ACACIA wapinga vikali Matokeo ya Kamati ya pili ya Rais

ACACIA wapinga vikali Matokeo ya Kamati ya pili ya Rais

Wanatathmini nini cha kufanya sio? Jamaa wamepuzzle... kimenukaaaaa..... kama nini wakubali tu waombe wapunguziwe deni.... wakiendelea na ubishi watajichongea. Mana tangu ripoti ya mwanzo wao hawajajitathmini nini cha kufanya. Hawana plan kabisa!
 
Siku zote mtuhumiwa huwa hakubali, mbona hawajakanusha kuwa hawajajisajili?

Wana haki ya kukanusha ili wasije onekana waovyo na kudaiwa zaidi kufanya kazi kinyume na sheria.

Ila pia niwaombeni watanzania huu ndio muda wa kuweka itikadi zetu pembeni na kujadili maslahi ya taifa
 
12 Juni 2017
Mwitikio wa Acacia kwenye matokeo ya kamati ya pili ya Rais

Acacia imeona matokeo ya kushtua ya kamati ya pili ya Rais iliyowasilishwa kwa Rais wa Tanzania Mh. Dk John P. Magufuli leo asubuhi ambayo imeangalia nyanja za historia za kiuchumi na kisheria ya mauzo ya nje ya makanikia ya madini.

Kamati ya Pili imetoa matokeo yake kwa kutumia matokeo ya Kamati ya Rais ya Kwanza, iliyotangazwa tarehe 24 Mei 2017, ambayo Acacia imeikanusha vikali. Kamati hiyo ilipata matokeo yake kwa kutumia sampuli ya kontena 44. Kwa mujibu wa data za zaidi ya miaka 20 tulizonazo ni vigumu kuoanisha matokeo yetu na yaliyokutwa na kamati, na kamati imetoa thamani ya juu kwa zaidi ya mara 10 kuliko thamani halisi ya makanikia

Kamati ya Pili inadai kuwa Acacia imetangaza kiasi cha chini cha mapato kuliko inavyopata na kulipa kodi kidogo kuliko inavyostahili kwa miaka mingi na kuficha mabilioni ya dola ya Marekani. Na hivyo imefanya mapendekezo kadhaa ikiwa ni pamoja na Acacia kulipa kodi inayodaiwa na mirahaba, kufanya majadiliano upya ya mikataba mikubwa ya uchimbaji madini, umiliki wa Serikali katika migodi, na muendelezo wa marufuku ya kuuza nje.

Acacia inakanusha vikali tuhuma hizi mpya zisizo na ushahidi. Sisi tumefanya biashara zetu kwa utaratibu bora kabisa na kwa kufuata sheria zote za Tanzania. Tunarudia kusema tena tumeweka wazi kila kitu chenye faida tulichokuwa tunazalisha tangia tuanze uchimbaji Tanzania na tumelipa kodi na mirabaha yote inayotakiwa kulipwa, na kwa kuongezea mahesabu yetu tunayotoa yanakaguliwa kila mwaka kwa viwango vya kimataifa vinavyoendana na IFRS.

Acacia kwa muda mrefu tulitaka kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuwa tunaamini wote tuna malengo sawa katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Hata hivyo, ushirikiano huu lazima uwe na misingi ya haki kwa wadau wote, ikiwa ni pamoja na 96% ya wafanyakazi katika migodi yetu ambao ni Watanzania, na wanahisa wetu ambao wamechangia dola bilioni 4 za uwekezaji ambazo Acacia imefanya ndani ya nchi hadi sasa.

Acacia bado inakaribisha mazungumzo na Serikali kuhusu suala hili na inaendelea kutathmini nini inaweza kufanya . Tutatoa taarifa zaidi kwa soko kadri tutakavyoweza kufanya .

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu
www.acaciamining.com


=================================

1
LSE:ACA www.acaciamining.com
12 June 2017
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION
Acacia Mining plc
LSE:ACA
(“Acacia” or the “Company”)
Update on the 2nd Presidential Committee Findings
Acacia notes the disappointing findings of the Presidential Second Committee’s report which were presented to the President of Tanzania H.E. Dr. John P. Magufuli this morning and which considered the historical economic and legal aspects of the export of metallic mineral concentrates.

The Second Committee has primarily based its findings on those of the First Presidential Committee, announced on 24 May 2017, that Acacia strongly refutes. That Committee based its findings on samples from 44 containers. Based on more than 20 years of data available to us it is impossible to reconcile those findings and they grossly overstate the value of the concentrates by more than 10 times.

The Second Committee has alleged that Acacia has under-declared revenues and tax payments over a number of years by tens of billions of US dollars. As a result it has made a series of recommendations including the payment of outstanding taxes and royalties, re-negotiation of large-scale Mineral Development Agreements, Government ownership in the mines, and the continuation of the export ban.

Acacia strongly refutes these new unfounded accusations. We have always conducted our business to the highest standards and operated in full compliance with Tanzanian law. We re-iterate that we have declared everything of commercial value that we have produced since we started operating in Tanzania and have paid all appropriate royalties and taxes on all of the payable minerals that we produce. In addition, our published accounts are annually audited to an international standard in accordance with IFRS.

Acacia has long sought to be a partner with the Government of Tanzania as we believe that we have similar goals in enhancing social and economic development in the country. However, this partnership must be based on fairness for all stakeholders, including the 96% of our employees at our mines who are Tanzanian, and our shareholders who have funded the US$4 billion of investment that Acacia has made into the country to date.

Acacia remains open to further dialogue with the Government regarding this issue and continues to assess all of its options. We will provide a further update to the market as soon as practical.

ENQUIRIES
For further information, please visit our website: www.acaciamining.com or contact us
Watupe chetu mapema
 
Hakuna anyewatetea ACACIA,wala makampuni mengine,tunachosema tufuate sheria ili tuweze kuwashinda,kwa kukurupuka hatufiki hata posta.

Tusifanye kazi kama punguani tufanye kazi kwa umakini.Waliotuangusha wala siyo Lissu,kama Lissu angesikilizwa miaka 17 iliyopita leo kusingekuwa na haya madubwana.

Kwangu mimi Lissu is my hero
Ingekua vizuri basi unatoa maoni yake, serikali iltakiwa ichukue hatua gani? Sio tu useme ifuatwe sheria, taja hizo sheria unazojua.
 
Hatua zilizochukuliwa
1. Hatua ya JPM kusitisha mchanga kwenda nje kwa ajili ya uchunguzi ni sahihi.
2. Report ya kwanza na Mapendekezo yake ni sahihi.
3.Report ya pili na Mapendekezo yake ni sahihi pia.

Mkakati ya Team JPM
Hatua zote tatu ni sahihi kwasababu alichofanya JPM sio kuvunja mkataba au kuzuia moja kwa moja usafilishaji wa mchanga bali ni strategy za kuwafanya ACACIA warudi kwenye meza ya majadiliano wakiwa hawana confidence kwa kudai share kubwa ukilinganisha kama wangeitwa bila JPM kutengeneza Cheos, kwahiyo uundaji wa tume zote mbili pamoja na ya Tatu ambayo alisema yeye mwenyewe haijui ni mpango mkakati wa kutengeneza room nzuri ya negotiation ili apate faida kama nilivyoanisha hapo chini.


Faida ya kutengeneza mtafaruku
1.JPM atakuwa na evidence ya uwizi wanaofanya wakati wa majadiliano mapya
2. JPM atakuwa anajua na ataenda na share anayoitaka kuidai kwenye meza ya majadiliano
3. Hata kama ACACIA wanabebwa na baadhi ya vipengele kwenye mkataba, watakuwa hawana confidence ya kudai share kubwa kutokana na Guilty Consciousness baada ya kuvuliwa taulo.
4.JPM atakuwa na room ya kudai share nyingi hadi kwenye pure gold mbali na makinikia
5.JPM atapata room kubwa ya kureview mikataba ya madini na gas kama ambavyo ameshaagiza kwasababu wawekezaji watamuona yuko serious tofauti na waliopita.
6.Kulingana na mazingira na ukweli uliojulikana, ni ngumu kwa ACACIA kwenda mahakamani, watataka hili swala liishie mezani. Kwahiyo habari ya ACACIA kwenda mahakamani sahauni.

Toafuti ya JPM na Lissu kimkakati

1.JPM aliamua kutengeneza mgogoro ili apate faida nilizo hainisha hapo juu na zitampa faida-Best Approach.
2.Lissu alitaka tuilete mikataba bungeni kwa ajili ya marekebisho, akaiponda aproach ya JPM-Weak Approach

Kwanini JPM yuko sahihi

Mikataba itakavyorudishwa bungeni kujadiliwa JPM atakuwa na evidence, na watajadili kulingana na evidence na Loop holes zilizoainishwa na kamati zote.

Kwanini Lissu hayuko sahihi sana

Approach yake ingesababisha bunge kujadili mikataba Blindly bila evidence yoyote hivyo serikali kuambilia kiduchu kama kamati ya akina Zitto.

Dhamira
Lissu anadhamira nzuri kama JPM, ila kwenye hili wamenzidi ujanja kweye approach ataonekana kama msaliti wakati siyo msaliti, na wanamchafua kwa kunakili mistari michache na mifupi kwenye hoja zake ili waonyeshe ni msaliti.


Hitimisho
JPM amejipanga kwenye hili swala na ndiyo maana kwenye conclusion yake aliwaita ACACIA kwenye majadiliano, na kabla ya kuwaita aliwapiga mkwara kama wataenda kumshtaki hawatachimba madini Tanzania, na unajua madini yamebaki nchi chache duniani, huamuzi wa kuondoka jumla utakuwa ni mgumu.

Hayo ndiyo maoni yangu.

Maoni yako ni mazurii..
Na umeongea kisomi/muelewa..
Bora uwasaidie wale mapopoma wanaopiga vigelegele pasipokujua hoja ni nini na mkazo hasa upo wapii..
"Kumbukeni kamati ya bunge ilishawahi kupitia sera na mikataba ya madini wakaishia kuambulia mabadiliko madogo sana." nikikunukuu hapa hili jambo silo geni kwa wafatiliaji mambo ya msingi na sio wale washangiliaji
 
Yaaan wanawaona wanao kosoa kama ndio walio ingia hyo miktaba hawajui waliyo yashangilia na kuyapitisha wao wenyewe ndio sasa wanayaona kama sio makosa yao, kuna watu wanakwaza sana Acasia wanakosa gani sasa mjibie wenyewe alafu mlaumu wazungu
Honestly watu nyinyi mnaniudhi sana!!! Sasa hoja yako ni nini? Kwakuwa watu wa chama tawala wa wakati huo walifanya makosa, basi makosa hayo yasirekebishwe?! Je huko upinzani si kuna lundo la former potential CCM members. Waliokuwa nafasi za juu serikalini. Waliopitisha mikataba hii. Sasa unatupaje lawama kwa CCM.

Hapa cha msingi tushughulike na wote waliohusika bila kujali wapo chama gani. Kama wapo CCM ama upinzani wawajibike.
 
Naona kila upande unamtegea mwenzie unasema upo tayari kwa majadiliano. Sasa hapa kama una akili utajiuliza maswali mengi. Wa kwanza alie ibiwa anadai chake lakini hamfikishi mahakamani mwizi wake, na yule alietuhumiwa kuiba na kuzuiliwa mali zake na kusababisha kuchafuliwa ambapo hisa zake zimeporomoka kwa kiasi kikubwa nae hataki kumshitaki aliemchafulia jina, aliemuingiza hasara ya hisa na bidhaa zake zilizoshikiliwa nae anasema yupo tayari kwa majadiliano. Kuna alama kubwa sana ya kuuliza na ya mshangao ambazo hazionekani ni za kufikirika ambazo hazionekani kwa macho zinahitaji majibu ya kufikirika.
Great thinker
 
It seems you are heavily affected by CHADEMAISM and CCMISM politics,read carefully and keenly between the lines do not rush to comment without thinking big.Listen once again the President speech and then compare with the last paragraph of your friend's ACACIA statement.Have a nice day!
I entirely agree with you mkuu, jamaa kakurupuka akusoma paragraph za mwisho za acacia. Amekimbilia kuchangia ki politics
 
Mwizi unamkamata na kithibiti Ila bado anakataa kuwa yeye siyo mwizi.

Hiyo ni kawaida ya wezi wote, awe amesoma, hajasoma, mwafrika ama mzungu koko.

Wezi wote , wanatabia moja ya kukataa kuwa siyo wezi.

Ngojeeni, utaoneni hata waliotajwa na rais kwa kushirikiana na wezi utaona majibu na porojo zao.
 
hivi kwa nini tusiwashitaki kwenye Maahakama za Kimataifa?na kama za kimataifa tunashindwa kwa nini tusiwashitaki kwenye Mahakama zetu?
 
Asome hii kwa makini
Acacia remains open to further dialogue with the Government regarding this issue and continues to assess all of its options. We will provide a further update to the market as soon as practical.
Alikurupuka tu akusoma kabisa mkuu
 
Sumaye ndo alikua PM. Alisha jinasibu kua yeye ilikua ndo kila kitu wakati wa BM.
[emoji1] [emoji2] akikujibu ni tag mkuu.
Wana kamsemo fulani eti magu si alikuwepo lakini awataki kusema Lowassa,mahanga, Sumaye walikuwepo pia.
 
Magufuli hili kasha limaliza.... Sijui hawa acacia wanataka nin tena au wanataka Magufuli atoe report ya 3?

Hawa ACACIA ni kuwatimua hapa nchini hawa wezi.....
 
Naona kila upande unamtegea mwenzie unasema upo tayari kwa majadiliano. Sasa hapa kama una akili utajiuliza maswali mengi. Wa kwanza alie ibiwa anadai chake lakini hamfikishi mahakamani mwizi wake, na yule alietuhumiwa kuiba na kuzuiliwa mali zake na kusababisha kuchafuliwa ambapo hisa zake zimeporomoka kwa kiasi kikubwa nae hataki kumshitaki aliemchafulia jina, aliemuingiza hasara ya hisa na bidhaa zake zilizoshikiliwa nae anasema yupo tayari kwa majadiliano. Kuna alama kubwa sana ya kuuliza na ya mshangao ambazo hazionekani ni za kufikirika ambazo hazionekani kwa macho zinahitaji majibu ya kufikirika.
Umetoa hoja fikirishi sana. Mbona kila upande unaonyesha unyenyekevu? Hapa kuna tatizo la ndani zaidi kuliko tunavyo aminishwa
 
Hawawezi kukubali kirahisi kusema ss ACACIA tunatubu kuwa tuliwaibia watanzania kupindukia lazima Waje na mbinu za kukataa ili hata wakiomba uwekezaji nchi nyingine za kiafrika wapewe natamani wakirudisha hela za watz serikali isiwape hata hiyo leseni
 
Si mnaye mwanasheria nguli na mahiri kuliko wote Tanzania, Tundu Lissu? Mwazimisheni kwa Acacia awasaidie
Hayo ndiyo yanayo haribu mijadala ya kitaifa kwa kuweka upuuzi wa aina hii
 
Sumaye hawezi kuchomoka yeye na Mkapa, Tatizo tunaongopewa mtu akiwa upinzani basi amekuwa msafi.Wachafu wako pande zote pasipo kujali chama na wasafi wapo pande zote, Rais anania njema sana kwa watanzania ndio maana kaamua kufanya haya yote pasipokujali amefanya nani au yupo upand gani makosa madogodogo yatakuwepo ila tuangali faida tunayopata nchi.
Wachache watakuelewa na nakubaliana na wewe mkuu
 
Back
Top Bottom