Naona kila upande unamtegea mwenzie unasema upo tayari kwa majadiliano. Sasa hapa kama una akili utajiuliza maswali mengi. Wa kwanza alie ibiwa anadai chake lakini hamfikishi mahakamani mwizi wake, na yule alietuhumiwa kuiba na kuzuiliwa mali zake na kusababisha kuchafuliwa ambapo hisa zake zimeporomoka kwa kiasi kikubwa nae hataki kumshitaki aliemchafulia jina, aliemuingiza hasara ya hisa na bidhaa zake zilizoshikiliwa nae anasema yupo tayari kwa majadiliano. Kuna alama kubwa sana ya kuuliza na ya mshangao ambazo hazionekani ni za kufikirika ambazo hazionekani kwa macho zinahitaji majibu ya kufikirika.