Adhabu za wanajeshi

Adhabu za wanajeshi

Dogo acha ujinga we na huyo bro wako wazazi walipoteza ada wakapeleka ng'ombe shuleni unatoa mfano wa bro wakati mimi binafsi nimeshawaonya hao wanajeshi kufanya vitendo ambavyo viko kinyume na maadili ya jeshi na kuvunja sheria? Hivi unajua kosa lolote la jinai ikiwepo kumshambulia mtu ni kosa la kufukuzwa kazi kwenye majeshi ya ulinzi?

Sasa kawatishe wajinga wenzako mtaani usituletee utoto hapa
Kumbe inawezekana kuwashtaki kunawale wa kututishia tidhia kutukosesha amani dawa Yao n ipi😀
 
Kwenye pitapita zangu nikaingia kwenye eneo la Jeshi kukata majani ya kulisha ng'ombe. Mbele yangu kulikuwa na maembe dodo yanatamanisha sana. Sasa mimi sikujua kama ni eneo la jeshi.

Nikaenda chini ya embe dodo nikaanza kuyapopoa maembe.

Muda kidogo naona pale nilipoacha mkokoteni wa kubebea majani kuna mtu amekaa na magwanda, huku anazuga anaongea na simu.

Oya, siisahau ile siku.
Jina lako la kibabe halafu wewe mwenyewe ni mdebwedo
 
Mpaka umuone mkubwa wao labda iwe tu ni bahati yako

Kama askari tu anazinguliwa na akitaka zinapigwa na hakuna anaefukuzwa kazi(kuna mjeshi alizinguliwa na polisi,akaenda kambini akawashitua wana,wana wakavamia kituo cha polis kikapigwa),na sikusikia mtu katimliwa
Sio kwa miaka hii ndugu!!!mwanajeshi hayupo juu ya sheria,na sana sana wanaofanya upuuzi huo ni wale wadogo wadogo ki vyeo!!kuanzia nyota moja hawafanyi upuuzi huo.
 
Aroo wewe B coy nanga wa kombania okota hiyo ming'ao nikukute nayo uwanja wa damu
 
Mimi nimesoma shule ya jeshi pale jitegemee jkt mgulani.
1. kuna siku moja kuna captain × alinichapa bakora nne kisa ninamzidi urefu! Yani alikuwa anafundisha nikamwambia sir naomba ruhusa niende chooni! Yani hapo hapo akabadilika kabisa, ety kwann unanizidi urefu alafu mimi nina nyota tatu???

Mzee zilitembea bakora, kuanzia siku hiyo nilikuwa namshangaaa sana yule afande.

02.Tukio la pili ni siku ya kwanza kwenda pale shuleni! Ilikuwa form five!
Aisee kwanza nilienda shule saa mbili ahsubui, nikamkuta MP anaitwa MSENGI. Akaniweka bakora nne, huwezi amini day one.

Nikaanza kwenda mdogomdogo, kuna sehemu wanaita smart area hurusiwi kutembea yani unatakiwa kupita nduki.. sikuwa najua.
Alooo alikuwa afande mmoja anaitwa kiyarunzi ni coplo hapo hapo nilikula bakora sita.

Aisee nikaanza kuona hii shule sio machozi yananilenga, huyo mdogomdogo mpaka class.
Kufika class namkuta captain shemahonge anafundisha kwa machungu nikagonga mlango mfululizo akasema unatutukana akampigia afande dani akaja mbio na bakora nne.akamwambka huyo kaja hapa anatukana

Mpige sjta....huwezi amini nikasema nikitoka humu ndani sirudi tena.. nikala sita kila mtu ananishangaaa nalio kisa mboko sita.

Nikaingia class nakakutana na wana nikawaadisia msanga.basi saa nne ikafika tukaenda canteen.

Sasa mwisho wa kuingia canteen na kutoka ni saa nne na nusu.
Mimi nilikuwa nakunywa supu mpaka saa nne na 40 aloooooh

Nilipigwa bakora za mgongo nikamwaga supu mbio nikasema huu ni usenge..nkasepa class
Nashukuru Mungu sikifuata.

Siku ya kwanza nilipigwa zaidi ya bakora 16
Wewe ni kilaza na ndo maana ulipigwa. Wewe ni kilaza,ulizaliwa kilaza na utaendelea kuwa kilaza
 
Mpaka umuone mkubwa wao labda iwe tu ni bahati yako

Kama askari tu anazinguliwa na akitaka zinapigwa na hakuna anaefukuzwa kazi(kuna mjeshi alizinguliwa na polisi,akaenda kambini akawashitua wana,wana wakavamia kituo cha polis kikapigwa),na sikusikia mtu katimliwa
Unachukulia mambo kienyeji mno... una processor ndogo mno ya ubongo
 
Kumbe inawezekana kuwashtaki kunawale wa kututishia tidhia kutukosesha amani dawa Yao n ipi
Huyo anakuingiza mkenge mdogo wangu.

Utarukishwa kichura chura,maezi mzima utakuwa huwezi kuchuchumaa. Unaweza kujisaidia huku umelala.
 
Wewe upo hapo nyuma ya keyboard unajiona ni jasiri sana, sasa mimi nakwambia nishawahi kukaa nao jamaa kwenye mafunzo huko walikuja watu watata sana na watukutu kupitiliza ila baadaye walikuwa wapole. Hao jamaa waone hivyohivyo na magwanda yao kama mabishoo ila wameshindikana. Kama unataka amani na kutetea haki yako kuwa mpole na upeleke malalamiko baadaye kwa wakubwa zao atashughulikiwa hata kupoteza kazi. Sasa wewe jitie una ujasiri wa waandamanaji wa UKAWA, utakuja kusimulia
Kijana nyoronyoro unatoa ushauri nyoronyoro
 
Wajuaji Wenzio walipita eneo la jeshi pale Lugalo mida ya saa 12 jioni kigiza kimeshaanza kuingia,na Sheria ya like eneo halifuhusiwi watembea kwa miguu kukatiza mida mibovu(enzi hizo sijui siku hizi utaratibu upoje). Walikuwa wanapiga kigoma Cha Uruguay wakitokea kawe wanakatiza Lugalo wanaelekea kule juu makongo.

Walipofika mitaa ya Lugalo wakakutana na Askari wakaulizwa mnaenda wapi saa hizi,wakajibu makongo kwenye shughuli. Afande akawaambia sasa mnaonaje mngetuburudisha kidogo kabla hamjaondoka? Jamaa kwa sifa wakaona hakuna shida,kigoma kikapigwa.

Kigoma kikapigwa Hadi usiku,jamaa walipojisikia njaa wakapewa na msosi, wajomba wakawaambi endeleeni kutoa burudani. Wazee walipiga ngoma mpaka asubuhi hadi wakaanza kulia. Kesho take ndiyo waliachiwa wakiwa mikono imevimba kwa kupiga ngoma.

Ungekuwepo katika hili kundi ungezichapa?
Unapokosa, uungwana ni kukiri na kuwa mpole, kisha kuomba radhi. Ukisamehewa shukuru, usiposamehewa shukuru. Hao walikosea! Hivyo walistahili.
 
Hawa Jamaa usiombe uingie kwenye 18 zao, utajuta kuwafahamu.

Siku moja Tulikuwa kwenye foleni ya kuelekea mjini, kuna jamaa wa Lori akaziba geti la kuingilia pale kambi ya Abdallah Twalipo uhasibu. MP akamfuata kistaarabu kabisa "mambo vipi Kaka?" Jamaa akaitikia "Safi kabisa afande". Afande akamuuliza hapa uliposimama si unajua Kama ni getini? Mwamba kwa kujiamini kabisa akaitikia ndiyo afande ila tatizo foleni haitembei, Sina jinsi, samahani sana.

Kama kawaida ya wanajeshi kujifanya wastaarabu kwenye matukio ya aina hii. Afande akamwambia sasa ndugu kwa kuwa foleni haiendi shuka tu hapa upumzike tupige stori, foleni ikitembea utaendelea na safari yako. Dereva wa Lori kwa mbwembwe akafungua mlango ashuke eti apumzike na wanajeshi. Hapo ndiyo 'ntiti' ulipoanza!!

MP akamwambia "kaka sijasema ushuke mlangoni, shukia dirishani" lilikuwa ni tukio la kuchekesha Sana kwa sisi wapita njia ila kwa lililomtokea lilikuwa ni tukio mbaya na la kufedhehesha.

Picha linaanza,gari anayoendesha jamaa ni Scania R 420,Chuma mpya kabisa ya Transit alafu imepanda hewani Kama farasi, imebeba mafuta inaelekea nje. Gari ikisimama dereva unamwona yule kuleee ghorofani. Sasa vuta picha dereva ameambiwa ashuke kupitia dirisha badala ya mlangoni. Sisi wengine wa pembeni Tulicheka Sana maana jamaa kwanza ni bonge alafu ili ashuke kwa kutumia dirisha inabidi ajikusanye awe Kama fungu la nyanya Kisha ndiyo atoe miguu nje. Ilimchukua karibia dakika 15 kushuka. Wakati huo MP alikuwa siriazi hacheki wala haongei. Yeye anamsubiri jamaa tu ashuke wapige stori. Dereva akadondoka chini Kama mzigo wa viazi mbatata vya Mbeya..Tiii!!

Suruali yote imechanika kwenye maungio ya miguu. Aliposhuka huku kijasho kinamtoka mjeda akaanza kupiga nae stori Kama hakuna kilichotokea "naona chuma imeshakunywa wese inasepa?" Dereva kinyonge akajibu yeah inaelekea Ndola, Zambia. Wakapiga stori Mara foleni ikafunguka magari yakaanza kutembea. Afande akamwambia dereva Sasa unaweza kwenda tu maana gari zinatembea. Dereva akatoa shukrani Kisha akaelekea kwenye gari yake asepe.

Cha ajabu wakati dereva anafungua mlango Mjeda akamwambia mzee baba si tulikubaliana tunapitia dirishani? Ahahahhaha kazi ya kupanda dirishani ikaanza tena. Nina uhakika Yule dereva alimtukana mjeda matusi yote ya hapa duniani ila kimoyomoyo.. Ile siku yule dereva hataisahau kamwe maishani.

Unakumbuka kisa chochote Cha wanajeshi na adhabu zao kwa raia pindi raia akijichanganya kwenye anga zao?
Na tuliotoa adhabu tunaruhusiwa kusimulia?
Mungu anisamehe tu
 
Mimi Huwa napita lugalo mara nyingi nikitembea sijawahi kupewa adhabu sana huniuliza naenda wapi Hadi maafande wamekuwa rafiki acheni uoga wa wajeda
Hiyo ninayokwambia ni miaka ya 90 ambapo wajeda waliogopeka zaidi ya yule malaika mtoa roho za watu.

Kwa sasa mambo hayo yamepungua baada ya wajeda wenyewe kutambua kwamba kwa sasa raia wengi wana uelewa mkubwa, wanajua sheria na haki zao. Lakini pia kuna hili swala la mjeda kumfanyia ushenzi raia afu kesho mjeda huyo anaanikwa katika mitandao fulan ya kijamii na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kupitia sheria zao za jeshi.

Yani kwa sasa ukiona mtu anahenyeshwa na mwanajeshi kizembe zembe basi jua kwamba huyo jamaa ndo kwanza anaingia mjini siku kadhaa zilizopita.
 
Jamaa wana adhabu kali
But kuna mkuu XXX aliteuliwaga kwenda ule mkoa wa Kigoma na back ground yake alikuwa na cheo kikubwa tu huko baka baka.

Sasa kuna sehemu ziwani huko watu walikuwa wanalima nyanya na walikuwa hawaruhusiwi basi mheshimiwa akaenda na vijana wake wakaenda kufyeka nyanya zote ziwani.

Wazee walokuwa wanalima zile nyanya walikuwa wanaomba ziachwe ili wavune hivyo hvyo japo hazijakomaa waliambulia virungu na kuondoka lakini walitoa kauli moja tu kuwa tunaenda kukuroga jamaa kutokana na kujiamini na ile morali ya baka baka akawa anajibu mbovu wazee wakaondoka zao.

Baada ya week jamaa alipata mimba kila siku mimba inazidi kuwa kubwa kufika miezi 3 ikabidi wampeleke hosptal,wakamkuta kweli ana ujauzito kutokana na unyeti wa jambo alihamishwa mkoa kimya kimya na issue ilizimwa kimya kimya jpo watu wa mkoa huo baadhi wanakumbuka hilo.

So hapo kwa upande wangu ni kila mmoja asimame kwenye upande wake raia asimamie sehemu yake kama raia,na askari asimame kama mlinda raia na mipaka yake kama kiapo chake kinavyomtaka,ila kuendelea kuwasifia humu kwa wanavyofanya kinyume na sheria muwakumbushe pia kuna upande wa pili kwani si kila raia utamfanyia hilo atakubali.

Wengine utamfanyia hilo ataenda kukufanyia ya kukufanyia ukapoteza hata maisha huku ukiiacha familia yako ikiteseka kwa pension yako ya milioni 10 utayoiacha kutokana na mshahara wako wa laki 4
Ni ushamba sana... upo sawa
 
Hawa Jamaa usiombe uingie kwenye 18 zao, utajuta kuwafahamu.

Siku moja Tulikuwa kwenye foleni ya kuelekea mjini, kuna jamaa wa Lori akaziba geti la kuingilia pale kambi ya Abdallah Twalipo uhasibu. MP akamfuata kistaarabu kabisa "mambo vipi Kaka?" Jamaa akaitikia "Safi kabisa afande". Afande akamuuliza hapa uliposimama si unajua Kama ni getini? Mwamba kwa kujiamini kabisa akaitikia ndiyo afande ila tatizo foleni haitembei, Sina jinsi, samahani sana.

Kama kawaida ya wanajeshi kujifanya wastaarabu kwenye matukio ya aina hii. Afande akamwambia sasa ndugu kwa kuwa foleni haiendi shuka tu hapa upumzike tupige stori, foleni ikitembea utaendelea na safari yako. Dereva wa Lori kwa mbwembwe akafungua mlango ashuke eti apumzike na wanajeshi. Hapo ndiyo 'ntiti' ulipoanza!!

MP akamwambia "kaka sijasema ushuke mlangoni, shukia dirishani" lilikuwa ni tukio la kuchekesha Sana kwa sisi wapita njia ila kwa lililomtokea lilikuwa ni tukio mbaya na la kufedhehesha.

Picha linaanza,gari anayoendesha jamaa ni Scania R 420,Chuma mpya kabisa ya Transit alafu imepanda hewani Kama farasi, imebeba mafuta inaelekea nje. Gari ikisimama dereva unamwona yule kuleee ghorofani. Sasa vuta picha dereva ameambiwa ashuke kupitia dirisha badala ya mlangoni. Sisi wengine wa pembeni Tulicheka Sana maana jamaa kwanza ni bonge alafu ili ashuke kwa kutumia dirisha inabidi ajikusanye awe Kama fungu la nyanya Kisha ndiyo atoe miguu nje. Ilimchukua karibia dakika 15 kushuka. Wakati huo MP alikuwa siriazi hacheki wala haongei. Yeye anamsubiri jamaa tu ashuke wapige stori. Dereva akadondoka chini Kama mzigo wa viazi mbatata vya Mbeya..Tiii!!

Suruali yote imechanika kwenye maungio ya miguu. Aliposhuka huku kijasho kinamtoka mjeda akaanza kupiga nae stori Kama hakuna kilichotokea "naona chuma imeshakunywa wese inasepa?" Dereva kinyonge akajibu yeah inaelekea Ndola, Zambia. Wakapiga stori Mara foleni ikafunguka magari yakaanza kutembea. Afande akamwambia dereva Sasa unaweza kwenda tu maana gari zinatembea. Dereva akatoa shukrani Kisha akaelekea kwenye gari yake asepe.

Cha ajabu wakati dereva anafungua mlango Mjeda akamwambia mzee baba si tulikubaliana tunapitia dirishani? Ahahahhaha kazi ya kupanda dirishani ikaanza tena. Nina uhakika Yule dereva alimtukana mjeda matusi yote ya hapa duniani ila kimoyomoyo.. Ile siku yule dereva hataisahau kamwe maishani.

Unakumbuka kisa chochote Cha wanajeshi na adhabu zao kwa raia pindi raia akijichanganya kwenye anga zao?
Watu wa Tanzania bara mnaogopa majeshi kupitiliza yni dah punguzeni uoga hao ni maafisa tu wa jeshi
 
Back
Top Bottom