Adhabu za wanajeshi

Adhabu za wanajeshi

Hawa Jamaa usiombe uingie kwenye 18 zao, utajuta kuwafahamu.

Siku moja Tulikuwa kwenye foleni ya kuelekea mjini, kuna jamaa wa Lori akaziba geti la kuingilia pale kambi ya Abdallah Twalipo uhasibu. MP akamfuata kistaarabu kabisa "mambo vipi Kaka?" Jamaa akaitikia "Safi kabisa afande". Afande akamuuliza hapa uliposimama si unajua Kama ni getini? Mwamba kwa kujiamini kabisa akaitikia ndiyo afande ila tatizo foleni haitembei, Sina jinsi, samahani sana.

Kama kawaida ya wanajeshi kujifanya wastaarabu kwenye matukio ya aina hii. Afande akamwambia sasa ndugu kwa kuwa foleni haiendi shuka tu hapa upumzike tupige stori, foleni ikitembea utaendelea na safari yako. Dereva wa Lori kwa mbwembwe akafungua mlango ashuke eti apumzike na wanajeshi. Hapo ndiyo 'ntiti' ulipoanza!!

MP akamwambia "kaka sijasema ushuke mlangoni, shukia dirishani" lilikuwa ni tukio la kuchekesha Sana kwa sisi wapita njia ila kwa lililomtokea lilikuwa ni tukio mbaya na la kufedhehesha.

Picha linaanza,gari anayoendesha jamaa ni Scania R 420,Chuma mpya kabisa ya Transit alafu imepanda hewani Kama farasi, imebeba mafuta inaelekea nje. Gari ikisimama dereva unamwona yule kuleee ghorofani. Sasa vuta picha dereva ameambiwa ashuke kupitia dirisha badala ya mlangoni. Sisi wengine wa pembeni Tulicheka Sana maana jamaa kwanza ni bonge alafu ili ashuke kwa kutumia dirisha inabidi ajikusanye awe Kama fungu la nyanya Kisha ndiyo atoe miguu nje. Ilimchukua karibia dakika 15 kushuka. Wakati huo MP alikuwa siriazi hacheki wala haongei. Yeye anamsubiri jamaa tu ashuke wapige stori. Dereva akadondoka chini Kama mzigo wa viazi mbatata vya Mbeya..Tiii!!

Suruali yote imechanika kwenye maungio ya miguu. Aliposhuka huku kijasho kinamtoka mjeda akaanza kupiga nae stori Kama hakuna kilichotokea "naona chuma imeshakunywa wese inasepa?" Dereva kinyonge akajibu yeah inaelekea Ndola, Zambia. Wakapiga stori Mara foleni ikafunguka magari yakaanza kutembea. Afande akamwambia dereva Sasa unaweza kwenda tu maana gari zinatembea. Dereva akatoa shukrani Kisha akaelekea kwenye gari yake asepe.

Cha ajabu wakati dereva anafungua mlango Mjeda akamwambia mzee baba si tulikubaliana tunapitia dirishani? Ahahahhaha kazi ya kupanda dirishani ikaanza tena. Nina uhakika Yule dereva alimtukana mjeda matusi yote ya hapa duniani ila kimoyomoyo.. Ile siku yule dereva hataisahau kamwe maishani.

Unakumbuka kisa chochote Cha wanajeshi na adhabu zao kwa raia pindi raia akijichanganya kwenye anga zao?
Ni ujinga wa majeshi ya Afrika tu. Duniani huko tunaona wanajeshi hawafanyi ujinga huo bali wanakuwa ni msaada sana kwa raia.

Kama huyo gari wangejuwa tatizo li[pi mpaka limefunga geti lao, kama limeharibika wangemsaidia, wangeleta mpaka breakdown zao na mafundi wao kumpa msaada.

Jeshi lipo kwa usalama wa wananchi siyo kwa kutesa wananchi.

Ni ujinga tu waufanyao.
 
Nakazia
 
Wabongo ni washanba tu,nakumbuka mwaka mmoja maeneo ya Kawe Ukwamani nilikuwa stendi ya daladala ndani ya basi la UDA.Kwa mbele naona wanajeshi wanafanya mazoezi ya kutembea na mizigo mgongoni...nikachukua simu yangu nyeupe blackberry nikaanza kuchukua video,nipo siti ya mbele pembeni ya dereva.

Jamaa wakaniona,wanajeshi wawili wakaja upande wangu...kabla hawajanishusha nilianza mimi kushuka kuwafuata,dereva akanimbia watakupiga...nikamwambia tulia wewe.

Pale chini mzozo ukaanza lete simu,kwanini unapiga picha na maswali mengi.Hadi muda huu hakuna aliyenigusa...niliwapa jibu moja tu kwamba nimepiga picha kwasabu nalipenda Jeshi langu.Mmoja akapaza sauti toa memory card,mwingine akmwambia achana naye.

Narudi kwenye basi,abiria hawaamini...wakasema mimi ni mwenzao lakini wapi nikujiamini tu na kujitambua.

Confidence beats all.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Samtaimz tunawaogopa kupita kiasi hadi wao wanafikia hatua ya kujiona ni untouchable.
 
Mimi sikubaligi upumbavu, huyo mwanajeshi mshamba na njaa Kali angekuja kwangu aone, ningevomjibu dry sitishiwi bunduki Mimi, Wala sitishiwi kifo hata siku moja

Angeenda ailete hata Kambi nzima, siogopagi kufa Mimi, liwalo na liwe na ndo wangejua kweli hii Dunia kuna watu watata, sio Dunia, Tanzania kuna watu watata. Mimi ndio MWAMBA.
Umekaa na kademu kako geto ,Basi unajiona shujaa kujibu hivi .

Njoo mbeya 44 gharama za nauli kuja na kurudi nitalipa ili uone Kama sitakutundika bakora .
 
Naona mnajifagilia siku hizi hatuwashobokei ni wa kawaida sana,,,migwanda tu mpaka mashoga wapo jeshini cku hz,,,vijana wengi wengi saizi unfit jeshi limekuwa ajira kama ajira nyingine
Ukweli mchungu, watoto wa wakubwa wanaharibu chombo , kama upinde wapo pia
 
Back
Top Bottom