ACT ni mbadala wa CHADEMA au CCM?

ACT ni mbadala wa CHADEMA au CCM?

Watu wanaongea sana hawajui mwanzo wa ACT-Tanzania, hawajui misingi yake wala hawajui kuanzishwa kwake, Zitto sio mwanzilishi wala sio mwanachama wa ACT-Tanzania, hofu yenu kwake isiwasababishe mkawa wapiga ramli kila jambo zuri linaloelekea kuvuruga upuuzi wenu mkadhani ni Zitto tu ndiye awezaye kulifanya.....nimekaa kimya sana mnapotosha sana kuhusu ACT-Tanzania sasa nitawajibu...!!
ACT-Tanzania ina historia ndefu kidogo ilianza tangu mwezi 08/2013 mpaka ilipofika mwezi 11/2013 ikawa imekamilisha taratibu zote za awali hata kabla ya mgogoro wa CC ya cdm na Zitto kufikia ulipofikia,
Pamoja na yote hayo mjue hakuna mipaka ya kuwakaribisha watu, hata huyo Zitto akiona inamfaa anakaribishwa sana na wengine wote.

Kuna watu wanajifanya kuwa wanauwezo wa kuandika habari za siri za serikali mbona wameshindwa kujua kuhusu ACT-Tanzania jambo ambalo lingekuwa rahisi sana kwao?
na badala yake wamekuwa watu wa kubuni tu andiko linalowaijia vichwani tu

Mkuu Nyakarungu mbona hujaeleza chochote juu ya 'ifahamu ACT'. Badala yake umebaki kutetea kuwa Zito haymow Au kutokuwemo Zito ndio maana ya ACT?
Unaandika Kama Mtoto Wa chekechea, Au ulitokea mahala mahala Na kukurupuka!
 
Msidhani demokrasia IPO CHADEMA tu huo niujinga kila MTU ana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa acheni utoto na unafiki

Milango iko wazi kwa yeyote anaye taka kuondoka CHADEMA.By Dr Slaa.
 
Nyakarungu aliwahi kuandika hivi kwenye wall yake fb na kwenye liblog lake...
watu wengi
wanainbox kuhusu ACT kifupi
sifahanu act ni kitu gani na wala
sijui chochote
Leo anaijua hadi historia
 
Last edited by a moderator:
Wanachofanya ccm ni simple wanataka kudivide and rule....hatugawanyiki ng"o,labda hao wasiojielewa.
 
Nani kakwambia cheti ndio kipimo cha kujua mambo. hicho cheti ulicho nacho wewe ndio kinachokupa busara ya kutukana watu. Ninamashaka na elimu yako ya weza kuwa ya shingo ya twiga.

unajua mambo gani wewe msukule chambua mada kwa mawanda mapana wewe unatetea ujinga wa huyu mwenzako kwa chama ambacho hakina hata ofisi,bendera,kadi unaleta mahaba kwamba wanachukua nchi mwakani hujapewa kichwa chenye nywele tu ni pamoja na kufikiri inaonekana wewe ni mwalimu wa UPE
 
Mm.m1.m2.m3 na genge lao waacheni wamepoteza mwilekeo uchu wa madaraka hapo hakuna democrasia wanataka uogozi na huyo m2 ndio mwekiti wenu ama na baadaye mtampa mm kiongoza cha kama mlivyo weka kwenye waraka wa siri
 
ACT ni kitengo maalum cha CCM kinachoratibu mipango ya kuivuruga Chadema.
 
Wakuu,
Baada ya chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kupoteza uelekeo na kusambaratika, hatimae chama mbadala wa CHADEMA kimepatikana.
Chama hiki makini na mkombozi wa watanzania ni ACT.
ACT ni chama makini sana na viongozi wake ni wasomi hawajakimbia shule wala kupata division zero kwenye mitihani yao,
Sera kuu ya ACT ni maendeleo kwa vijana wote wa tanzania.
ACT ni chama cha watanzania wote hakina ubaguzi wa kidini, kikabila wala kikanda kama vyama vingine
Naomba serikali iboreshe daftari la kudumu la mpiga kura haraka ili vijana wajiunge na chama chao makini wanachokipenda cha ACT.
Naomba kuwakilisha hoja.

ACT imeanza kwa kushindwa; Kama hata viongozi wake hawajulikani, Ni chama cha kibaguzi-vijana pekee, kimeanzwisha ili kuwa mbadala Wa Chadema! hakuna jipya
 
Mm.m1.m2.m3 na genge lao waacheni wamepoteza mwilekeo uchu wa madaraka hapo hakuna democrasia wanataka uogozi na huyo m2 ndio mwekiti wenu ama na baadaye mtampa mm kiongoza cha kama mlivyo weka kwenye waraka wa siri

pole sana. act itakukomboa kifikra
 
Kweli CHADEMA ni chama makini, kwa nini kila chama kinaanzishwa kwa lengo la kupambana nacho wala si kwa lengo la kutoa wananchi katika lindi la umaskini na ujinga.
 
Nyakarungu
Point of correction.
ACT means Alliance for coward traitors
 
Last edited by a moderator:
Watu wanaongea sana hawajui mwanzo wa ACT-Tanzania, hawajui misingi yake wala hawajui kuanzishwa kwake, Zitto sio mwanzilishi wala sio mwanachama wa ACT-Tanzania, hofu yenu kwake isiwasababishe mkawa wapiga ramli kila jambo zuri linaloelekea kuvuruga upuuzi wenu mkadhani ni Zitto tu ndiye awezaye kulifanya.....nimekaa kimya sana mnapotosha sana kuhusu ACT-Tanzania sasa nitawajibu...!!

ACT-Tanzania ina historia ndefu kidogo ilianza tangu mwezi 08/2013 mpaka ilipofika mwezi 11/2013 ikawa imekamilisha taratibu zote za awali hata kabla ya mgogoro wa CC ya cdm na Zitto kufikia ulipofikia,
Pamoja na yote hayo mjue hakuna mipaka ya kuwakaribisha watu, hata huyo Zitto akiona inamfaa anakaribishwa sana na wengine wote.

Kuna watu wanajifanya kuwa wanauwezo wa kuandika habari za siri za serikali mbona wameshindwa kujua kuhusu ACT-Tanzania jambo ambalo lingekuwa rahisi sana kwao?
na badala yake wamekuwa watu wa kubuni tu andiko linalowaijia vichwani tu

Nurse Nyakarungu kwa Mbwembwe...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom