ACACIA wapinga vikali Matokeo ya Kamati ya pili ya Rais

ACACIA wapinga vikali Matokeo ya Kamati ya pili ya Rais

Hatua zilizochukuliwa
1. Hatua ya JPM kusitisha mchanga kwenda nje kwa ajili ya uchunguzi ni sahihi.
2. Report ya kwanza na Mapendekezo yake ni sahihi.
3.Report ya pili na Mapendekezo yake ni sahihi pia.

Mkakati ya Team JPM
Hatua zote tatu ni sahihi kwasababu alichofanya JPM sio kuvunja mkataba au kuzuia moja kwa moja usafilishaji wa mchanga bali ni strategy za kuwafanya ACACIA warudi kwenye meza ya majadiliano wakiwa hawana confidence kwa kudai share kubwa ukilinganisha kama wangeitwa bila JPM kutengeneza Cheos, kwahiyo uundaji wa tume zote mbili pamoja na ya Tatu ambayo alisema yeye mwenyewe haijui ni mpango mkakati wa kutengeneza room nzuri ya negotiation ili apate faida kama nilivyoanisha hapo chini.
Kumbukeni kamati ya bunge ilishawahi kupitia sera na mikataba ya madini wakaishia kuambulia mabadiliko madogo sana.

Faida ya kutengeneza mtafaruku
1.JPM atakuwa na evidence ya uwizi wanaofanya wakati wa majadiliano mapya
2. JPM atakuwa anajua na ataenda na share anayoitaka kuidai kwenye meza ya majadiliano
3. Hata kama ACACIA wanabebwa na baadhi ya vipengele kwenye mkataba, watakuwa hawana confidence ya kudai share kubwa kutokana na Guilty Consciousness baada ya kuvuliwa taulo.
4.JPM atakuwa na room ya kudai share nyingi hadi kwenye pure gold mbali na makinikia
5.JPM atapata room kubwa ya kureview mikataba ya madini na gas kama ambavyo ameshaagiza kwasababu wawekezaji watamuona yuko serious tofauti na waliopita.
6.Kulingana na mazingira na ukweli uliojulikana, ni ngumu kwa ACACIA kwenda mahakamani, watataka hili swala liishie mezani. Kwahiyo habari ya ACACIA kwenda mahakamani sahauni.

Toafuti ya JPM na Lissu kimkakati

1.JPM aliamua kutengeneza mgogoro ili apate faida nilizo hainisha hapo juu na zitampa faida-Best Approach.
2.Lissu alitaka tuilete mikataba bungeni kwa ajili ya marekebisho, akaiponda aproach ya JPM-Weak Approach

Kwanini JPM yuko sahihi

Mikataba itakavyorudishwa bungeni kujadiliwa JPM atakuwa na evidence, na watajadili kulingana na evidence na Loop holes zilizoainishwa na kamati zote.

Kwanini Lissu hayuko sahihi sana

Approach yake ingesababisha bunge kujadili mikataba Blindly bila evidence yoyote hivyo serikali kuambilia kiduchu kama kamati ya akina Zitto.

Dhamira
Lissu anadhamira nzuri kama JPM, ila kwenye hili wamenzidi ujanja kweye approach ataonekana kama msaliti wakati siyo msaliti, na wanamchafua kwa kunakili mistari michache na mifupi kwenye hoja zake ili waonyeshe ni msaliti.


Hitimisho
JPM amejipanga kwenye hili swala na ndiyo maana kwenye conclusion yake aliwaita ACACIA kwenye majadiliano, na kabla ya kuwaita aliwapiga mkwara kama wataenda kumshtaki hawatachimba madini Tanzania, na unajua madini yamebaki nchi chache duniani, huamuzi wa kuondoka jumla utakuwa ni mgumu.

Hayo ndiyo maoni yangu.
Nimependa uchambuzi wako. Ni kunyangsnyana fito tu
 
Naona kila upande unamtegea mwenzie unasema upo tayari kwa majadiliano. Sasa hapa kama una akili utajiuliza maswali mengi. Wa kwanza alie ibiwa anadai chake lakini hamfikishi mahakamani mwizi wake, na yule alietuhumiwa kuiba na kuzuiliwa mali zake na kusababisha kuchafuliwa ambapo hisa zake zimeporomoka kwa kiasi kikubwa nae hataki kumshitaki aliemchafulia jina, aliemuingiza hasara ya hisa na bidhaa zake zilizoshikiliwa nae anasema yupo tayari kwa majadiliano. Kuna alama kubwa sana ya kuuliza na ya mshangao ambazo hazionekani ni za kufikirika ambazo hazionekani kwa macho zinahitaji majibu ya kufikirika.
Tatizo ni wachache sana wanaoweza kutafakari namna hii. Wengi tunapiga makofi na vigelegele.
 
Nishasemaga mim kua kama kweli magu anania njema basi afukue kabisa makaburi.hili jambo hili liishe hakutakiwi kusalia jiwe juu ya jiwe.sasa mim ngoja nikae mkao kuona wanavyovuana nguo.Hiyo inaitwa wao kwa wao.
 
Tatizo JPM anatenda kwa imani na hisia! Sijui ingekuwaje leo kamati ingesema tofauti na imani na hisia hizo!

Kama lipo tatizo ni vigumu sana kuwapata katika meza huru! Waliotuangusha ni viongozi wetu, watendaji wetu , wanasheria wetu na wabunge wetu! Hawakutafakari walichoamua na hawakuamua walichotafakari!
Hapo kwenye wabunge na yeye alikuwemooo
 
Mazungu majizi sana pumbav zao....yanakuja kuchukua rasilimali zetu...yanatumia udhaifu wa baadhi ya viongozi wetu....yanatucheka.....rais wangu kaza uzi.....hatutaki wevi...
 
Hawa acacia nimajizi wakubwa wala ss wapinzani tusibadilikebadilike kama kinyonga haya majitu yametuibia sana nakama kuna mpinzani anawatetea hawa jamaa basi nibola nikaacha siyasa hakunahaja nakuwa nawatu wanaojiita wapinzani nawakati niwachumia tumbo
 
Tatizo JPM anatenda kwa imani na hisia! Sijui ingekuwaje leo kamati ingesema tofauti na imani na hisia hizo!

Kama lipo tatizo ni vigumu sana kuwapata katika meza huru! Waliotuangusha ni viongozi wetu, watendaji wetu , wanasheria wetu na wabunge wetu! Hawakutafakari walichoamua na hawakuamua walichotafakari!
Uko sahihi ndio maana magufuli anajaribu kudai haki kwa kupambana na watumishi wa serikali yake wasio waaminifu hali kadhalika acacia huu ni mwanzo mzuri tumeanguka sasa tunainuka tukiwa na kizunguzungu lkn tunajaribu kusimama na tutasimama ni kweli wabunge wa ccm wametuangusha lkn Je tuendelee kulia kulia bila kujirekebisha?
 
Naona kila upande unamtegea mwenzie unasema upo tayari kwa majadiliano. Sasa hapa kama una akili utajiuliza maswali mengi. Wa kwanza alie ibiwa anadai chake lakini hamfikishi mahakamani mwizi wake, na yule alietuhumiwa kuiba na kuzuiliwa mali zake na kusababisha kuchafuliwa ambapo hisa zake zimeporomoka kwa kiasi kikubwa nae hataki kumshitaki aliemchafulia jina, aliemuingiza hasara ya hisa na bidhaa zake zilizoshikiliwa nae anasema yupo tayari kwa majadiliano. Kuna alama kubwa sana ya kuuliza na ya mshangao ambazo hazionekani ni za kufikirika ambazo hazionekani kwa macho zinahitaji majibu ya kufikirika.
Sio kila suluhu lazima ipatikane mahakamani hata mkielewana wenyewe ni suluhu tosha.
 
Hata raisi ametoa nafasi ya Dialogue.
Lakini nadhani wajitokeze tu kuwa walikuwa wanatupiga kiasi gani na wako tayari kutu lipa.


Hii ni kama EPA tu...wezi walipewa msamaha na waambiwa warudishe hela yaishe...leo Acacia nao wameambiwa wakubali kukaa kwenye meza ya mazungumzo na mambo yataisha.

Nadhani hatutakaa tuambiwe hayo mazungumzo yameishaje na ni muafaka gani umefikiwa.

Wezi wa budget ya miaka mitatu ya 31tr+/yr na change ya kujenga SGR dar mwanza unawataka kukaa nao meza moja...haya maajabu utayashuhudia Tanzania pekee.
 
Sasa hapa nani mkweli?? Serikali inataka chao ila ACACIA wanadai hawadaiwi?? Nahisi kma ICSID inanukia ili ukweli ujulikane
Mkuu mbona hawajakanusha kuwa mchanga wote ule wa makontena 250 umeshauzwa na wamechukua chao kinyume na madai yao kuwa mchanga unaenda kuchenjuliwa kwanza.
Hawa watu sio wa kuwaamini nyie,tokea walipogushi hesabu TRA ili walipe corporate tax ya chini.halafu London stock exchange wakapeleka hesabu za juu ili kupandisha bei ya hisa,nimewaona ni wezi tu.
Sasa hivi wataanza kupanguana najua makampuni dizaini hii
 
Hakuna anyewatetea ACACIA,wala makampuni mengine,tunachosema tufuate sheria ili tuweze kuwashinda,kwa kukurupuka hatufiki hata posta.

Tusifanye kazi kama punguani tufanye kazi kwa umakini.Waliotuangusha wala siyo Lissu,kama Lissu angesikilizwa miaka 17 iliyopita leo kusingekuwa na haya madubwana.

Kwangu mimi Lissu is my hero
Ni kweli hakusikilizwa makosa yamefanyika kwahiyo hatuna nafasi ya kureview? Kwanini tusijipongeze kwa kuamua kumsikiliza lissu na wengine badala ya kuendelea kulaumiana?
 
Mkweli atapatikana ila nadhani kamati zimesema ukweli, Haikua na haja YA ndege kutua na kuruka migodini huko huko na vile vile Kwanini wazuie watanzania kuingia huko nawaza tu!
 
Tatizo JPM anatenda kwa imani na hisia! Sijui ingekuwaje leo kamati ingesema tofauti na imani na hisia hizo!

Kama lipo tatizo ni vigumu sana kuwapata katika meza huru! Waliotuangusha ni viongozi wetu, watendaji wetu , wanasheria wetu na wabunge wetu! Hawakutafakari walichoamua na hawakuamua walichotafakari!
Wewe na magu nani mwenye access yakujua ukweli na unahisi suala kama ili akapoteza muda kwa kudanganya watu?
 
NILITEGEMEA 100 % YA LAWAMA RAIS AZIELEKEZE KWA MKAPA, KIKWETE ,WABUNGE WA CCM AKIWAPO YEYE NA WATENDAJI WENGINE WHO WERE KEY S TO THE DECISIONS OF THIS ROBERRY BACK THEN. cha ajabu rawama za hasira kazimalizia kwa TL. Shida ya hii inchi ni mi CCM
Inawezekana ikawa kweli lkn hakuna mbadala wa ccm kwa sasa.
 
Acacia bado inakaribisha mazungumzo na Serikali kuhusu suala hili na inaendelea kutathmini nini inaweza kufanya . Tutatoa taarifa zaidi kwa soko kadri tutakavyoweza kufanya .
Tunataka chetu kwanza halafu ndio mengine yaendelee
 
Back
Top Bottom