Acha kujidanganya pesa sio kila kitu

Acha kujidanganya pesa sio kila kitu

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
58,001
Reaction score
134,197
dozenselection_6d15321d0a0d4e7e8a1018c30ee1b270.jpg

Huyu hapa Prince Al-Waleed bin Khaled bin Talal, ambaye anafahamika ulimwenguni kwa jina maarufu la “Sleeping Prince” April 18 mwaka huu, alitimiza umri wa miaka 36, ambapo umri huo umemkuta akiwa bado kitandani ‘coma’ bila fahamu zozote.

Mwanamfalme huyo wa Saudi amekuwa kwenye hali hiyo ya kupoteza fahamu ‘coma’ tangu mwaka 2005 kufuatia ajali mbaya ya gari ambayo aliipata Jijini London, Uingereza. Kwa miaka 20 sasa, Maisha ya Prince yanategemea mashine ya kupumulia, hata kula yake ni kupitia mipira.
 
Mbona kama heading na yaliyomo haviendani? Umemwona alivyopendeza? Bila shaka anapata first class care pamoja na kwamba yuko kwenye vegetative state. Bila pesa ingewezekanaje kumtunza hivi kwa miaka zaidi ya 20?

Kauli hiyo kwenye heading haikupaswa kutolewa na wewe mwasibu CPA mzima unayeelewa umuhimu wa pesa. Hiyo ni kauli ya kujifariji tu ambayo hutolewa na watu masikini waliojikatia tamaa huko!

Na kama pesa si kila kitu; nini ni kila kitu? Kuna hiyo kila kitu? 😳😳😳
 
Pesa sio kila kitu ni msemo wa kujifariji.
Bila pesa angeshakufa miaka mingi iliyopita ila pesa imefanya wapendwa wao kumuona hadi leo hata kama haongei.
Kilichomfanya awe hai wala sio pesa ni Neema ya Mungu tu,
Kumbuka alipata ajali na hakufa je pesa inaweza kumuokoa mtu na kifo cha ajali?
Wapo matajiri weeengi wameshindwa kujiokoa na kifo kwa pesa.
Pesa sio kila kitu ndo maana hata bill gate aliachana na mke wake pia jeff bezo aliachana na mkewe pesa hazikuwasaidia kwenye hilo na wanamiliki zaidi ya dollor billion 100.
Pesa inatoa tu utatuzi kwa mambo yanayoshikika( tangable things) lakini haifanyi lolote kwa mambo ambayo hayashikiki
Mfano unaweza nunua mwanamke na kufanya nae mapenzi lakini huwezi kumnunua mwanamke ali akupende utafeli
Asante nawasilisha
 
K
View attachment 3318502
Huyu hapa Prince Al-Waleed bin Khaled bin Talal, ambaye anafahamika ulimwenguni kwa jina maarufu la “Sleeping Prince” April 18 mwaka huu, alitimiza umri wa miaka 36, ambapo umri huo umemkuta akiwa bado kitandani ‘coma’ bila fahamu zozote.

Mwanamfalme huyo wa Saudi amekuwa kwenye hali hiyo ya kupoteza fahamu ‘coma’ tangu mwaka 2005 kufuatia ajali mbaya ya gari ambayo aliipata Jijini London, Uingereza. Kwa miaka 20 sasa, Maisha ya Prince yanategemea mashine ya kupumulia, hata kula yake ni kupitia mipira.
Kweli mkuu,Kuna siku tuko na Boss wangu, yeye alikuwa mtu wa kujisikia sana na kujiona MSOMI sana na kudharau watu!Siku Moja tumeeenda Singida njia ya Kwamtoro,Ambaye kapita njia hiyo ,anapajua ni mapori kwa kweli.
Tukiwa njiani gari ikapata pancha na rimu likawa limepinda na spare tyre halina upepo na hakuna magari yanayopita mara kwa mara!Kipindi hicho Hamna Hawa bodaboda,hivyo pikipiki ni za shida pia.Mimi nimekulia vijijini na nayaelewa maisha ya vijijini.Nikatafuta wanakijiji Rika langu,nikawaeleza shida yetu ya gari nk.Hali ikabadilika msaada Hakuna Basi linalopita hapo,ni Moja tuu na linaenda asubuhi na kurudi jioni.Bosi mazingira kwake haya ni mapya!Yule kijana niliyemfanya Rafiki,ndie Tukawa tunamtumia kwa dharula pale,Boss hana hata Moja hajui tunatokaje hapo ,Njaa,Njaa,Dogo akatutafutia kuku ,akasonga na ugali.Kumbuka tuna hela na tuko na Boss ila hapo hakuna Bar,Mgahawa Wala duka! Wanategemea minada ya kila mwezi kununua mahitaji Yao .Baada ya hapo asubuhi tukampa kijana ya kwenda mjini Singida na kuziba pancha na kurudi jioni na tyre!Kwa ufupi boss wangu alijifunza vitu vingi na Heshima debe!.Sure pesa si kila kitu kuna mahali haiitajiki pesa hata uwe nazo!.Mungu mwema humpa ampendaye na Humnyima ampendaye vilevile!
 
Kilichomfanya awe hai wala sio pesa ni Neema ya Mungu tu,
Kumbuka alipata ajali na hakufa je pesa inaweza kumuokoa mtu na kifo cha ajali?
Wapo matajiri weeengi wameshindwa kujiokoa na kifo kwa pesa.
Pesa sio kila kitu ndo maana hata bill gate aliachana na mke wake pia jeff bezo aliachana na mkewe pesa hazikuwasaidia kwenye hilo na wanamiliki zaidi ya dollor billion 100.
Pesa inatoa tu utatuzi kwa mambo yanayoshikika( tangable things) lakini haifanyi lolote kwa mambo ambayo hayashikiki
Mfano unaweza nunua mwanamke na kufanya nae mapenzi lakini huwezi kumnunua mwanamke ali akupende utafeli
Asante nawasilisha
Ndio maana naipenda JF!
 
View attachment 3318502
Huyu hapa Prince Al-Waleed bin Khaled bin Talal, ambaye anafahamika ulimwenguni kwa jina maarufu la “Sleeping Prince” April 18 mwaka huu, alitimiza umri wa miaka 36, ambapo umri huo umemkuta akiwa bado kitandani ‘coma’ bila fahamu zozote.

Mwanamfalme huyo wa Saudi amekuwa kwenye hali hiyo ya kupoteza fahamu ‘coma’ tangu mwaka 2005 kufuatia ajali mbaya ya gari ambayo aliipata Jijini London, Uingereza. Kwa miaka 20 sasa, Maisha ya Prince yanategemea mashine ya kupumulia, hata kula yake ni kupitia mipira.

Pesa ndio imefanya mpaka leo yupo, bila pesa angeshakufa kitambo sana, unajua cost za kumtunza mtu kwenye coma?
 
Kilichomfanya awe hai wala sio pesa ni Neema ya Mungu tu,
Kumbuka alipata ajali na hakufa je pesa inaweza kumuokoa mtu na kifo cha ajali?
Wapo matajiri weeengi wameshindwa kujiokoa na kifo kwa pesa.
Pesa sio kila kitu ndo maana hata bill gate aliachana na mke wake pia jeff bezo aliachana na mkewe pesa hazikuwasaidia kwenye hilo na wanamiliki zaidi ya dollor billion 100.
Pesa inatoa tu utatuzi kwa mambo yanayoshikika( tangable things) lakini haifanyi lolote kwa mambo ambayo hayashikiki
Mfano unaweza nunua mwanamke na kufanya nae mapenzi lakini huwezi kumnunua mwanamke ali akupende utafeli
Asante nawasilisha
Huyu jamaa alipata brain haemorrhage baada ya ajali, akaingia kwenye comma.

Fuatilia matibabu ya brain haemorrhage uone gharama zake. Hizo CT scan, na gharama za upasuaji si mchezo.

Lakini kwavile kwao wana hela, wameweza kumtunza kwa miaka 20. Wangekuwa masikini wangeshampoteza.

Kama Allah angekuwa anampenda kweli asingeruhusu apate ile ajali iliyomsababishia haya.
 
Pesa sio kila kitu ni msemo wa kujifariji.
Bila pesa angeshakufa miaka mingi iliyopita ila pesa imefanya wapendwa wao kumuona hadi leo hata kama haongei.
VEry true haya maisha bila ya pesa utaishia kudhalilika tu hadi mke wako utagongewa, pesa ndio heshima ya binaadamu, angalia leo musk amekuwa kama waziri mkuu wa marekani kisa pesa tu
 
Kilichomfanya awe hai wala sio pesa ni Neema ya Mungu tu,
Kumbuka alipata ajali na hakufa je pesa inaweza kumuokoa mtu na kifo cha ajali?
Wapo matajiri weeengi wameshindwa kujiokoa na kifo kwa pesa.
Pesa sio kila kitu ndo maana hata bill gate aliachana na mke wake pia jeff bezo aliachana na mkewe pesa hazikuwasaidia kwenye hilo na wanamiliki zaidi ya dollor billion 100.
Pesa inatoa tu utatuzi kwa mambo yanayoshikika( tangable things) lakini haifanyi lolote kwa mambo ambayo hayashikiki
Mfano unaweza nunua mwanamke na kufanya nae mapenzi lakini huwezi kumnunua mwanamke ali akupende utafeli
Asante nawasilisha
Kama Hautonipenda Mimi utapenda pesa zangu, Tupambane Tupate pesa, kwa Upande huuu wa wanawake Bora usingesema wanapenda sana Pesa dada Zetu.
 
Back
Top Bottom