Uchaguzi 2020 Adam Mchomvu ampiga mtama Emmanuel Mbasha stejini kwenye tamasha la CCM uwanja wa Uhuru

Amen kubwa!
 
Wameperekwa kwa ajili ya kupiga hela,ngoja watifuane.wote waliokua chadema wote wamebadilishwa kupiga hela.
 
Good job Baba Jonii,,,mnatuwakilisha vyema machalii wa araaa..mtu analeta mbambambaa miiiingiii af dizaini kuzarau kitu cha donyo sambu juu..unamtuliza tu..na hapo naamini haijaisha harakati lazima ziendelee.
 
Chama cha mapinduzi kupitia katibu wake wa uenezi, Ndugu H. Pole pole wameandaa tukio lililowakutanisha wadau mbalimbali wa burudani wakiwemo wasanii wa maigizo, muziki n.k. Waliloliita #UhuruKunaJambo linalofanyika katika uwanja wa uhuru.

Katika tukio hilo kuna tukio lingine limetokea, ambapo mtangazaji wa Clouds Fm pamoja na msanii Mbasha wamevutana mashati.

Tukio lilianza baada ya Mbasha kutumbuiza na kuwauliza mashabiki kuwa aendelee ama ashuke? Mashabiki wakasikika wakisisitiza kuwa ashuke lakini Mbasha akamwambia Adam kuwa wanasema aendelee. Kisha akaongezea kwa kusema "tatizo wewe Adamu bangi sana" maneno yale yalionyesha moja kwa moja hayakumpendeza Adamu maana hata Mbasha alivyokuwa anataka kumkumbatia, alimkwepa na kumputa mikono.

Adam akawa amesogea kwa pembeni kiasi, Mbasha akawa bado anang'ang'ania kubaki kwenye stage ndipo Adam akamkata ngwara na Mbasha kudondoka.

Wengi wamelitazama katika namna tofauti tukio hili. Wengine wakisema Mbasha amemkosea Adam kwa kusema kuwa Adam anavuta bangi tena mbele ya hadhira. Ni kumkosea, na anaweza kumfanya Adam kuwekwa chini na kuchunguzwa maana vyombo vya ulinzi na usalama vipo pale.

Baadhi wanamlaumu Adam kwa kumdhalilisha mwenzie mbele ya umati kwa kumkata ngwara, wanasema angesubiri wayazungumze wakiwa nyuma ya stage.

Wewe unalionaje hili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…