ACACIA wapinga vikali Matokeo ya Kamati ya pili ya Rais

ACACIA wapinga vikali Matokeo ya Kamati ya pili ya Rais

Bia na sigara ndo zimekuwa zikiongoza kwa mapato apa nchini.. Sasa kweli usipoamin tulikuwa tunaibiwa tukuelewe vp..
1gram of gold = 32 beerbottles...!!
Kwa hesabu za kawaida iyo ACACIA wanayodai kuzidishiwa x10 ipo sahihi wala ata hawajaonewa..
Hofu yangu ili swala linaweza kuishia njiani kwa sababu wahusika wakuu ni KIKWETE & MKAPA.. mtapindisha kwa kina CHENGE & YONA ila hawa ndo wakubeba huu msalaba
 
Mola amuongezee ujasiri kiongozi wetu wa nchi haswa katika jambo hili kubwa na zito.kuna watu sijui ni utoto au uwehu unawasumbua;hata kama mtu ni mpinzani lakini kubali ukweli na tuwe na uzalendo na nchi yetu.
 
Sasa hapa nani mkweli?? Serikali inataka chao ila ACACIA wanadai hawadaiwi?? Nahisi kma ICSID inanukia ili ukweli ujulikane

Tatizo kubwa lililopo no uongozi mbaya unaoongozwa na jazba.

Tulipata hasara kubwa ya kulipa mabilioni ya shilingi kwa wavuvi maharamia na meli yao, ingawa hatua zilizochukuliwa zinlionekana kushangiliwa na watu wakaonekana mashujaa. Baada ya hasara ile, hakuan tena aliyejitokeza kulinzungumzia ili angalau liwe funidisho kwa watu wengine na nyakati zingine.

Ninajua tume imejumuisha wataalamu wakuaminika. Lakini mashaka yangu ni juu ya kuffanya kzi kisiasa na kugemea upande mmoja kwa lengo la kujipendekeza. Ninaona bashite amewapa seminar na mwongozo wa hali ya juu wote wanaotaka kudumu kwenye green circles. KWAMBA UNAFIKI UNALIPA!. Mnafiki anakula taratibu kivulini, ila anapoharibu hasara ni kwa walilpa kodi. mali ya umma haina uchungu.!.

Umesikia wengine (katika hali y akushangaza), na as if shetani aliamua kuwaumbua, hata wakadiriki kutapika uchafu ulioko katika miyo yao kwamba "HATA KAMA TUKISHINDWA KESI, GHARAMA SI TUTALIPA SOTE?"? Eti hii ni kauli ya mtu aliyeaminiwa kuwa kiongozi mkuu wa masuala ya sheria za nchi! Eti kateuliwa asaidie kusukuma gurudumu la taifa katika kitengo cha sheria, badala ya kulisukuma kumbe analirudisha nyuma kwa upumbavu kwamba hata likikwana hasra ya wote. Huyu kweli anasthili kupewa hata ukatibu wa kijiji?

Narudi kwenye hoja kwamba kama hakuna kelele za kisiasa zinazoasisiwa na utashi wa kucheza kwa kufuata mdundo uliopo wa kukurupuka, kutaka sifa, ubabe na unafiki, bila shaka kamati itakuwa imefanya kazi na maamuzi yake yamesimama katika nguzo isiyoyumba (ambayo sikeele za kidictator kwa kuwa dictatorship bila kanuni ni mauaji ya halaiki.

Kinachonipa hofu ni kwa nini kila report inapotoka ACACIA wanapinga kwa nguvu? Hizi report zimechunguzwa wapi? Wamepata nafasi ya kukaa na uongozi wa ACACIA ili kupata maelezo na vielelezo vyao au ni maneno ya CCM? Kama wameshirikishwa katika vikao vya uchunguzi, kwa nini kila taarifa inapotoka wanaonyesha mshituko mkubwa wa kukataa? Nini hatima ya mshituko na kukataa kwao kwa upole huku wakiipa nafasi tanzania ya kukaa nao meza moja kuzungumza? Ina maana katika uchunguzi hawakukaa meza moja kufahamu hata nguzo zinazowapa ujasiri wa kuiba? Hii isingekuwa fursa muhimu kwetu kujua wapi panatakiwa usimamizi hasa kwa Regulator and supersors wa hawa investors?

Hivi hadi haya yote yanafanyika na ACACIA inafanya kazi bila kibali, hii serikali ilikuwa wapi? Hizo fedha za mirahaba sijui tozi, tulikuwa tunazichukua kwenye kampuni isiyokuwepo, kama serikali ni kwa misingi gani? Tunawezje kuchukua kodi kwenye biashara ya kuu za bangi wakati tunafahamu hiyo ni haramu?

Ninajua kuna regulatory systems za serikalil na supervisory services. Hawa wanaosimamia makampuni ya uchimbaji ni akina nani? Muda waote wanasimamia kampuni hewa, wanasimamiaji hewa? Kumbe wanaangalia nini katika kuhakikisha compliance kwa requirements na standards? Kizi terms na viwango wanavyotakiw kuangalia hawa jamaa ni vipi?

Kama hawajashirikishwa ACACIA, na ACACIA wakaja na vielelezo muhimu kwamba wamefuata kila walichotakiwa kukifanya ndani ya mikataba yao na CCM, ambayo siku zote imekuwa ni siri kubwa na mauti kwa Watanzania, nini yatakuwa madhara? Serikali itatuambia tukae kwenye runinga tusikie mwenendo wa mashitaka au utetezi wa AcACIA kama tulivyohamasishwa leo hadi Bunge kuwal live wakati ni siku ya kazi AU tutaambiwa hakuna kurushwa ili tufanye kazi au ITAKUW AKIMYA KIMYA KAMA MAHARAMIA WA SAMAKI?

Nina maswali mengi kuliko majibu.

Ninaomba anayefahamu anisaidie.
 
Kuna watu wanajitoa ufahamu na kufuata mikumbo tu hata kwenye masuala ambayo yanagusa mpaka familia zao,kwa hili nampa BIGUP sana MAGU,hongera sana raisi wetu
 
Sasa hapa nani mkweli?? Serikali inataka chao ila ACACIA wanadai hawadaiwi?? Nahisi kma ICSID inanukia ili ukweli ujulikane
Wewe unaonaje,hawadaiwi?Tabia hizi za undumi la kuwili Watanzania hazitatufikisha popote,ni lazima tubadilike.
 
Acacia wezi tu kwanza waliwafukuza wafanyakazi Wa Tanzania wengi bila fidia...wametuibia sana
 
Magu naona kuna watu anawafuta Sema approach anayotumia itakula kwake, nakumbuka kikwete naye wakati anaingia madarakani alianza hivi hivi kumtafuta che nkapa kutokana na bifu zao, tatizo likawa approach maana kila anapogusa iliamalize anajikuta na yeye yumo matokeo yake yeye mwenyewe ilibidi aombe poo.
Ndio ramli yako inavyokupa majibu
 
Hatua zilizochukuliwa
1. Hatua ya JPM kusitisha mchanga kwenda nje kwa ajili ya uchunguzi ni sahihi.
2. Report ya kwanza na Mapendekezo yake ni sahihi.
3.Report ya pili na Mapendekezo yake ni sahihi pia.

Mkakati ya Team JPM
Hatua zote tatu ni sahihi kwasababu alichofanya JPM sio kuvunja mkataba au kuzuia moja kwa moja usafilishaji wa mchanga bali ni strategy za kuwafanya ACACIA warudi kwenye meza ya majadiliano wakiwa hawana confidence kwa kudai share kubwa ukilinganisha kama wangeitwa bila JPM kutengeneza Cheos, kwahiyo uundaji wa tume zote mbili pamoja na ya Tatu ambayo alisema yeye mwenyewe haijui ni mpango mkakati wa kutengeneza room nzuri ya negotiation ili apate faida kama nilivyoanisha hapo chini.
Kumbukeni kamati ya bunge ilishawahi kupitia sera na mikataba ya madini wakaishia kuambulia mabadiliko madogo sana.

Faida ya kutengeneza mtafaruku
1.JPM atakuwa na evidence ya uwizi wanaofanya wakati wa majadiliano mapya
2. JPM atakuwa anajua na ataenda na share anayoitaka kuidai kwenye meza ya majadiliano
3. Hata kama ACACIA wanabebwa na baadhi ya vipengele kwenye mkataba, watakuwa hawana confidence ya kudai share kubwa kutokana na Guilty Consciousness baada ya kuvuliwa taulo.
4.JPM atakuwa na room ya kudai share nyingi hadi kwenye pure gold mbali na makinikia
5.JPM atapata room kubwa ya kureview mikataba ya madini na gas kama ambavyo ameshaagiza kwasababu wawekezaji watamuona yuko serious tofauti na waliopita.
6.Kulingana na mazingira na ukweli uliojulikana, ni ngumu kwa ACACIA kwenda mahakamani, watataka hili swala liishie mezani. Kwahiyo habari ya ACACIA kwenda mahakamani sahauni.

Toafuti ya JPM na Lissu kimkakati

1.JPM aliamua kutengeneza mgogoro ili apate faida nilizo hainisha hapo juu na zitampa faida-Best Approach.
2.Lissu alitaka tuilete mikataba bungeni kwa ajili ya marekebisho, akaiponda aproach ya JPM-Weak Approach

Kwanini JPM yuko sahihi

Mikataba itakavyorudishwa bungeni kujadiliwa JPM atakuwa na evidence, na watajadili kulingana na evidence na Loop holes zilizoainishwa na kamati zote.

Kwanini Lissu hayuko sahihi sana

Approach yake ingesababisha bunge kujadili mikataba Blindly bila evidence yoyote hivyo serikali kuambilia kiduchu kama kamati ya akina Zitto.

Dhamira
Lissu anadhamira nzuri kama JPM, ila kwenye hili wamenzidi ujanja kweye approach ataonekana kama msaliti wakati siyo msaliti, na wanamchafua kwa kunakili mistari michache na mifupi kwenye hoja zake ili waonyeshe ni msaliti.

Hitimisho
JPM amejipanga kwenye hili swala na ndiyo maana kwenye conclusion yake aliwaita ACACIA kwenye majadiliano, na kabla ya kuwaita aliwapiga mkwara kama wataenda kumshtaki hawatachimba madini Tanzania, na unajua madini yamebaki nchi chache duniani, huamuzi wa kuondoka jumla utakuwa ni mgumu.

Hayo ndiyo maoni yangu.

Umeongea facts mkuu na hongera
 
Umeongea facts mkuu na hongera kwa uchambuzi mzuri
 
Dude limeamshwa,ngoja tuone serikali na kampuni nani zaidi.
 
Naona kila upande unamtegea mwenzie unasema upo tayari kwa majadiliano. Sasa hapa kama una akili utajiuliza maswali mengi. Wa kwanza alie ibiwa anadai chake lakini hamfikishi mahakamani mwizi wake, na yule alietuhumiwa kuiba na kuzuiliwa mali zake na kusababisha kuchafuliwa ambapo hisa zake zimeporomoka kwa kiasi kikubwa nae hataki kumshitaki aliemchafulia jina, aliemuingiza hasara ya hisa na bidhaa zake zilizoshikiliwa nae anasema yupo tayari kwa majadiliano. Kuna alama kubwa sana ya kuuliza na ya mshangao ambazo hazionekani ni za kufikirika ambazo hazionekani kwa macho zinahitaji majibu ya kufikirika.

Ukiona mtu ameshikwa ugoni halafu anasema nakubali yaishe WE TIA AKILI
 
Nani alitegemea hawa wakoloni wakubaliane na findings za tume? Haijawai kutokea

Kumbe nyinyi wakoloni wa Tanganyika mbona mnapoambiwa muungano ni uvamizi hamkubali ?? Huku mnaendelea kuikandamiza Zanzibar na kuwafunga watu wake kwa kudai uhuru. Laana za uvamizi zitaendelea kuwatafuna mpaka muiteme Zanzibar
 
nawapa pole kwa wafanyakazi wa kampuni za madini kwa maana naona sasa wanahangaika kutuma cv sehemu nyingine, sio makosa yenu ni makosa ya wawekezaji wenu kwa kuleta ubabaishaji tanzania.
 
]Acacia remains open to further dialogue with the Government regarding this issue and continues to assess all of its options. We will provide a further update to the market as soon as practical.
Anameremeta anamereneta Acacia anameremeta Lazima aolewe tu
 
Issue hii inataka uwe
Si mnaye mwanasheria nguli na mahiri kuliko wote Tanzania, Tundu Lissu? Mwazimisheni kwa Acacia awasaidie
Huru na,si kupelekeshwa na misisimuko.Tundu Lissu na JPM wote wana haki ya kusikilizwa.Tumefika hapa tulipofika si kwa miujiza,bali kuna wenzetu ndiyo wametufikisha hapo na,JPM ni sehemu ya hao waliotufikisha hapo. Busara inataka aombewe radhi kwa niaba ya wenzie.Akili ya ku-shift mambo haikubaliki hata kidogo.
 
12 Juni 2017
Mwitikio wa Acacia kwenye matokeo ya kamati ya pili ya Rais

Acacia imeona matokeo ya kushtua ya kamati ya pili ya Rais iliyowasilishwa kwa Rais wa Tanzania Mh. Dk John P. Magufuli leo asubuhi ambayo imeangalia nyanja za historia za kiuchumi na kisheria ya mauzo ya nje ya makanikia ya madini.

Kamati ya Pili imetoa matokeo yake kwa kutumia matokeo ya Kamati ya Rais ya Kwanza, iliyotangazwa tarehe 24 Mei 2017, ambayo Acacia imeikanusha vikali. Kamati hiyo ilipata matokeo yake kwa kutumia sampuli ya kontena 44. Kwa mujibu wa data za zaidi ya miaka 20 tulizonazo ni vigumu kuoanisha matokeo yetu na yaliyokutwa na kamati, na kamati imetoa thamani ya juu kwa zaidi ya mara 10 kuliko thamani halisi ya makanikia

Kamati ya Pili inadai kuwa Acacia imetangaza kiasi cha chini cha mapato kuliko inavyopata na kulipa kodi kidogo kuliko inavyostahili kwa miaka mingi na kuficha mabilioni ya dola ya Marekani. Na hivyo imefanya mapendekezo kadhaa ikiwa ni pamoja na Acacia kulipa kodi inayodaiwa na mirahaba, kufanya majadiliano upya ya mikataba mikubwa ya uchimbaji madini, umiliki wa Serikali katika migodi, na muendelezo wa marufuku ya kuuza nje.

Acacia inakanusha vikali tuhuma hizi mpya zisizo na ushahidi. Sisi tumefanya biashara zetu kwa utaratibu bora kabisa na kwa kufuata sheria zote za Tanzania. Tunarudia kusema tena tumeweka wazi kila kitu chenye faida tulichokuwa tunazalisha tangia tuanze uchimbaji Tanzania na tumelipa kodi na mirabaha yote inayotakiwa kulipwa, na kwa kuongezea mahesabu yetu tunayotoa yanakaguliwa kila mwaka kwa viwango vya kimataifa vinavyoendana na IFRS.

Acacia kwa muda mrefu tulitaka kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuwa tunaamini wote tuna malengo sawa katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Hata hivyo, ushirikiano huu lazima uwe na misingi ya haki kwa wadau wote, ikiwa ni pamoja na 96% ya wafanyakazi katika migodi yetu ambao ni Watanzania, na wanahisa wetu ambao wamechangia dola bilioni 4 za uwekezaji ambazo Acacia imefanya ndani ya nchi hadi sasa.

Acacia bado inakaribisha mazungumzo na Serikali kuhusu suala hili na inaendelea kutathmini nini inaweza kufanya . Tutatoa taarifa zaidi kwa soko kadri tutakavyoweza kufanya .

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu
www.acaciamining.com

=================================

1
LSE:ACA www.acaciamining.com
12 June 2017
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION
Acacia Mining plc
LSE:ACA
(“Acacia” or the “Company”)
Update on the 2nd Presidential Committee Findings
Acacia notes the disappointing findings of the Presidential Second Committee’s report which were presented to the President of Tanzania H.E. Dr. John P. Magufuli this morning and which considered the historical economic and legal aspects of the export of metallic mineral concentrates.

The Second Committee has primarily based its findings on those of the First Presidential Committee, announced on 24 May 2017, that Acacia strongly refutes. That Committee based its findings on samples from 44 containers. Based on more than 20 years of data available to us it is impossible to reconcile those findings and they grossly overstate the value of the concentrates by more than 10 times.

The Second Committee has alleged that Acacia has under-declared revenues and tax payments over a number of years by tens of billions of US dollars. As a result it has made a series of recommendations including the payment of outstanding taxes and royalties, re-negotiation of large-scale Mineral Development Agreements, Government ownership in the mines, and the continuation of the export ban.

Acacia strongly refutes these new unfounded accusations. We have always conducted our business to the highest standards and operated in full compliance with Tanzanian law. We re-iterate that we have declared everything of commercial value that we have produced since we started operating in Tanzania and have paid all appropriate royalties and taxes on all of the payable minerals that we produce. In addition, our published accounts are annually audited to an international standard in accordance with IFRS.

Acacia has long sought to be a partner with the Government of Tanzania as we believe that we have similar goals in enhancing social and economic development in the country. However, this partnership must be based on fairness for all stakeholders, including the 96% of our employees at our mines who are Tanzanian, and our shareholders who have funded the US$4 billion of investment that Acacia has made into the country to date.

Acacia remains open to further dialogue with the Government regarding this issue and continues to assess all of its options. We will provide a further update to the market as soon as practical.

ENQUIRIES
For further information, please visit our website: www.acaciamining.com or contact us
Eeeh haya
 
Back
Top Bottom