BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Hatua hiyo inafuatia Ukaguzi uliofanywa na CAG kubaini hasara ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), imeongezeka kutoka Tsh. Bilioni 104 mwaka 2020/21 hadi kufikia Tsh. Bilioni 205 mwaka 2021/22.
ACT imependekeza Mifuko hiyo ya Hifadhi ya Jamii iwe na Fao la Matibabu ambapo 20% ya Michango ya wanachama itawasilishwa #NHIF kila mwezi na makusanyo yake yatakuwa Tsh. Bilioni 530 kwa mwaka.
Uchunguzi wa CAG kwa mwaka 2021/22 umebaini Kadi za Bima ya Afya 21,042 zilitumika kupata huduma za Afya za Tsh. Bilioni 1.78 bila kuchangia chochote. Pia, Wategemezi 104,729 wasio na sifa walisababisha ongezeko la madai ya Tsh. Bilioni 15.17.
=========
Katika ripoti yake ya ukaguzi CAG amebaini hoja zifuatazo kuhusu Mfuko wa NHIF;
i.Wafanyakazi wa NHIF kujikopesha bila utaratibu na kushindwa kurejesha fedha za wanachama Matumizi mabovu ya fedha michango bilioni 41.42 kama mikopo isiyorejeshwa kwa watumishi wa NHIF ambapo alibaini kuwa wafanyakazi wa NHIF wamelimbikiza deni la shiingi bilioni 41.42 ambazo wamekuwa wakikopeshana.
Mfuko wa NHIF unatumia fedha za uendeshaji kufadhili mikopo ya wafanyakazi kinyume na Sera ya Mikopo kwa wafanyakazi ya NHIF uliopaswa kuwa na mfuko wa kuzungusha fedha.
ii. Malipo hewa
Vituo binafsi vya huduma za afya vinaongoza kwa kulipwa na NHIF madai yasiyo ya kweli ambapo CAG amebaini kuwa jumla ya shilingi bilioni 14.5 zililipwa kwa madai ya uongo na kugushi. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 10.38 (72%) zililipwa kwa vituo binafsi, vituo vya mashirika ya dini ilikuwa ni biliioni 2.49 (17%) na vituo vya Serikali ilikuwa bilioni 1.57(11%).
iii. Wanufaika wasiochangia
Uwepo wa wanuafaika wa huduma ambao hawachangii chochote ambapo CAG ameabaiini uwepo wa kadi hai 21,042 za NHIF ambazo zilitumika kupokea huduma mbalimbali za afya zenye thamani yashilingi bilioni 1.78 ingawa wachangiaji wao hawakutoa mchango wowote.
iv.Wategemezi waliokosa sifa
Wategemezi wa Zaidi ya Umri wa miaka 18 watumia shilingi bilioni 15.2 ambapo CAG amebaini uwepo wa wategemezi 104,729 wenye umri Zaidi ya miaka 18 ambao walinuafaika na huduma mbalimbali za afya ambazo madai yake yalifikia shilingi 15.17 bilioni.
Mfuko wa NHIF unakufa kwa sababu ya hoja zilizoainishwa hapo juu na vile vile Mfumo wetu wa Bima ya Afya sio endelevu na lazima ungekufa tu. Jitihda zote za Serikali kuokoa NHIF zimejikita kwenye ama kuongeza wachangiaji au kupunguza mafao na huduma kwa wanachama. Zimekuwa ni juhudi za kuokoa Mfuko badala ya kuokoa Mfumo wa huduma za Afya Nchini.
ACT Wazalendo inapendekeza kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo mzima wa Bima ya Afya nchini kwa kufungamanisha Bima ya Afya na Hifadhi ya Jamii. Tunapendekeza; Moja, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (NSSF na PSSSF) iwe na Fao la Matibabu ambapo kila mwanachama wa Mifuko hiyo awe moja kwa moja mwanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (ulioboresha).
20% ya Michango ya Wanachama wa Mifuko hii itawasilishwa NHIF kila mwezi kwa ajili ya kugharamia Fao la Matibabu. Kwa Pendekezo hili NHIF itapata wanachama wapya milioni 1.9 waliopo kwenye mifuko kutoka sekta rasmi na makusanyo ya takribani shilingi bilioni 530 kwa mwaka.
Pili, Serikali itoe kivutio kwa watu waliopo sekta isiyorasmi kama vile wafanyabiashara wadogo, wavuvi, wakulima, wafugaji, mamalishe nk kujiunga na Skimu ya Hifadhi ya Jamii kwa kuwachangia theluthi ya mchango wa kila Mwezi yaani shilingi 10,000 (Matching Scheme). Moja ya chanzo cha fedha cha kivutio hiki ni 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri kama ilivyopendekezwa hapo juu. Kwa Pendekezo hili takribani watu milioni 7.4 watakuwa wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na hivyo hivyo wanachama wa NHIF na makusanyo ya USD 266M
kwa kugharamia Matibabu.
Tatu, Serikali iwalipie asilimia 100 wafaidika wa TASAF kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na hivyo kuwa wanachama wa NHIF. Pendekezo hili takribani watu milioni 6.3 watapata Fao la Matibabu na makusanyo ya USD 205M kwa Mfuko.
Nne, ili kutekeleza mapendekezo yote hapo juu Serikali itenge kwenye bajeti ya kila mwaka asilimia 2.5 ya Pato la Taifa kwa ajili ya kugharamia matibabu na hivyo kuwezesha Watu wazima Milioni 11 kuwa na Bima ya Afya pamoja na wategemezi wao. Kwa mfumo huu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hautakufa na ndoto ya Bima ya Afya kwa wote itafikiwa.
Tano, kutokana na Hali ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ilivyo kufuatia hoja za ukaguzi zilizobainishwa na CAG, tunapendekeza kuwa Bodi na Menejimenti yote ibadilishwe, Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote uandikwe upya kuzingatia mapendekezo yetu hapo juu na sheria mpya ya NHIF itungwe ili kuimarisha mifumo ya huduma za Afya nchini.
ACT WAZALENDO