavamia kituo cha polis kikapigwa),na sikusikia mtu katimliwa
Mambo ya Seminari hayo, ukisema uliepigwa na aliekupiga wote mnafukuzwa Seminari, kwa hio mnayamaliza chini kwa chini tofauti zenu mnaziweka sawa chini kwa chini hakuna kusemeleana hapo father asijue km ulipigwa na fulani
 
Back
Top Bottom