ACACIA wapinga vikali Matokeo ya Kamati ya pili ya Rais

ACACIA wapinga vikali Matokeo ya Kamati ya pili ya Rais

Tume imefanya kazi kwa siku 14 ndo wakaja na data hizo ila wao wanandika kila Wanapo jisikia.Research hupingwa kwa Research
 
Hata raisi ametoa nafasi ya Dialogue.
Lakini nadhani wajitokeze tu kuwa walikuwa wanatupiga kiasi gani na wako tayari kutu lipa.

wataelewana tu na nilichokiona leo wala JPM hahitaji ugomvi na hao jamaa ila anataka kuvuta chake maana kakuta akina mkapa walishavuta vyao, hivyo wakimchana hayo matrillion lazima biashara iendelee kama inavyoendelea kwa akina bakhresa na dangote....
akina yona na karamagi watabaki salama tu wanachotakiwa ni kuhojiwa ili ukweli ujulikane ambao naamini kabisa hata yeye anaujua ila kwa vile watanzania wengi ni manyumbu inabidi acheze na akili zao halafu yeye afanye yake....hakuna kitu kizuri kama kujificha katika kivuli cha uzalendo unaweza piga mabilioni mpaka ukachanganyikiwa na mamnyumbu yakaendelea kukusifia huku yanakufa na njaaa na wala hayana madawa hospitalini na wala haya ajiriwi.. na pia yanakosa mikopo ya limu ya juuu..


hahaha i must be honest to my country
 
Wenye akili zetu zilizotukuka tunamuamini 100% Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari Dkt. John Pomba Joseph Magufuli na sio hao Wezi Rasilimali za Watanzania ACACIA. Rais ni Taasisi hivyo nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Watendaji wa Rais ambao kiujumla ni Idara zake Nyeti zote pamoja na Tume aliyoiteua zimefanya Kosa hadi zikampa taarifa Mheshimiwa Rais pamoja na Wasaidizi wake Wakuu wote Makamu Samia na Waziri Mkuu Kassim mbele ya Hadhara kubwa kama ile yenye Watu wazito na wanaoheshimika katika nchi hii.

Tanzania tulimuhitaji Rais Magufuli miaka 20 iliyopita na nina uhakika kama angekuwepo Yeye kwa haya anayoyafanya na aliyoyafanya leo hii Tanzania tungekuwa tunakimbizana na akina South Africa, Morocco na Malaysia Kimaendeleo na Kiuchumi. Uthubutu huu wa Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ni ishara kubwa ya Ushujaa wake na Uzalendo wake wa Kweli kwa Taifa hili na nadhani hao ACACIA badala ya kutaka kuwazuga na kuwafanya Watanzania ni Wapumbavu / Mapopoma basi wangeanza Kwanza Kutubu kwa Mwenyezi Mungu kisha kwa sisi Watanzania kwa Ufedhuli na Ukatili wa Kiuchumi waliotufanyia tokea mwaka 1998 hadi leo.

Mungu mbariki sana Rais wa JMT Dkt. Magufuli
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Africa.
Umejiita mwenye akili nataka unijibu kulingana na uwezo wa akili zako zilivo kubwa, Hiv Acasia na hawa viongozi wa chama chako nani mwenye makosa?
 
Tatizo JPM anatenda kwa imani na hisia! Sijui ingekuwaje leo kamati ingesema tofauti na imani na hisia hizo!

Kama lipo tatizo ni vigumu sana kuwapata katika meza huru! Waliotuangusha ni viongozi wetu, watendaji wetu , wanasheria wetu na wabunge wetu! Hawakutafakari walichoamua na hawakuamua walichotafakari!
Walitafakari sana na wala elewa sana tatizo ni mshiko uliosababisha sauti ya ndiyoooooooo ikawa kubwa zaidi kuliko siyooo. Kwahiyo ICSID inahusu hapa kama alivyosema commander tal. Nani anabisha?
 
How about one big fact that acacia has never be registered with brela??
Kuna vitu vingine havina logic kabisa. Hivi hawa kutosajiliwa ni kosa la nani?

Waliwezaje kufanya biashara bila ya kusajiliwa? Waliwezaje kusajiliwa soko la hisa DSE wakati hawatambuliki kisheria? Walilipa kodi kwa account/TIN gani? Waliwezaje kufanya kazi muda wote huo bila kuwa na uhalali? TRA waliwezaje kwenda kumdai kodi asiyefahamika?

Kama ni kweli basi nchi hii ni tupu. Ukilitazama hili la usajili, kama ni kweli, basi matatizo ni yetu, siyo ya ACACIA. TIC ndiyo ina jukumu la kuwaelekeza wawekezaji wote juu ya taratibu za kuwekeza Tanzania. TIC ni yetu, siyo ya ACACIA, ilitimiza wajibu wake? Kwa hiyo ina maana nchi hii kampuni inaweza kuingia na kuanza na sisi tukakimbilia kukusanya kodi bila ya kutambua kama inatambulika au la!! Ajabu kweli!! Kampuni inapoandikishwa soko la hisa la DSE huwa halitakiwi kupeleka Registration Certificate? Nafahamu hata ufunguaji wa bank account makampuni hutakiwa kupeleka Certificate of Incorporation, hao ACACIA walikuwa wanapeleka nini?

Kuna vitu ambavyo kwenye ripoti havijakaa sawa. Tumeambiwa Acacia walianza kuchimba mwaka 1998 - siyo kweli. Hii kampuni ilikuwa bado haijaanzishwa.

Tumeambiwa China ina smelter wakati haina dhahabu, siyo kweli hata kidogo. China ina migodi mingi tena mikubwa. Inazalisha dhahabu zaidi ya tani 400 kwa mwaka, karibia mara 15 ya uzalishaji wa Tanzania. Wazalishaji wakubwa kabisa watatu wa dhahabu Duniani 1) China 2) Australia 3) Russia.
 
Naona kila upande unamtegea mwenzie unasema upo tayari kwa majadiliano. Sasa hapa kama una akili utajiuliza maswali mengi. Wa kwanza alie ibiwa anadai chake lakini hamfikishi mahakamani mwizi wake, na yule alietuhumiwa kuiba na kuzuiliwa mali zake na kusababisha kuchafuliwa ambapo hisa zake zimeporomoka kwa kiasi kikubwa nae hataki kumshitaki aliemchafulia jina, aliemuingiza hasara ya hisa na bidhaa zake zilizoshikiliwa nae anasema yupo tayari kwa majadiliano. Kuna alama kubwa sana ya kuuliza na ya mshangao ambazo hazionekani ni za kufikirika ambazo hazionekani kwa macho zinahitaji majibu ya kufikirika.
ndg yangu nakuapia utapata presha ya kushuka pamoja na kisukari km utaendelea kujiuliza hayo maswali na kufuatilia 'kindakindaki' suala hili; WANAJUANA HAO!!!!. ushauri wangu, chukua ngwamba lako km huna kazi nenda zako nanjilinji -kilwa kajilimie ufuta....mwaka huu bei ndogo wakulima wanalia lkn mwakani inaweza kupaa kidogo...ni kuishi kwa matumaini tu. km huniamini basi subiri halafu nitakuja kukuuliza lilipoishia.
 
Umejiita mwenye akili nataka unijibu kulingana na uwezo wa akili zako zilivo kubwa, Hiv Acasia na hawa viongozi wa chama chako nani mwenye makosa?

Akili zangu Kubwa haziniruhusu Mimi kujibu swali la Kipumbavu / Kipopoma kama hili lako.
 
ndg yangu nakuapia utapata presha ya kushuka pamoja na kisukari km utaendelea kujiuliza hayo maswali na kufuatilia 'kindakindaki' suala hili; WANAJUANA HAO!!!!. ushauri wangu, chukua ngwamba lako km huna kazi nenda zako nanjilinji -kilwa kajilimie ufuta....mwaka huu bei ndogo wakulima wanalia lkn mwakani inaweza kupaa kidogo...ni kuishi kwa matumaini tu. km huniamini basi subiri halafu nitakuja kukuuliza lilipoishia.
Hahaa ... ushauri wako nitazingatia.
 
Kwa hiyo ACACIA wanachosema ni kua hizi findings za pili wamechukua sample ya data kutoka kwenye zile za kwanza.
Hili ni kweli? Kama ni kweli kwa nini wamefanya hivyo? Makontena yapo si wangeenda wabebe tu sample nyingine yaani wafanye kila kitu from scratch? au kuna mtu anahofia makontena yatakua yameguswa?
Kwa mchumi na mwanasheria sample ya mchanga akafanyie nini?!
 
Big up Tanzania and Tanzanians who are willing and ready to sacrifice everything for the protection of motherland. The neocolonialists and their locally embeded leeches have to stop their dirty tricks.
 
Nani alitegemea hawa wakoloni wakubaliane na findings za tume? Haijawai kutokea
All in all tuko vitani sawa, lakini mimi ninaulizia swali la msingi aliyewaonyesha ma adui mlango wa armery yetu ni nani? Bado yuko hai? Kuna nini kinachoendelea kuhusu huyo? Inawezekana kweli waziri wa madini on his own ataliamsha dude likaanza kuwatafuna wananji bila white house kujua? Bila wale jamaa wa makirikiri kujua? Kule bungeni kwenye kura za ndiyoooooooo zilikuwa za hivi hivi? Ni kweli jamani? Hebu tuache unafiki tujifunze kuita a spoon a spoon
 
Magu kasema waende huko ICSID halafu warudi tena kama watachimba Madini.Utachimbaje madini Bila ulinzi
Kwahiyo wakienda wakashinda kesi na ukawalipa mabilioni wakaamua kufunga mgodi wanapata hasara gani??? Kwani kabla hawajaitwa ACACIA si walikuwa na jina jingine na walikuwa wanatuibia kama kawa????? Wataondoka ila watarudi kwa jina jingine na kuendelea kutunyoosha

Na je tukishindwa kesi magu yupo radhi kujiuzulu kwa kuingiza nchi kwenye hasara ama mzigo tutaubeba sisi???? kwa wachina si alisema hivi hivi hadi akaishia kuzigawa samaki zao ila tulilipishwa bila kupenda

Kaz kwelikweli
 
Wanajitoa ufahama hawa .... afu mbona hawakanushi vyote!! mbona hawasemi kama ni kweli hawajasajiliwa + plus mambo mengine mengi ambayo yameongelewa kwenye ripoti! nilitegemea labda wangetoa jibu moja badala ya jingine kama ripoti inavosema matokeo yake wana copy na ku paste statement ngonjera zao zile zile wanazozisema siku zote!!

Hawa ni wa kufilisi tu na waondoke nchini.
wasubiri yule mwanasheria wa miga aje awatetee
 
Mikataba yote iwekwe wazi na wahusika wote wachukuliwe hatua sio waliotajwa kwenye taarifa hiyo kuna watu anawaficha huyu rais sijui vipi na watu wakisema hili atasema wanaropoka
Mikataba yote itizamwe tuna migodi zaidi ya kumi amewataja watu watano tu hao wengine je? ukitaka kuwa mkweli kuwa mkweli asilimia 100 ili watu wakusupport kama kusamehe samehe wote
 
Kuna aliyetegemea kusikia kitu tofauti kutoka kwao
Mwizi hata ukimkuta eneo la tukio anaiba lazima atabisha tu
 
eti anauliza nani alietuloga...huyu jamaa bana ilitakiwa aulize nani aliewaroga ccm mana wakati wanapitisha hii mikataba yot
 
Back
Top Bottom