Acha kuishi kwa hofu na wenge, kapime ujue afya yako

RoadLofa

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
1,347
2,957
Acha Hofu na Wenge kapime ujue afya yako...

Kwa kipindi Cha miaka miwili nimekuwa nikiishi kwa Hofu na kujichukulia kama mwathirika HIV aka ukimwi aka Ngoma aka umeme utaongeza aka nyingine

Basi bhana kutokana na iyo Hofu nilikuwa najikuta nakonda kweli na kuumwa hakuishi yaani nikiumwa tu kidogo najisemea moyoni tayari kitu kimeitika basi nilikuwa naishi kinyonge sana na wasiwasi Hadi watu WA karibu na Mimi walikuwa wananiuliza vipi unaumwa mi nawakatalia uku nikiwa na yangu kichwani

Iyo Hofu ilikuwa unakuja kutokana na machaka niliyopita ni mengi aisee sio shivaz chugga,kaumba Moro na mengine mengi kutokana na kujichukulia mwathirika Tena bila kupima nilikuwa naishi maisha ya kujikatia tamaa sana na kuishi maisha rough na kushiriki ngono rough rough,.

Ila Leo baada ya kwenda hospital kwa ugonjwa x ( please respect my privacy) dr.alinishauri kucheck na Ngoma aisee nilikuwa na ogopa kinoma na kijasho chembamba ila results zilikuja Niko negative aisee nimefurahi sana

Nachojihaidi kwenye nafsi yangu kuanzia Leo sitoishi maisha niliyoishi hapo nyuma na ntaitunza afya yangu kwa nguvu zote,na nimepanga kuja kuthibitisha Tena baada ya miezi mitatu hospital nyingine.

Ushauri wangu vijana tuishi kwa kujali sana afya zetu ,afya ndo Kila kitu kwenye Aya maisha pia kapimeni acheni kuishi kwa Hofu.

Unaweza kushare experience yako ulipoenda kupima kwa mara ya kwanza hapo chini.
 
Tulia wewe. Nyie ndo mnarudisha Canada nyuma. Unaishi Ottawa hata kifaransa hujui. Rudisha iyo passport ya Canada urudi nyumbani. Traduea has 18 months to go.

Nyau ww
Nyie Conservative mna wenge sana. Trudeau hana nongwa hata kidogo. Harufu za mikojo za mabibi zikikuchosha karibu.

Acha kukosea jina la PM. Wewe hujawahi kuwa na akili..
 
Kupima Afya sio VVU pekee bwashee. Wewe umepima kwa bahati mbaya (shinikizo) tu, kisha unakuja kushangaa wenzio!

Kupima ugonjwa usio na tiba ni wendawazimu.
 
Kuna magonjwa hatari zaidi ya hiyo ngoma uliyokuwa unaiogopa.
+ Kuna inflammation nyingi sana exp: nephritis, hepatitis B, cervicitis, etc

+ Kuna cancers nyingi sana zote tupo kwenye hatari zakupata muda wa wowote za zikapelekea kifo.
Bila kusahau ajali na majanga.

+ Be humble, kula vizuri kumbuka kucheki afya mara Kwa mara, muombe Mungu Kwa pumzi yake Fanya kazi Kwa nguvu mengine muachie yeye.
 
Back
Top Bottom