ACACIA wapinga vikali Matokeo ya Kamati ya pili ya Rais

Kuwa na akili huru, penda kusikia hata yale yanayopingana na imani, itikadi na misimamo yako. Kuuliza uzawa/utanzania kwa misingi tu utofauti wa kufikiri ni ujuha wa kiwango cha reli standard gauge.
Inawezekana hupo Serious na ulichoandika. Hatahivyo kwakuwa umeandika mambo ya Utanzania na pia umetaja ujuha basi nitakuuliza maswali kidogo.

Je, Unafahamu kinachongumziwa?
Je, unaelewa kinachozungumziwa?
Je, mleta mada Unadhani ana elewa?

Unaelewa kwanini nilimuuliza mleta mada swali hilo?

Nini maoni yako juu ya sakata la sasa.

Dhihirisha kuwa mimi ni JUHA lakini wewe siyo JUHA kwa kujibu maswali hayo.
 
Jmn jmn tafadharini sana tena sana hakuna kitu inayoitwa Acacia kisheria mpaka sasa kwa ishu yoyote inayohusiana na Acacia ni haramu kisheria, wala hatutakiwi kujadili, kwa hiyo kama mchanga uliozuiliwa ni Wa Acacia basi kimsingi huo ulikuwa unaibiwa na jizi linalojiita Acacia na ni lazima atueleze kauiba wapi na kwa maoni yangu management ya Acacia toka jana walitakiwa wawe lock up tayari kwa kupandishwa mahakamani.
 
Nilitegemea Acacia wangeanza na kututhibitishia kwamba wao wako kisheria, hiyo ndio ingekuwa hoja naomba moja kabla ya blabla nyingine hizi
 
12 Juni 2017
Mwitikio wa Acacia kwenye matokeo ya kamati ya pili ya Rais

Acacia imeona matokeo ya kushtua ya kamati ya pili ya Rais iliyowasilishwa kwa Rais wa Tanzania Mh. Dk John P. Magufuli leo asubuhi ambayo imeangalia nyanja za historia za kiuchumi na kisheria ya mauzo ya nje ya makanikia ya madini.

Kamati ya Pili imetoa matokeo yake kwa kutumia matokeo ya Kamati ya Rais ya Kwanza, iliyotangazwa tarehe 24 Mei 2017, ambayo Acacia imeikanusha vikali. Kamati hiyo ilipata matokeo yake kwa kutumia sampuli ya kontena 44. Kwa mujibu wa data za zaidi ya miaka 20 tulizonazo ni vigumu kuoanisha matokeo yetu na yaliyokutwa na kamati, na kamati imetoa thamani ya juu kwa zaidi ya mara 10 kuliko thamani halisi ya makanikia

Kamati ya Pili inadai kuwa Acacia imetangaza kiasi cha chini cha mapato kuliko inavyopata na kulipa kodi kidogo kuliko inavyostahili kwa miaka mingi na kuficha mabilioni ya dola ya Marekani. Na hivyo imefanya mapendekezo kadhaa ikiwa ni pamoja na Acacia kulipa kodi inayodaiwa na mirahaba, kufanya majadiliano upya ya mikataba mikubwa ya uchimbaji madini, umiliki wa Serikali katika migodi, na muendelezo wa marufuku ya kuuza nje.

Acacia inakanusha vikali tuhuma hizi mpya zisizo na ushahidi. Sisi tumefanya biashara zetu kwa utaratibu bora kabisa na kwa kufuata sheria zote za Tanzania. Tunarudia kusema tena tumeweka wazi kila kitu chenye faida tulichokuwa tunazalisha tangia tuanze uchimbaji Tanzania na tumelipa kodi na mirabaha yote inayotakiwa kulipwa, na kwa kuongezea mahesabu yetu tunayotoa yanakaguliwa kila mwaka kwa viwango vya kimataifa vinavyoendana na IFRS.

Acacia kwa muda mrefu tulitaka kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuwa tunaamini wote tuna malengo sawa katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Hata hivyo, ushirikiano huu lazima uwe na misingi ya haki kwa wadau wote, ikiwa ni pamoja na 96% ya wafanyakazi katika migodi yetu ambao ni Watanzania, na wanahisa wetu ambao wamechangia dola bilioni 4 za uwekezaji ambazo Acacia imefanya ndani ya nchi hadi sasa.

Acacia bado inakaribisha mazungumzo na Serikali kuhusu suala hili na inaendelea kutathmini nini inaweza kufanya . Tutatoa taarifa zaidi kwa soko kadri tutakavyoweza kufanya .

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu
www.acaciamining.com


=================================

1
LSE:ACA www.acaciamining.com
12 June 2017
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION
Acacia Mining plc
LSE:ACA
(“Acacia” or the “Company”)
Update on the 2nd Presidential Committee Findings
Acacia notes the disappointing findings of the Presidential Second Committee’s report which were presented to the President of Tanzania H.E. Dr. John P. Magufuli this morning and which considered the historical economic and legal aspects of the export of metallic mineral concentrates.

The Second Committee has primarily based its findings on those of the First Presidential Committee, announced on 24 May 2017, that Acacia strongly refutes. That Committee based its findings on samples from 44 containers. Based on more than 20 years of data available to us it is impossible to reconcile those findings and they grossly overstate the value of the concentrates by more than 10 times.

The Second Committee has alleged that Acacia has under-declared revenues and tax payments over a number of years by tens of billions of US dollars. As a result it has made a series of recommendations including the payment of outstanding taxes and royalties, re-negotiation of large-scale Mineral Development Agreements, Government ownership in the mines, and the continuation of the export ban.

Acacia strongly refutes these new unfounded accusations. We have always conducted our business to the highest standards and operated in full compliance with Tanzanian law. We re-iterate that we have declared everything of commercial value that we have produced since we started operating in Tanzania and have paid all appropriate royalties and taxes on all of the payable minerals that we produce. In addition, our published accounts are annually audited to an international standard in accordance with IFRS.

Acacia has long sought to be a partner with the Government of Tanzania as we believe that we have similar goals in enhancing social and economic development in the country. However, this partnership must be based on fairness for all stakeholders, including the 96% of our employees at our mines who are Tanzanian, and our shareholders who have funded the US$4 billion of investment that Acacia has made into the country to date.

Acacia remains open to further dialogue with the Government regarding this issue and continues to assess all of its options. We will provide a further update to the market as soon as practical.

ENQUIRIES
For further information, please visit our website: www.acaciamining.com or contact us
Acheni maneno weka certificate ya usajili wa Acacia kwanza, ili tuendelee na hoja nyingine.
 
Yaaan wanawaona wanao kosoa kama ndio walio ingia hyo miktaba hawajui waliyo yashangilia na kuyapitisha wao wenyewe ndio sasa wanayaona kama sio makosa yao, kuna watu wanakwaza sana Acasia wanakosa gani sasa mjibie wenyewe alafu mlaumu wazungu
kuna watu nchi hii wanatengeneza matatizo wao wenyewe afu wanajifanya kuyatatua kwa kutafuta kick za kisiasa..
 
Hawa jamaa wanapinga utafiti wetu wanasema hauna ushahidi wa kutosha wakati wao hawajaweka hadharani ushahidi wao wanaodai unatosheleza sasa hapa mbona wanatuacha mataani?
 
Sasa hao WASOMI tena maprofessor wasioropoka kma muhongo kafumu sijui chenge ambao walitajwa kwenye ripoti ya jana je hao mbona hamuwatolei povu humu???

Hivi kweli mjadala umehama mnamjadili lisu ila mnaacha kujadili kafumu na kina yona waliotufikisha hapa tulipo????

Maendeleo tutayasikia kwenye bomba
Wewe ndio maendeleo utayasikia kwenye bomba, wenzio tunasonga, nafikiri news unazipata vyema, endelea na lissu ziro wako!
 
Wewe ndio maendeleo utayasikia kwenye bomba, wenzio tunasonga, nafikiri news unazipata vyema, endelea na lissu ziro wako!
Hahahhahahaha maendeleo kwani umeskia nategemea msahahara wa serikali au chadema ili niendeshe maisha yangu???? Nina maisha yangu and am contented sasa maendeleo gani hayo ambayo ntayasikia kwenye bomba???

Shida yangu mjadala umehama kutoka kwa ripoti ya makinikia eti kumjadili lisu lazma nishangae!! Kwamba kivp tunaacha kujadili wezi waliotajwa kwenye ripoti ya usoro eto tunaanza kujadili maoni ya lisu

Kwa staili hii viwanda mtavisikia kwenye redio na nakuhakikishia hao kufkia 2020 hakuna hta kiwanda kimoja kitakuwa kimejengwa!
 
Sijaona details nyingi za taarifa ya pili, hivyo nahisi ni kadirio kwenye msingi wa taarifa ya kwanza. Taarifa hii bado nashindwa kuiamini eti walificha mara kumi kiasi cha dhahabu au mengine jinsi walivyodeclare. Maana naweza kuamini kabisa makampuni haya wanadanganya, na maafisa wa hapa wanahongwa ILA TU:
Makapuni haya ni makampuni ya hisa kwenye masoko mbalimbali ya kimataifa.
KAMA kweli wangechimba dhahabu nyingi kama vile taarifa ya kwanza ilivyodai basi pia faida yao ingekuwa mara kadhaa jinsi walivyotangaza.

Hapa siwezi kuamini ya kwamba wangeweza kudanganya hao mabepari wote wenye hisa zao kimataifa ambao wangestahili kupata asilimia yao ya faida halisi sawa na hisa wanazoshika. Hapa sioni dalili yoyote. Nani anaamini mbepari anaweka pesa katika hisa za Acacia halafu hataki kuona asilimia yake???

nani anaamini hao wangeweza kuficha profits (kama ni mara 10) kuwa siri?? Na kuficha profits ni jinai kote duniani, si Tanzania tu. Sheria kali kimataifa.

Hapo sababu sina imani bado katika utafiti wa kwanza hadi maabara mengine (yasiyo na athira za kisiasa) yarudie vipimo. Baadaye jambo la kupiga hesabu kwenye msingi uliokubalika.
 
Back
Top Bottom