Adhabu za wanajeshi

Adhabu za wanajeshi

Hawa Jamaa usiombe uingie kwenye 18 zao,utajuta kuwafahamu.

Siku moja Tulikuwa kwenye foleni ya kuelekea mjini,kuna jamaa wa Lori akaziba geti la kuingilia pale kambi ya Abdallah Twalipo uhasibu. MP akamfuata kistaarabu kabisa "mambo vipi Kaka?" Jamaa akaitikia "Safi kabisa afande". Afande akamuuliza hapa uliposimama si unajua Kama ni getini? Mwamba kwa kujiamini kabisa akaitikia ndiyo afande ila tatizo foleni haitembei,Sina jinsi, samahani sana.

Kama kawaida ya wanajeshi kujifanya wastaarabu kwenye matukio ya aina hii. Afande akamwambia sasa ndugu kwa kuwa foleni haiendi shuka tu hapa upumzike tupige stori,foleni ikitembea utaendelea na safari yako. Dereva wa Lori kwa mbwembwe akafungua mlango ashuke eti apumzike na wanajeshi. Hapo ndiyo 'ntiti' ulipoanza!!

MP akamwambia "kaka sijasema ushuke mlangoni,shukia dirishani" lilikuwa ni tukio la kuchekesha Sana kwa sisi wapita njia ila kwa lililomtokea lilikuwa ni tukio mbaya na la kufedhehesha.

Picha linaanza,gari anayoendesha jamaa ni Scania R 420,Chuma mpya kabisa ya Transit alafu imepanda hewani Kama farasi,imebeba mafuta inaelekea nje. Gari ikisimama dereva unamwona yule kuleee ghorofani. Sasa vuta picha dereva ameambiwa ashuke kupitia dirisha badala ya mlangoni. Sisi wengine wa pembeni Tulicheka Sana maana jamaa kwanza ni bonge alafu ili ashuke kwa kutumia dirisha inabidi ajikusanye awe Kama fungu la nyanya Kisha ndiyo atoe miguu nje. Ilimchukua karibia dakika 15 kushuka. Wakati huo MP alikuwa siriazi hacheki wala haongei. Yeye anamsubiri jamaa tu ashuke wapige stori. Dereva akadondoka chini Kama mzigo wa viazi mbatata vya Mbeya..Tiii!!

Suruali yote imechanika kwenye maungio ya miguu. Aliposhuka huku kijasho kinamtoka mjeda akaanza kupiga nae stori Kama hakuna kilichotokea "naona chuma imeshakunywa wese inasepa?" Dereva kinyonge akajibu yeah inaelekea Ndola,Zambia. Wakapiga stori Mara foleni ikafunguka magari yakaanza kutembea. Afande akamwambia dereva Sasa unaweza kwenda tu maana gari zinatembea. Dereva akatoa shukrani Kisha akaelekea kwenye gari yake asepe.

Cha ajabu wakati dereva anafungua mlango Mjeda akamwambia mzee baba si tulikubaliana tunapitia dirishani? Ahahahhaha kazi ya kupanda dirishani ikaanza tena,Nina uhakika Yule dereva alimtukana mjeda matusi yote ya hapa duniani ila kimoyomoyo.. Ile siku yule dereva hataisahau kamwe maishani.

Unakumbuka kisa chochote Cha wanajeshi na adhabu zao kwa raia pindi raia akijichanganya kwenye anga zao?
Humo ndani ya kambi nahisi kulikuwa na mzito yupo ndani, na muda wowote alitakiwa kutoka. Kama kungekutwa geti limezibwa vile angezinguliwa vibaya na hata kutukanwa. Kuliko aje kuzinguliwa lazima akuzingue wewe
 
Tena wewe ndiyo utakuja kuumizwa kabisa ukileta ujinga huo. Kule kuna watu wameshindikana na zaidibya wahuni, ukitaka ukae nao wale kwa amani punguza ujuaji
Hakuna kitu hapo, watz acheni uoga wa kijinga, ndo maana mnaonewaga kifala kisa ya uoga, mwanajeshi ni binadam kama binadam mwingine tuu, akijilengesha kwenye 18 unaweza kumua na akafa kama wanavokufa binadam wengine
 
Sasa hivi sifa ni pesa sio upot, aje na upot wake aje na mwenye pesa zake hata Dem, alaf tuwafungulie mbwa wakali tuone ni nani atakaeng'atwa

yani hapo lazma pot ang'atwe na upot Wake maana hana pesa.
Unachoshupalia ni nini hapa?kwani huyo dereva hakutenda kosa?ushaambiwa ukitenda kosa kwenye eneo lao ww unakazania huwaogopi cha kufanya kakojoe pale kambini kwao utuletee mrejesho
 
Hakuna kitu watz acheni uoga wa kijinga, ndo maana mnaonewaga kifala kisa ya uoga, mwanajeshi ni binadam kama binadam mwingine tuu, akijilengesha kwenye 18 unaweza kumua na akafa kama wanavokufa binadam wengine
Wewe upo hapo nyuma ya keyboard unajiona ni jasiri sana, sasa mimi nakwambia nishawahi kukaa nao jamaa kwenye mafunzo huko walikuja watu watata sana na watukutu kupitiliza ila baadaye walikuwa wapole. Hao jamaa waone hivyohivyo na magwanda yao kama mabishoo ila wameshindikana. Kama unataka amani na kutetea haki yako kuwa mpole na upeleke malalamiko baadaye kwa wakubwa zao atashughulikiwa hata kupoteza kazi. Sasa wewe jitie una ujasiri wa waandamanaji wa UKAWA, utakuja kusimulia
 
Mimi nimesoma shule ya jeshi pale jitegemee jkt mgulani.
1. kuna siku moja kuna captain × alinichapa bakora nne kisa ninamzidi urefu! Yani alikuwa anafundisha nikamwambia sir naomba ruhusa niende chooni! Yani hapo hapo akabadilika kabisa, ety kwann unanizidi urefu alafu mimi nina nyota tatu???

Mzee zilitembea bakora, kuanzia siku hiyo nilikuwa namshangaaa sana yule afande.

02.Tukio la pili ni siku ya kwanza kwenda pale shuleni! Ilikuwa form five!
Aisee kwanza nilienda shule saa mbili ahsubui, nikamkuta MP anaitwa MSENGI. Akaniweka bakora nne, huwezi amini day one.

Nikaanza kwenda mdogomdogo, kuna sehemu wanaita smart area hurusiwi kutembea yani unatakiwa kupita nduki.. sikuwa najua.
Alooo alikuwa afande mmoja anaitwa kiyarunzi ni coplo hapo hapo nilikula bakora sita.

Aisee nikaanza kuona hii shule sio machozi yananilenga, huyo mdogomdogo mpaka class.
Kufika class namkuta captain shemahonge anafundisha kwa machungu nikagonga mlango mfululizo akasema unatutukana akampigia afande dani akaja mbio na bakora nne.akamwambka huyo kaja hapa anatukana

Mpige sjta....huwezi amini nikasema nikitoka humu ndani sirudi tena.. nikala sita kila mtu ananishangaaa nalio kisa mboko sita.

Nikaingia class nakakutana na wana nikawaadisia msanga.basi saa nne ikafika tukaenda canteen.

Sasa mwisho wa kuingia canteen na kutoka ni saa nne na nusu.
Mimi nilikuwa nakunywa supu mpaka saa nne na 40 aloooooh

Nilipigwa bakora za mgongo nikamwaga supu mbio nikasema huu ni usenge..nkasepa class
Nashukuru Mungu sikifuata.

Siku ya kwanza nilipigwa zaidi ya bakora 16
Hahaha umenikumbusha kuhusu JITE UTE.

Mie nimepiga pale 6 years yaan O and A levels.

Kuna kale kazee kanajiita NDYAMKAMA yule mzee alijaa ktk 18 zetu tulimla mitama sana nje ya ukuta. Kimbembe wiki iliyofuata. Tulikoma.

Hahah kuhusu canteen aisee nilikuw nakimbizana na wale Service na private flan hivi muda umeisha wa kula ila unakimbia na bakur la supu (SUPU ya kioo) huku na kule..

Smart Area pale.. aiseee uwanja wa DAMU palee kuna siku Kondakta alijichanganya wauni wakashuka nae wakamuingiza ndani mule. Kilichomtokea nahisi alibadiri ruti ya daladala kesho yake.
 
Mimi nimesoma shule ya jeshi pale jitegemee jkt mgulani.
1. kuna siku moja kuna captain × alinichapa bakora nne kisa ninamzidi urefu! Yani alikuwa anafundisha nikamwambia sir naomba ruhusa niende chooni! Yani hapo hapo akabadilika kabisa, ety kwann unanizidi urefu alafu mimi nina nyota tatu???

Mzee zilitembea bakora, kuanzia siku hiyo nilikuwa namshangaaa sana yule afande.

02.Tukio la pili ni siku ya kwanza kwenda pale shuleni! Ilikuwa form five!
Aisee kwanza nilienda shule saa mbili ahsubui, nikamkuta MP anaitwa MSENGI. Akaniweka bakora nne, huwezi amini day one.

Nikaanza kwenda mdogomdogo, kuna sehemu wanaita smart area hurusiwi kutembea yani unatakiwa kupita nduki.. sikuwa najua.
Alooo alikuwa afande mmoja anaitwa kiyarunzi ni coplo hapo hapo nilikula bakora sita.

Aisee nikaanza kuona hii shule sio machozi yananilenga, huyo mdogomdogo mpaka class.
Kufika class namkuta captain shemahonge anafundisha kwa machungu nikagonga mlango mfululizo akasema unatutukana akampigia afande dani akaja mbio na bakora nne.akamwambka huyo kaja hapa anatukana

Mpige sjta....huwezi amini nikasema nikitoka humu ndani sirudi tena.. nikala sita kila mtu ananishangaaa nalio kisa mboko sita.

Nikaingia class nakakutana na wana nikawaadisia msanga.basi saa nne ikafika tukaenda canteen.

Sasa mwisho wa kuingia canteen na kutoka ni saa nne na nusu.
Mimi nilikuwa nakunywa supu mpaka saa nne na 40 aloooooh

Nilipigwa bakora za mgongo nikamwaga supu mbio nikasema huu ni usenge..nkasepa class
Nashukuru Mungu sikifuata.

Siku ya kwanza nilipigwa zaidi ya bakora 16
Ukiacha hilo la huyo Kapteni kukuonea hayo galiyobaki yote ni makosa na ilikuwa ni sahihi kabisa kutandikaa. Jitegemee kabla ya hujaanza kusoma na hata sare hamjapewa unasomewa sheria zote za shule, wewe inaonekana ulikwepa siku za mwanzo kuijua shule
 
Mimi sikubaligi upumbavu, huyo mwanajeshi mshamba na njaa Kali angekuja kwangu aone, ningevomjibu dry sitishiwi bunduki Mimi, Wala sitishiwi kifo hata siku moja

Angeenda ailete hata Kambi nzima, siogopagi kufa Mimi, liwalo na liwe na ndo wangejua kweli hii Dunia kuna watu watata, sio Dunia, Tanzania kuna watu watata. Mimi ndio MWAMBA.
Watu Kama wewe ndiyo mnakuwaga wapole Kama mmemwagiwa maji mkiwaona bakabaka. Ila kwa background mnaandika kishujaa Kama hivi.

Keyboard warrior.
 
Hawa jamaa ni shida Kuna siku jamaa yangu alijichanganya huko kambini akapewa adhabu ya kuhamidha tofali 500 kuxitoa upande mmoja ma kuxipeleka upande mwingine akapambana na kuweza kuhamisha tofali 350 huku jasho likiwa limemtoka gafla akaonana na ndugu yake ambae ni mjeda na ana cheo kikubwa akamwelezea kosa na adhabu aliyopatiwa akawa anamuomba msaada huyo mjeda akasema nitakusaidia usijali hebu rudisha hizo tofali ilipozitoa nafikiri tatizo litakuwa limeisha! Da jamaa aliishiwa pozi
20211219_202239.jpg
 
Nakumbuka 2009 nikiwa ndani ya kigoma, nilipewa adhabu ya kujaza pipa kwa kijiko...

Ntaludi kumalizia but usiombe ujae angle za hao jamaa.
Dodoma makutupora iyo 2010 raia kapewa kisoda ajaze ndoo ya lita 20 maji umbali wa kama hatua 30 ivi kutoka bombani adi ndoo ilikowekwa.. Kwa kosa la kuzurura eneo la jeshi
 
We bado mshamba!! Siku hizi mwanajeshi Hana maajabu yoyote akijichanganya anapigwa tu
Uliza mtoni mtongani walivofunga mitaa kwa kosa la mwana jeshi kukabwa na kuuwawa relini... Usijidanganye kupiga mwana jeshi.. Labda uwe hukai mitaa hiyo
 
Zaman nikiwa na miaka 16 tulienda kutafuta magoli ya miti, kwakua kambi za jeshi huwa kuna mapori fulan tukaenda kukata huko.

Wakati tumemaliza kukata yale magoli tunarudi tukakutana na mjeshi mmoja amevaa sare zao ila sio hizi za kijeshi nahisi atakua na cheo yule jamaa.

Akatuuliza mnatoka wapi? Tukasema tumekuja kuchukua magoli tukacheze mpira,, pale tulipokutana nae kulikua na kibao kimeandikwa "eneo hili ni Mali ya JWTZ, ni marufuku kukata miti, kuchunga mifugo na kupita eneo hili kuanzia sa 12 jioni".

Yule mjeshi akaanza kutuliza maswali tukawa tunajibu fresh tu,akasema tusome kile kibao kwa sauti tukasoma mmoja mmoja kisha akaanza kuuliza swali mmoja mmoja, akaanza na mimi ulivokuja ulikiona hiki kibao? Nikajibu ndio nilikiona huku najitetea tusamehe, akasema kumbe ulikiona na ukakaidi haya ww kaa chini hapa .

Wale wenzangu walivoona nimeambiwa vile kwamba "'kumbe uliona kibao hiki na ukakaidi"walipoanza kuulizwa wao lile swali ulikona hiki kibao kila mtu akawa anajibu sikuona kibao kisha anaambiwa kaa upande huu, upande mwingine tofauti na mimi.

Yule mjeshi akasema kwakua ww umesema ulikiona hiki kibao nenda ila nyie wengine laleni chini huku anavunja yale magoli. Yale magoli ndo ilikua fimbo za kuwachapia, aisee walipigwa !! Nilikua nasikia tu sauti za mwangwi zinajirudia watu wanalia balaa. Unajua ukiwa porini ukiita kwa sauti huwa sauti kama inajirudia vile ndo ilivokuwa walipigwa vibaya sana na kuanzia siku hiyo mpaka nakuwa sikuwahi kukanyaga eneo lile.

Story ya pili nikiwa secondary, shule yetu ilikua barabarani sana, sasa siku hiyo saa 5 tumetoka kuna jamaa alikua anapita kavaa tshirt ya kijeshi akakutana pale shuleni na mwanajeshi akasimamishwa.

Yule jamaa kwanz akavuliwa ile tshirt alafu akambiwa aogelee kwenye yale madimbwi ya maji machafu barabarani yaani apige mbizi pale!! Jamaa akatii akaanza kugalagala pale kwenye maji machafu alafu asukutue yale maji akatii.

Baadae akaambiwa atangulie mbele waende jeshini akawa anamambiwa kimbia kisha anambiwa chuchumaa huku yule mjeshi anakuja mdogo mdogo sijui hata walifika wapi.

Ila kiukweli hatupaswi kufurahia huu upumbavu na uonevu, kwasasa siwezi kubali kuonewa kipuuzi hivo.

Kuna siku nipo soko fulan hapa dar mwanajeshi mmoja akaja na gari binafs akapaki gari vibaya mbele ya duka, yule jamaa wa dukan hakujua kama ni mwanajeshi maana alikua kavaa suruali ya jeshi na tshirt ya kawaida kwahyo alivokuwa ndani ya gari hauwezi jua kama ni mwanajeshi mpaka ashuke.

Yule jamaa wa dukan alimwambia tu vizuri oya usipaki hapo unaziba njia yule mwanajeshi akashuka kwa hasira kutoka kwenye gari. toka dukani jamaa akatoka dukan akamuomba msamaha baada ya kugundua ni mwanajeshi.

Sasa nikajiuliza mbona hamna kosa hapa la kuomba msamaha! na ukiangalia kweli kapaki vibaya pale.
 
Mimi sikubaligi upumbavu, huyo mwanajeshi mshamba na njaa Kali angekuja kwangu aone, ningevomjibu dry sitishiwi bunduki Mimi, Wala sitishiwi kifo hata siku moja

Angeenda ailete hata Kambi nzima, siogopagi kufa Mimi, liwalo na liwe na ndo wangejua kweli hii Dunia kuna watu watata, sio Dunia, Tanzania kuna watu watata. Mimi ndio MWAMBA.
Kaka usimalize maneno... Wako watu watata na wanajua mchezo ya hatari.. Ila ukiyaingia kwa wanajeshi Kua mpole
 
Hawa jamaa ni shida Kuna siku jamaa yangu alijichanganya huko kambini akapewa adhabu ya kuhamidha tofali 500 kuxitoa upande mmoja ma kuxipeleka upande mwingine akapambana na kuweza kuhamisha tofali 350 huku jasho likiwa limemtoka gafla akaonana na ndugu yake ambae ni mjeda na ana cheo kikubwa akamwelezea kosa na adhabu aliyopatiwa akawa anamuomba msaada huyo mjeda akasema nitakusaidia usijali hebu rudisha hizo tofali ilipozitoa nafikiri tatizo litakuwa limeisha! Da jamaa aliishiwa pozi
 
We bado mshamba!! Siku hizi mwanajeshi Hana maajabu yoyote akijichanganya anapigwa tu
Wajuaji Wenzio walipita eneo la jeshi pale Lugalo mida ya saa 12 jioni kigiza kimeshaanza kuingia,na Sheria ya like eneo halifuhusiwi watembea kwa miguu kukatiza mida mibovu(enzi hizo sijui siku hizi utaratibu upoje). Walikuwa wanapiga kigoma Cha Uruguay wakitokea kawe wanakatiza Lugalo wanaelekea kule juu makongo.

Walipofika mitaa ya Lugalo wakakutana na Askari wakaulizwa mnaenda wapi saa hizi,wakajibu makongo kwenye shughuli. Afande akawaambia sasa mnaonaje mngetuburudisha kidogo kabla hamjaondoka? Jamaa kwa sifa wakaona hakuna shida,kigoma kikapigwa.

Kigoma kikapigwa Hadi usiku,jamaa walipojisikia njaa wakapewa na msosi, wajomba wakawaambi endeleeni kutoa burudani. Wazee walipiga ngoma mpaka asubuhi hadi wakaanza kulia. Kesho take ndiyo waliachiwa wakiwa mikono imevimba kwa kupiga ngoma.

Ungekuwepo katika hili kundi ungezichapa?
 
Mimi Nina msimamo sitishiwi nyau, ukishaanza kigugumizi ndo wanakuchukulia poa, mwanaume ongea straight Kwa kujiamini na kunguruma kama simba, ikiwezekana unawatandika na maswali mpaka waone hii kichwa sio nyenzetu hii Wala sio ya kuchezea. Kudadeki mbona na salute wangenipigia.
Watu kama ww ndo waoga balaa ila mkiwa mna type sasa mbwembwe nyingi, miaka ya nyuma walifunga mtaa wetu wote kisa mabomba yaliibiwa jeshini unafikiri mtaa mzima ni wajinga kutii kutotoka?

aisee usiombe ww mbona yalipatikana mabomba siku hiyo hiyo.
 
Mpaka umuone mkubwa wao labda iwe tu ni bahati yako

Kama askari tu anazinguliwa na akitaka zinapigwa na hakuna anaefukuzwa kazi(kuna mjeshi alizinguliwa na polisi,akaenda kambini akawashitua wana,wana wakavamia kituo cha polis kikapigwa),na sikusikia mtu katimliwa
Ilitokea wapi hii brother?
 
Hawa Jamaa usiombe uingie kwenye 18 zao,utajuta kuwafahamu.

Siku moja Tulikuwa kwenye foleni ya kuelekea mjini,kuna jamaa wa Lori akaziba geti la kuingilia pale kambi ya Abdallah Twalipo uhasibu. MP akamfuata kistaarabu kabisa "mambo vipi Kaka?" Jamaa akaitikia "Safi kabisa afande". Afande akamuuliza hapa uliposimama si unajua Kama ni getini? Mwamba kwa kujiamini kabisa akaitikia ndiyo afande ila tatizo foleni haitembei,Sina jinsi, samahani sana.

Kama kawaida ya wanajeshi kujifanya wastaarabu kwenye matukio ya aina hii. Afande akamwambia sasa ndugu kwa kuwa foleni haiendi shuka tu hapa upumzike tupige stori,foleni ikitembea utaendelea na safari yako. Dereva wa Lori kwa mbwembwe akafungua mlango ashuke eti apumzike na wanajeshi. Hapo ndiyo 'ntiti' ulipoanza!!

MP akamwambia "kaka sijasema ushuke mlangoni,shukia dirishani" lilikuwa ni tukio la kuchekesha Sana kwa sisi wapita njia ila kwa lililomtokea lilikuwa ni tukio mbaya na la kufedhehesha.

Picha linaanza,gari anayoendesha jamaa ni Scania R 420,Chuma mpya kabisa ya Transit alafu imepanda hewani Kama farasi,imebeba mafuta inaelekea nje. Gari ikisimama dereva unamwona yule kuleee ghorofani. Sasa vuta picha dereva ameambiwa ashuke kupitia dirisha badala ya mlangoni. Sisi wengine wa pembeni Tulicheka Sana maana jamaa kwanza ni bonge alafu ili ashuke kwa kutumia dirisha inabidi ajikusanye awe Kama fungu la nyanya Kisha ndiyo atoe miguu nje. Ilimchukua karibia dakika 15 kushuka. Wakati huo MP alikuwa siriazi hacheki wala haongei. Yeye anamsubiri jamaa tu ashuke wapige stori. Dereva akadondoka chini Kama mzigo wa viazi mbatata vya Mbeya..Tiii!!

Suruali yote imechanika kwenye maungio ya miguu. Aliposhuka huku kijasho kinamtoka mjeda akaanza kupiga nae stori Kama hakuna kilichotokea "naona chuma imeshakunywa wese inasepa?" Dereva kinyonge akajibu yeah inaelekea Ndola,Zambia. Wakapiga stori Mara foleni ikafunguka magari yakaanza kutembea. Afande akamwambia dereva Sasa unaweza kwenda tu maana gari zinatembea. Dereva akatoa shukrani Kisha akaelekea kwenye gari yake asepe.

Cha ajabu wakati dereva anafungua mlango Mjeda akamwambia mzee baba si tulikubaliana tunapitia dirishani? Ahahahhaha kazi ya kupanda dirishani ikaanza tena,Nina uhakika Yule dereva alimtukana mjeda matusi yote ya hapa duniani ila kimoyomoyo.. Ile siku yule dereva hataisahau kamwe maishani.

Unakumbuka kisa chochote Cha wanajeshi na adhabu zao kwa raia pindi raia akijichanganya kwenye anga zao?
Jamaa wana adhabu kali
But kuna mkuu XXX aliteuliwaga kwenda ule mkoa wa Kigoma na back ground yake alikuwa na cheo kikubwa tu huko baka baka.

Sasa kuna sehemu ziwani huko watu walikuwa wanalima nyanya na walikuwa hawaruhusiwi basi mheshimiwa akaenda na vijana wake wakaenda kufyeka nyanya zote ziwani.

Wazee walokuwa wanalima zile nyanya walikuwa wanaomba ziachwe ili wavune hivyo hvyo japo hazijakomaa waliambulia virungu na kuondoka lakini walitoa kauli moja tu kuwa tunaenda kukuroga jamaa kutokana na kujiamini na ile morali ya baka baka akawa anajibu mbovu wazee wakaondoka zao.

Baada ya week jamaa alipata mimba kila siku mimba inazidi kuwa kubwa kufika miezi 3 ikabidi wampeleke hosptal,wakamkuta kweli ana ujauzito kutokana na unyeti wa jambo alihamishwa mkoa kimya kimya na issue ilizimwa kimya kimya jpo watu wa mkoa huo baadhi wanakumbuka hilo.

So hapo kwa upande wangu ni kila mmoja asimame kwenye upande wake raia asimamie sehemu yake kama raia,na askari asimame kama mlinda raia na mipaka yake kama kiapo chake kinavyomtaka,ila kuendelea kuwasifia humu kwa wanavyofanya kinyume na sheria muwakumbushe pia kuna upande wa pili kwani si kila raia utamfanyia hilo atakubali.

Wengine utamfanyia hilo ataenda kukufanyia ya kukufanyia ukapoteza hata maisha huku ukiiacha familia yako ikiteseka kwa pension yako ya milioni 10 utayoiacha kutokana na mshahara wako wa laki 4
 
Wewe upo hapo nyuma ya keyboard unajiona ni jasiri sana, sasa mimi nakwambia nishawahi kukaa nao jamaa kwenye mafunzo huko walikuja watu watata sana na watukutu kupitiliza ila baadaye walikuwa wapole. Hao jamaa waone hivyohivyo na magwanda yao kama mabishoo ila wameshindikana. Kama unataka amani na kutetea haki yako kuwa mpole na upeleke malalamiko baadaye kwa wakubwa zao atashughulikiwa hata kupoteza kazi. Sasa wewe jitie una ujasiri wa waandamanaji wa UKAWA, utakuja kusimulia
Anajifanya chizi😀
 
Watu kama ww ndo waoga balaa ila mkiwa mna type sasa mbwembwe nyingi, miaka ya nyuma walifunga mtaa wetu wote kisa mabomba yaliibiwa jeshini unafikiri mtaa mzima ni wajinga kutii kutotoka?

aisee usiombe ww mbona yalipatikana mabomba siku hiyo hiyo.
A Wapi mi sionewagi kipumbavu eti kisa mwanajeshi kwenye haki mi ni mkali Zaid ya Simba lazma haki itendeke
 
Back
Top Bottom