Uchaguzi 2020 Adam Mchomvu ampiga mtama Emmanuel Mbasha stejini kwenye tamasha la CCM uwanja wa Uhuru

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
12,381
2,000
Wakuuu huko Uwanja Wa taifa wasaniii wamezichapa live bila chenga baada Ya mbasha kumwiiita mchovu kuwa anavuta bangi.

Hakika kuna kitu hapa walioandaa hilo tamasha watakuwa wamejifunza kuwa wanachokifanya kinamchukiza MUNGU, watu kupigana live wakiwa wanatazamwa kwenye TV zaidi ya tano ni Aibu kubwa na hiii ni ishara Fulani kuwa MUNGU hayupo upande wenu na huenda mkakutwa na majanga zaidi.
Amen kubwa!
 

AGOLA

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,383
2,000
Wameperekwa kwa ajili ya kupiga hela,ngoja watifuane.wote waliokua chadema wote wamebadilishwa kupiga hela.
 

r2ga

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,233
2,000
Good job Baba Jonii,,,mnatuwakilisha vyema machalii wa araaa..mtu analeta mbambambaa miiiingiii af dizaini kuzarau kitu cha donyo sambu juu..unamtuliza tu..na hapo naamini haijaisha harakati lazima ziendelee.
 

Nsoji go Nvaa

JF-Expert Member
Oct 15, 2019
493
1,000
Adam na mbasha wapigana jukwaan baada ya mbasha kumtolea maneno ya kashfa Adam angalia video
 

Attachments

  • File size
    8.8 MB
    Views
    0

RAMAJ

Member
Sep 24, 2018
83
125
Chama cha mapinduzi kupitia katibu wake wa uenezi, Ndugu H. Pole pole wameandaa tukio lililowakutanisha wadau mbalimbali wa burudani wakiwemo wasanii wa maigizo, muziki n.k. Waliloliita #UhuruKunaJambo linalofanyika katika uwanja wa uhuru.

Katika tukio hilo kuna tukio lingine limetokea, ambapo mtangazaji wa Clouds Fm pamoja na msanii Mbasha wamevutana mashati.

Tukio lilianza baada ya Mbasha kutumbuiza na kuwauliza mashabiki kuwa aendelee ama ashuke? Mashabiki wakasikika wakisisitiza kuwa ashuke lakini Mbasha akamwambia Adam kuwa wanasema aendelee. Kisha akaongezea kwa kusema "tatizo wewe Adamu bangi sana" maneno yale yalionyesha moja kwa moja hayakumpendeza Adamu maana hata Mbasha alivyokuwa anataka kumkumbatia, alimkwepa na kumputa mikono.

Adam akawa amesogea kwa pembeni kiasi, Mbasha akawa bado anang'ang'ania kubaki kwenye stage ndipo Adam akamkata ngwara na Mbasha kudondoka.

Wengi wamelitazama katika namna tofauti tukio hili. Wengine wakisema Mbasha amemkosea Adam kwa kusema kuwa Adam anavuta bangi tena mbele ya hadhira. Ni kumkosea, na anaweza kumfanya Adam kuwekwa chini na kuchunguzwa maana vyombo vya ulinzi na usalama vipo pale.

Baadhi wanamlaumu Adam kwa kumdhalilisha mwenzie mbele ya umati kwa kumkata ngwara, wanasema angesubiri wayazungumze wakiwa nyuma ya stage.

Wewe unalionaje hili?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom