Adhabu gani inamfaa mwanamke huyu?

Adhabu gani inamfaa mwanamke huyu?

Haya mambo yapo, kuna x wangu mmoja alikua mpuuzi sana.
Kina jamaa walichumbiana anamuhudumia akanitafuta after 3 yrs turudiane.
Uwongo mwingi sana tukaanza kuishi wote.
Mara mimba puh.
Katoe hataki mi hata mpango wa familia sina.
Huku na kule jamaa akapata habari tukafumaniwa.
Alivyo mpuuzi eti kaandika hadi tar katia mimba.
Nikamuachia mkewe na mtoto.
Wakaendelea na life lao.
Badae sana jamaa kagundua mtoto sio wake.
Kanirudishia na mwanamke mwenyewe.
Nikafukuzilia mbali.
Mpk leo sijawaona tena.
Atakua mtoto anakaribia 30 sasa.
Duuu hiyo roho mbaya sasa mkuu,mpaka mwanao huna mpango naye! Au sijaelewa?
 
Mwambie fresh.. ila nitaendelea kupiga hata ukiolewa na huyo jamaa yako. halaf endelea kupiga
 
watu kama hao ndio huwa wanatufanya watu tuwe na roho mbaya sana....ila do not trust any one...ishike hiyo
 
Ulianza mahusiano naye akiwa tayari ana mimba ya mwezi mmoja,wakati huo wewe hukujua lolote kuhusu mimba,miezi mitatu baadaye mtu wake anakuja kugundua kwamba Demu wake ana anachepuka nawewe,anambwaga yeye pamoja na mimba yake.

Demu anakusimulia kila kitu anakuomba pesa ili akachomoe mimba kwa madai kwamba hana uwezo kujihudumia yeye akiwa na mimba pamoja na mtoto atakayezaliwa,Unamshauri asitoe mimba utamsaidia kila kitu,demu anakubali na kushukuru sana, Baada ya kukubali nawewe unachomeka haja ya moyo wako, unamwambia bibie "mtoto akishafikisha miaka mitatu itabidi nikuoe, Demu anakubali na kuendelea kushukuru.

Mtoto anazaliwa sura kama ya baba yake, baada ya kutimiza miaka mitatu unamwambia bibie," Mtoto keshatimiza umri ambao tulishakubaliana kuoana inabidi nije kwenu nijitambulishe rasmi tuanze maisha ya ndoa, Anakujibu "Samahani najua nitakukwaza sana suala la kuoana haliwezekani kwasasa, baada baba yake mtoto kugundua mtoto ni wake alikuja tukamaliza tofauti zetu, na tumekubaliana kuoana mwakani, kilichonifanya nikubali kurudiana naye ni kitu kimoja tu sipendi kuzaa watoto kwa baba tofauti,nilikubali kuoelwa na wewe kwasababu sikuwa na namna nyingine.

Ukweli ni kwamba nakupenda sana na nathamini sana msaada wako,nakushukuru sana kwa moyo wako wa upendo please usiniache,sipo tayari kuachana nawewe hata nikiolewa, bila wewe pengine ningeshakufa nikitoa mimba hata nisingekufa lakini huyu mtoto asingekuwepo, Sina cha kukulipa zaidi ya kukuombea kwa Mungu.

Ni ndefu sana nisikuchoshe, Utafanya nini?
Hakuna adhabu kubwa ambayo unaweza kumpa mwanamke pale anapokukosea na akawa anajua fika kama amefanya makosa na wewe kama mwanaume ukakaa kimya asijue unafikiria nini,,,hii ni adhabu kubwa sana kwao maana atahangaika muda wote kujua unachofikiria na kama una msimamo hawezi kamwe kujua na hiyo ndo itakuwa adhabu tosha kwake(amani kwake itatoweka)
 
Kuna Jamaa alikuwa anafanya kazi ya ulinzi,mkewe alikuwa na mazoea ya kuingiza mahawara mumewe akiwa kazini,siku ya siku akawafumania,Jamaa hakusema lolote wala kumgusa mgoni wake,Mkewe na mgoniwe wakaanza kuishi maisha ya hofu wakidhani kwamba Jamaa anataka kuwafanya kitu kibaya, haiwezekani awafumanie halafu asichukue hatua yoyote ,basi wakashauriana na hawara yake wamuwahi jamaa kabla hajawadhuru,walimuuwa ,mwanamke kafia jela mwanaume bado anatumikia kifungo,nadhani umenielewa wakati mwingine kukaa kimya kunaweza kukakugharimu.
 
Usipotumia akili yako vizuri kwa hawa watu mtaishia kutujazia server za JF kila siku humu ndani...
 
Kuna Jamaa alikuwa anafanya kazi ya ulinzi,mkewe alikuwa na mazoea ya kuingiza mahawara mumewe akiwa kazini,siku ya siku akawafumania,Jamaa hakusema lolote wala kumgusa mgoni wake,Mkewe na mgoniwe wakaanza kuishi maisha ya hofu wakidhani kwamba Jamaa anataka kuwafanya kitu kibaya, haiwezekani awafumanie halafu asichukue hatua yoyote ,basi wakashauriana na hawara yake wamuwahi jamaa kabla hajawadhuru,walimuuwa ,mwanamke kafia jela mwanaume bado anatumikia kifungo,nadhani umenielewa wakati mwingine kukaa kimya kunaweza kukakugharimu.
Sasa kwa mazingira kama hayo hata ukaongea then ukanyamaza kimya inategemea mwanamke bado atakuwa na amani???,,maana kama ukimpiga utaleta matatizo tena ya jinai,,kwaio dawa kubwa ni kuwa kimya,,na si wote wanaweza kufikiria kukuua wengine huwa wanajiadhibu wenyewe kwa kujipa talaka unakuta kikitokea hivyo ukakaa kimya anatoka kurudi kwao
 
Hongera kwa moyo wako mkuu ila usijilaum kwa msaada uliompa mwache aolewe na wewe endelea na mishe zako. usipokee malipo ya fadhila ulyotenda kwa ngono maana huo msaada wako utakuwa hauna dhamani. kaamua kuolewa mheshim mke wa mwenzio ili na wako aheshimiwe.
 
Umeeleweka Mkuu (thamani)
 
Back
Top Bottom