Kuna mjeda mmoja pale maeneo ya Mwenge alimpush muuza machungwa na gari lake,sasa badala awe mpole si akataka kuleta utemi bhana,sasa alikuwa kavaa kiraia,si akaanza kufoka foka pale watu wote wanaogopa,kuna jamaa akaja akaanza kubishana nae,bahati mbaya yule mjeshi akamkunja yule jamaa,basi jamaa akampiga teke yule mjeda akaanguka chini,watu wakaamulizia,cha kushangaza yule mjeda kesho yake kaja na wenzake watano wanamtafuta jamaa wampige,yule mwamba wiki nzima hakutokea yale maeneo.ushauri wangu kama wewe ni mjeda na umeleta ukorofi mtaani ukachapika maliza mwenyewe,sio unapigwa na mtu mmoja alafu wewe unaenda kuleta kikosi kwa ajili ya kumpiga mtu mmoja.
Sent from my SM-A305F using
JamiiForums mobile app