Achana na 'connection' ambayo haina manufaa

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Kuna kitu Wabongo tunajipa mizigo mizito tusiyoweza kuibeba.

Unakuta mtu ana contacts/followers/friends maelfu ambao huwajui, hamjawahi kuonana, hakuna uwezekano wa kuonana kikazi, hauendani naye lakini anang'ang'ana tu kuwa busy nao, kuchat, kutumiana emojis, picha na mengineyo.

Tuachane na msemo 'Connection ni dili'

Mtu hufanyi naye biashara atakuwaje na manufaa na wewe? Au manufaa ni kula beer, wanawake?

Ni bora niwe na contacts chache zenye manufaa kuliko kujaza MB za bure kwenye kichwa changu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakunaga mtu au kitu kisichokuwa na manufaa na wewe. Kama hakitakufaa leo kitaweza kukufaa kesho, na kama si kesho basi ni kesho kutwa ama mtondogoo, na hata kama sivyo basi siku au miaka ijayo kitakufaa....

Usidharau kitu au jambo au mtu ambavyo vimekuja katika maisha yako na ukaona vipovipo tu.

Kuna watu walipomaliza darasa la saba hawakuweza kuendelea na shule wakaingia mtaani wale walioendelea na shule wakawabeza sana ambao hawakufanikiwa kuendelea na shule na kubakia mtaani wakibangaiza....

Pengine hata wazazi wa hawa vijana walioendelea na shule wakashauri kuwa waache urafiki na hao ambao hawakumaliza shule.

Miaka imekwenda, dharau na kupuuzana na kudharauliwa kwa wazi wazi kukaanza.....

Leo yule aliyekwenda shule yupo kwenye desk la ofisi ya halmashauri, ofisi ya mamlaka ya kodi na kukata vibali, counter ya bank, au ni engineer akishuhudia yule wa darasa la saba akija kulipa kodi ya biashara yake ya mamilioni, akija benki kuweka mamilioni, akienda halmashauri kulipia leseni na vibari vya biashara mpya kila uchao, akisimamia ujenzi wa nyumba ya ghorofa ya yule wa darasa la saba.

Kalaga baho na kudharau watu au vitu sababu havina msaada na wewe kwa sasa. Ila mimi kwetu kupitia mzee wangu amenifunza kuheshimu kila mtu na kumthamini hata kama roho, akili na nafsi yako vinakukataza.

Tulikuwa tukipokea wageni waajabu sana kutoka bush ila mzee alikuwa akiongea nao kwa upendo na heshima na kuwajali na kuwasaidia. Sikuona faida yake zaidi ya kuona kero ila nilipokuja kuwa mtu mzima nikaelewa alichokuwa akikifanya mzee kuwa ni utu.....

Jifunze utu......

Haitakugharimu chochote ukituma sms hata ya salamu mara moja kwa wiki kwa wale ambao si msaada kwako ila wanaonyesha kukujali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfano connection ya madem kuna jamaa ww ukitaka demu mda wote anakupa connection na utampata


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom