Adhabu gani inamfaa mwanamke huyu?

Adhabu gani inamfaa mwanamke huyu?

Hakuna kitu kinatesa kama mtu akukosee lakini usilalamike wala kuonyesha chuki.
Onyesha kuwa hujaumia na uko sawa.
Muonyeshe upendo lkn kidogokidogo anza kujiondoa katika maisha yake.

Hii kitu itamuumiza hakuna mfano.
Naunga mkono hoja
 
Kubaliana naye kama anavyotaka akaolewe wewe endelea kujipakulia kama mwanzoni ilivyokuwa
 
..📢..Tangazo kwa WANAUME wote 📢..Nawaomba leo jioni mfike kwenye kikao naona sheria mmeanza kuzisahau na wachache ndio watatuaibisha. Hivyo basi mfike bila kukosa ili tukumbshane 📢📢..
Na anae somesha mchumba kesho atakuja😂🤣🤣
 
Ulianza mahusiano naye akiwa tayari ana mimba ya mwezi mmoja,wakati huo wewe hukujua lolote kuhusu mimba,miezi mitatu baadaye mtu wake anakuja kugundua kwamba Demu wake ana anachepuka nawewe,anambwaga yeye pamoja na mimba yake.

Demu anakusimulia kila kitu anakuomba pesa ili akachomoe mimba kwa madai kwamba hana uwezo kujihudumia yeye akiwa na mimba pamoja na mtoto atakayezaliwa,Unamshauri asitoe
mimba utamsaidia kila kitu,demu anakubali na kushukuru sana, Baada ya kukubali nawewe unachomeka haja ya moyo wako, unamwambia bibie "mtoto akishafikisha miaka mitatu itabidi nikuoe, Demu anakubali na kuendelea kushukuru.

Mtoto anazaliwa sura kama ya baba yake, baada ya kutimiza miaka mitatu unamwambia bibie," Mtoto keshatimiza umri ambao tulishakubaliana kuoana inabidi nije kwenu nijitambulishe rasmi tuanze maisha ya ndoa, Anakujibu "Samahani najua nitakukwaza sana suala la kuoana haliwezekani kwasasa, baada baba yake mtoto kugundua mtoto ni wake alikuja tukamaliza tofauti zetu, na tumekubaliana kuoana mwakani, kilichonifanya nikubali kurudiana naye ni kitu kimoja tu sipendi kuzaa watoto kwa baba tofauti,nilikubali kuoelwa na wewe kwasababu sikuwa na namna nyingine.

Ukweli ni kwamba nakupenda sana na nathamini sana msaada wako,nakushukuru sana kwa moyo wako wa upendo please usiniache,sipo tayari kuachana nawewe hata nikiolewa, bila wewe pengine ningeshakufa nikitoa mimba hata nisingekufa lakini huyu mtoto asingekuwepo, Sina cha kukulipa zaidi ya kukuombea kwa Mungu.

Ni ndefu sana nisikuchoshe, Utafanya nini?
Mkuu achana nae Mungu ndio atakulipa hata usiwe na mahusiano nae potezea
 
Ningemshukuru sana kwa kunifungua akili Mpumbavu Mimi.

Maana mpaka niamue kumtunzia mimba, kisha nisubiri Mtoto afike miaka mitatu kwa lengo la kumwoa itakuwa akili nimezifukia shimoni.
 
Ningemshukuru sana kwa kunifungua akili Mpumbavu Mimi.

Maana mpaka niamue kumtunzia mimba, kisha nisubiri Mtoto afike miaka mitatu kwa lengo la kumwoa itakuwa akili nimezifukia shimoni.
Duuu
 
Kwa bahati mbaya sana mwanamke yuko sahihi na wewe hauko sahihi Sasa ni uchague TU kama utakubaliana na alichosema au utaachana nae ili uanze maisha mapya ila samahani kusema you are very soft aisee hapo ulipaswa kuwa kama mtu anayepiga TU no commitment Sasa we unaweka na commitment kabisa kwa mke wa mtu
 
Kwa bahati mbaya sana mwanamke yuko sahihi na wewe hauko sahihi Sasa ni uchague TU kama utakubaliana na alichosema au utaachana nae ili uanze maisha mapya ila samahani kusema you are very soft aisee hapo ulipaswa kuwa kama mtu anayepiga TU no commitment Sasa we unaweka na commitment kabisa kwa mke wa mtu
Alikuwa mke wa mtu kivipi?
 
Back
Top Bottom