"Faida, msaada, umuhimu, maana" does not answer the question.
Cha faida, msaada, umuhimu, maana ni kipi?
Na faida kwa nani?
Ukoloni ulikuwa na faida kwa Waingereza, kimsingi haukuwa na faida kwa Watanganyika wengi.
Sasa ukoloni ulikuwa na faida au haukuwa na faida?
Ukiongelea faida bila muktadha, habari nzima inakosa maana. Ni kama vile kuongelea faida ya ukoloni bila kuongelea faida kwa mkoloni au mtwana.
Na unaposema mahusiano yawe ya faida tu, pengine kwako, siku utakapokuwa umepungukiwa, unataka msaada kutoka kwangu Kiranga.
Tuseme wewe masikini, umepungukiwa.
Unaniomba msaada nikusaidie.
Najua wewe masikini, huna namna ya kunifaidisha.
Uwezo wa kukusaidia ninao.
Nikukatalie kukusaidia, kwa sababu nikikusaidia wewe masikini, kwa kutaka kukusaidia tu uondokane na matatizo yako, mimi siwezi kufaidika?
Hili swali si la kinadharia tu.
Ni swali la kiukweli.
Kuna watu wanaomba misaada hapa tunasaidiana hata bila ya kujua kwamba tutakutana. Tunasaidiana tu kwa kanuni za ubinadamu.
Kanuni za Kiswahili za "Tenda wema wende zako, usingoje shukurani".
Sasa tuache kusaidia watu tusiowajua hata kama tuna uwezo, kwa sababu tu hatutafaidika kwa kuwasaidia?
Sent using
Jamii Forums mobile app