Adhabu za wanajeshi

Adhabu za wanajeshi

Kaka usimalize maneno... Wako watu watata na wanajua mchezo ya hatari.. Ila ukiyaingia kwa wanajeshi Kua mpole
Wana nini? Kama bunduki hata sisi tunazo Tena Kwa kibali maalum, wakimwaga mboga namwaga ugali, nitahakikisha nakufa na wawili au watatu kama hamza na hawatokaa wanisahau Kwa ushenzi ntakao wafanyia

Tatizo lenu wabongo mnaasili ya uoga wa kifala, jaribuni kuchanganya dam mzae hata na waarabu na wasomali mjaze kizazi Cha majasiri na wenye kujitoa mhanga
 
Hawa Jamaa usiombe uingie kwenye 18 zao, utajuta kuwafahamu.

Siku moja Tulikuwa kwenye foleni ya kuelekea mjini, kuna jamaa wa Lori akaziba geti la kuingilia pale kambi ya Abdallah Twalipo uhasibu. MP akamfuata kistaarabu kabisa "mambo vipi Kaka?" Jamaa akaitikia "Safi kabisa afande". Afande akamuuliza hapa uliposimama si unajua Kama ni getini? Mwamba kwa kujiamini kabisa akaitikia ndiyo afande ila tatizo foleni haitembei, Sina jinsi, samahani sana.

Kama kawaida ya wanajeshi kujifanya wastaarabu kwenye matukio ya aina hii. Afande akamwambia sasa ndugu kwa kuwa foleni haiendi shuka tu hapa upumzike tupige stori, foleni ikitembea utaendelea na safari yako. Dereva wa Lori kwa mbwembwe akafungua mlango ashuke eti apumzike na wanajeshi. Hapo ndiyo 'ntiti' ulipoanza!!

MP akamwambia "kaka sijasema ushuke mlangoni, shukia dirishani" lilikuwa ni tukio la kuchekesha Sana kwa sisi wapita njia ila kwa lililomtokea lilikuwa ni tukio mbaya na la kufedhehesha.

Picha linaanza,gari anayoendesha jamaa ni Scania R 420,Chuma mpya kabisa ya Transit alafu imepanda hewani Kama farasi, imebeba mafuta inaelekea nje. Gari ikisimama dereva unamwona yule kuleee ghorofani. Sasa vuta picha dereva ameambiwa ashuke kupitia dirisha badala ya mlangoni. Sisi wengine wa pembeni Tulicheka Sana maana jamaa kwanza ni bonge alafu ili ashuke kwa kutumia dirisha inabidi ajikusanye awe Kama fungu la nyanya Kisha ndiyo atoe miguu nje. Ilimchukua karibia dakika 15 kushuka. Wakati huo MP alikuwa siriazi hacheki wala haongei. Yeye anamsubiri jamaa tu ashuke wapige stori. Dereva akadondoka chini Kama mzigo wa viazi mbatata vya Mbeya..Tiii!!

Suruali yote imechanika kwenye maungio ya miguu. Aliposhuka huku kijasho kinamtoka mjeda akaanza kupiga nae stori Kama hakuna kilichotokea "naona chuma imeshakunywa wese inasepa?" Dereva kinyonge akajibu yeah inaelekea Ndola, Zambia. Wakapiga stori Mara foleni ikafunguka magari yakaanza kutembea. Afande akamwambia dereva Sasa unaweza kwenda tu maana gari zinatembea. Dereva akatoa shukrani Kisha akaelekea kwenye gari yake asepe.

Cha ajabu wakati dereva anafungua mlango Mjeda akamwambia mzee baba si tulikubaliana tunapitia dirishani? Ahahahhaha kazi ya kupanda dirishani ikaanza tena. Nina uhakika Yule dereva alimtukana mjeda matusi yote ya hapa duniani ila kimoyomoyo.. Ile siku yule dereva hataisahau kamwe maishani.

Unakumbuka kisa chochote Cha wanajeshi na adhabu zao kwa raia pindi raia akijichanganya kwenye anga zao?

Jambo la ajabu Sana
 
Afande akileta upuuzi huo unamgomea tu, maana ni kinyume cha maadili ya kazi za jeshi. Hawezi kukufanya lolote. Hawezi kukuua na kama Akikudhuru unamfikisha kwa wakubwa wake tu , uone kama kibarua chake hakijaota nyasi.

Tatizo watu hawajui haki zao na wanaogopa magwanda. Lakini nidhamu za kijeshi zinakataza kabisa askari kuonea raia.

Aisee kabisa tena mambo mengine ya ajabu

Kuna siku pale machava niliona Mzee anarushwa kichura et kisa ametema mate eneo la jeshi
 
Watu Kama wewe ndiyo mnakuwaga wapole Kama mmemwagiwa maji mkiwaona bakabaka. Ila kwa background mnaandika kishujaa Kama hivi.

Keyboard warrior.
Mimi Nina damu ya kiarabu, Nasemeje Kuna haja ya wabongo kuzaa na waarabu na wasomali tupate wapambanaji walio tayari kujitoa muhanga kwaajili ya kutetea haki, wabongo mnaasili ya kauoga, Mimi sipo hivo, Mimi Nina dam ya kiarabu nipo Razi kuvaa bomu nikafe na washenzi buku kuokoa taifa
 
Afande akileta upuuzi huo unamgomea tu, maana ni kinyume cha maadili ya kazi za jeshi. Hawezi kukufanya lolote. Hawezi kukuua na kama Akikudhuru unamfikisha kwa wakubwa wake tu , uone kama kibarua chake hakijaota nyasi.

Tatizo watu hawajui haki zao na wanaogopa magwanda. Lakini nidhamu za kijeshi zinakataza kabisa askari kuonea raia.
Sahihi.
 
Mimi sikubaligi upumbavu, huyo mwanajeshi mshamba na njaa Kali angekuja kwangu aone, ningevomjibu dry sitishiwi bunduki Mimi, Wala sitishiwi kifo hata siku moja

Angeenda ailete hata Kambi nzima, siogopagi kufa Mimi, liwalo na liwe na ndo wangejua kweli hii Dunia kuna watu watata, sio Dunia, Tanzania kuna watu watata. Mimi ndio MWAMBA.
Kijana utajaa tu siku moja ndio utajua wajenda ni vichaa zaidi yako. Utanyooshwa na jamaa ukimshtaki afukuzwi kazi
 
Tena wewe ndiyo utakuja kuumizwa kabisa ukileta ujinga huo. Kule kuna watu wameshindikana na zaidibya wahuni, ukitaka ukae nao wale kwa amani punguza ujuaji
Muache mjuaji huyo akojaa18 atakubali mziki.
 
Unachokifanya ni kushangilia ujinga wa kutokujua haki zako, Askari wa jeshi lolote haruhusiwi kukushambulia hata kama umevunja sheria ilimradi tu hujakataa kutii amri ikiwa amekuja kukukamata haruhusiwi kukupiga Wala kukudhalilisha kwa adhabu yoyote chombo kinachotoa adhabu ni mahakama anachotakiwa kukifanya ni kukufikisha mbele ya vyombo vya sheria ili ukahukumiwe kwa kosa ulilofanya kama kweli hilo kosa lipo

Akikwambia chuchumaa/kaa chini we kubali ila akikwambia ruka kichura mwambie siwezi kwasababu za kiafya hapo sasa chochote atakacho kufanya ikiwa ni kukushambulia unaruhusiwa kumshitaki utaratibu wa kushtaki ni uleule
Shambulizi lolote atakalo kufanyia ni kosa kama makosa mengine ya shambulio na unaruhusiwa kufungua kesi dhidi yake na akawajibishwa

Huyo dereva alitakiwa akatae kwanzia amri ya kuambiwa ashukie dirishani kwakua siyo amri halali na ni kinyume na utaratibu kwakua ilikua inahatarisha usalama wake
Nasemaje!, usije kutana na hao watu ukaleta ujuaji, utaumia mzee baba!. Nasema utaumia sababu hakuna atakayeajibishwa kwa wajeshi wa nchi hii. Bro wangu mmoja hivi alikutana na kisanga pale makongo kipindi anasoma pale Tumaini bachelor of laws, alileta ujuaji wa sheria lkn kilichokuja kumpata hatasahau maisha yake yote.
Wale wana wanatumia neno AMRI, zingatia sana hilo neno usije jichanganya aisee...
 
Acha uoga ww jambo lakwanza ww kamata ile number yake kwisha habari yake akikuamrisha chochote kilicho na element ya udhalilishaji usifanye.
 
Dogo acha ujinga we na huyo bro wako wazazi walipoteza ada wakapeleka ng'ombe shuleni unatoa mfano wa bro wakati mimi binafsi nimeshawaonya hao wanajeshi kufanya vitendo ambavyo viko kinyume na maadili ya jeshi na kuvunja sheria? Hivi unajua kosa lolote la jinai ikiwepo kumshambulia mtu ni kosa la kufukuzwa kazi kwenye majeshi ya ulinzi?

Sasa kawatishe wajinga wenzako mtaani usituletee utoto hapa
 
Acha uoga ww jambo lakwanza ww kamata ile number yake kwisha habari yake akikuamrisha chochote kilicho na element ya udhalilishaji usifanye.
Rejea hiyo story yangu kisha mengine jiongeze. Huyo bro wangu alifanya kila ujanja, kilichomtokea hakisimuliki ww.
Jamaa baada ya kwenda kwa viongozi kaongezewa adhabu nyingine.
Haya mambo tuyaache tu
 
Dogo acha ujinga we na huyo bro wako wazazi walipoteza ada wakapeleka ng'ombe shuleni unatoa mfano wa bro wakati mimi binafsi nimeshawaonya hao wanajeshi kufanya vitendo ambavyo viko kinyume na maadili ya jeshi na kuvunja sheria? Hivi unajua kosa lolote la jinai ikiwepo kumshambulia mtu ni kosa la kufukuzwa kazi kwenye majeshi ya ulinzi?

Sasa kawatishe wajinga wenzako mtaani usituletee utoto hapa
Sina cha kukujibu kaka mkubwa maana naona tutadhalilishana tu
 
Kwenye pitapita zangu nikaingia kwenye eneo la Jeshi kukata majani ya kulisha ng'ombe. Mbele yangu kulikuwa na maembe dodo yanatamanisha sana. Sasa mimi sikujua kama ni eneo la jeshi.

Nikaenda chini ya embe dodo nikaanza kuyapopoa maembe.

Muda kidogo naona pale nilipoacha mkokoteni wa kubebea majani kuna mtu amekaa na magwanda, huku anazuga anaongea na simu.

Oya, siisahau ile siku.
tanga nini hii
 
Rejea hiyo story yangu kisha mengine jiongeze. Huyo bro wangu alifanya kila ujanja, kilichomtokea hakisimuliki ww.
Jamaa baada ya kwenda kwa viongozi kaongezewa adhabu nyingine.
Haya mambo tuyaache tu
Hakuna mtu ambaye Yuko juu ya Sheria. Panda mbele mahakamani kafungue kesi,
 
Rejea hiyo story yangu kisha mengine jiongeze. Huyo bro wangu alifanya kila ujanja, kilichomtokea hakisimuliki ww.
Jamaa baada ya kwenda kwa viongozi kaongezewa adhabu nyingine.
Haya mambo tuyaache tu
Alitakiwa apande juu zaidi baada ya aliekwenda kumshatakia kutomsikiliza lao lilikuwa moja

kuna rafiki yangu aligongewa bajaji yake nagari yao ya jeshi kosa lilikuwa la mjeda na driver bajaji aliogopa kwahizo amri zao. Driver akampigia bosi wake ambae ndo rafiki yangu wakati mm nipo nikamwambia fukuzia na boda chukua hiyo plate number.

Unafikiria tuliangaika sana waliitengeneza hiyo bajaji kwahela zao zamfukoni baada yakujua walipo.

Hayo mambo yalikuwa zamani kuhalalisha kosa lao kuwa haki kwao.
 
Ukiwa ndezi,ndo utazidi kuumia zaidi
Jaribu uende kuleta ujuaji wako, utasimulia hadi wajukuu kitakachokupata. Wanajeshi epuka sana akiwa yupo eneo la kazi na hapo ulimkuta alipangiwa jukumu fulani, kazi ikiharibika anaadhibiwa na kuliko litokee hilo ndiyo anakuzingua. Kama huyo wa lori aliyekutana na MP, wale kituo chao cha kazi ni hapo getini kama angekutwa na wakubwa geti limezibwa hivyo angezinguliwa na ndiyo hapo aliamua kumzingua yeye.

Cheza na mwanajeshi sehemu zingine zote ila si eneo lake la kazi, wanaadhibiwa adhabu mbaya sana wale jamaa au kutukanwa kabisa na wakubwa kama mambo yakienda hovyo
 
Back
Top Bottom