Nchaby
JF-Expert Member
- Aug 12, 2013
- 797
- 259
Watu wanaongea sana hawajui mwanzo wa ACT-Tanzania, hawajui misingi yake wala hawajui kuanzishwa kwake, Zitto sio mwanzilishi wala sio mwanachama wa ACT-Tanzania, hofu yenu kwake isiwasababishe mkawa wapiga ramli kila jambo zuri linaloelekea kuvuruga upuuzi wenu mkadhani ni Zitto tu ndiye awezaye kulifanya.....nimekaa kimya sana mnapotosha sana kuhusu ACT-Tanzania sasa nitawajibu...!!
ACT-Tanzania ina historia ndefu kidogo ilianza tangu mwezi 08/2013 mpaka ilipofika mwezi 11/2013 ikawa imekamilisha taratibu zote za awali hata kabla ya mgogoro wa CC ya cdm na Zitto kufikia ulipofikia,
Pamoja na yote hayo mjue hakuna mipaka ya kuwakaribisha watu, hata huyo Zitto akiona inamfaa anakaribishwa sana na wengine wote.
Kuna watu wanajifanya kuwa wanauwezo wa kuandika habari za siri za serikali mbona wameshindwa kujua kuhusu ACT-Tanzania jambo ambalo lingekuwa rahisi sana kwao? na badala yake wamekuwa watu wa kubuni tu andiko linalowaijia vichwani tu
![]()
Mkuu Nyakarungu, naomba tafsiri ya nyota kwenye bendera hiyo ya chama.
Kisha, naomba kujuzwa kadi za ACT zinapatikana wapi hapa Dar. Maana tunazisaka kwelikweli, tunashindwa wapi pa kuanzia.
Vilevile kama kuna uwezekano, ingekuwa vizuri watu tukajuzwa kilichomo ndani ya katiba ya ACT.